Tarehe 21 mwezi wa 5 mwaka 1996 nilikuwa nna miaka kumi nimebakiza siku chache kutimiza miaka 11( I was born on May 31)
Nikiwa natoka shuleni ( nilikuwa darasa la tano) nakuta kuna watu wengi nyumbani, mama na Dada zangu wengine wakiwa wanalia kwa uchungu, hapo ndipo ninagundua imetokea ajali ya Mv Bukoba. Ndani ya ajali hiyo alikuwemo Dada yangu wa kwanza (first born she was ten years older than me) . Alikuwa amemaliza kidato cha Sita kwenye shule ya Secondary ya Rugambwa iliyopo mjini Bukoba.
Kibaya ama kizuri zaidi, hata mwili wake haukupatikana.. Nadhani eidha alikuwa vyumba vya juu au baba alishindwa kuutambua mwili wake.. .. Tukio hili sintolisahau maishani mwangu mpaka naondoka duniani. . Namhurumiaga Sana baba yangu mzazi ( Rest In Peace) kwa sababu alikuwa anaenda uwanja wa Nyamagana kila siku kutambua mwili wa marehemu binti yake but all in vain. ( pengine isingekuwa rahisi kwake kutambua mwili kwa sababu miili ya kwenye ajali ya maji huwa ina haribika vibaya)..
Kadri miaka inavyozidi kwenda ndio nina umia zaidi kwa sababu ndio ninazidi kuamini kwamba Dada yangu kweli alifariki kwenye ile ajali.
Toka huo mwaka 1996 nilikuwaga naamini kwamba huenda siku moja Dada yangu angerudi nyumbani ( nilikuwa nna assume labda aliokolewa na wavuvi etc " Wakamchukua" ( This was more pleasing to me to the extent that I wished it happened to her than her being gone : A man will always be willing to choose a lesser evil when he is faced with two evils with one to choose), lakini kila nikipiga hesabu za uwezekano wa jambo hilo la kuokolewa hesabu zinakuwa ngumu kwa sababu tukio lilitokea karibu kabisa na bandari ya Mwanza..( Hakuna visiwa karibu na eneo hilo)
( Nlikuwa najaribu kuidanganya akili yangu ikubali ama iamini kwamba Dada yangu labda aliokolewa na wavuvi Waka mchukua and then baadae she will escape and come home au wao wenyewe watamuachia atarudi nyumbani. Nilikuwa nagombana na ndugu Dada zangu kaka zangu baba na mama kwa kumrefer Dada angu kwa jina la marehemu na sijawahi kumrefer kama marehemu, huwa I talk about her as if she still living)
In fact nadhani my subconscious mind sensed my feelings and it decided to satisfy my feelings by giving me this experience through my dream. For at least 20 years since 96 ilikuwa Mara kwa Mara naota ndoto hii kwamba yupo nyumbani as if she was just travelled somewhere and now she is back)
Tukio hili lilinifanya nimkufuru Mungu ( kwanini alimpangia Dada yangu shule ya Bukoba. Mtu kamaliza Jangwani Secondary form mwaka 1993, selection form v unampeleka Rugambwa, Bukoba.Why? Kwanini usimpeleke hata hapo Kila Kala Morogoro basi kama umeshindwa kumpangia shule za Dar?) ( Niliamini Mungu ndo alipanga Dada angu kwenda kusoma Bukoba)
Na kwanini hakumzuia asipande meli siku hiyo hata kumpa homa ambayo ingefanya asipande meli siku hiyo? Au angemchelewesha angekuta tiketi zimeisha ( Hii ilitokea kwa Justin Kalikawe alikosa tiketi kwa sababu alikuta zimeisha kumbe ndio kaepuka na kifo) Au kwanini hakumuokoa kama alivyo waokoa wengine? ( Kuna Mzee mmoja alikuwa anahojiwa alisema yeye ni shati lake tu ndio lililowana )
Lakini kila nilipokua nikikumbuka mafundisho ya dini yanasema kazi ya Mungu haina makosa na kwamba yeye ndio ametoa na ndio ametwaa basi nikawa nabaki kuyaacha kama jinsi alivyo.. Nilikuwa sielewi kabisa kwanini Mungu aliona inafaa kwa Dada yangu yule ( a very nice ssiter, very hard working, very intelligent, very God fearing person who was like a de facto " second mother " to me to go down just like that?)
Tukio hilo lilinifanya nikamchukia Mzee wa Lupaso , mosi lilitokea ikiwa ndio kwanza akiwa ameingia madarakani na pili kulikua na tetesi zilikuwa zinasemwa Sana kuhusu tukio hilo na Mambo ya kafara huku akihusishwa yeye ( Nilimchukia kweli. Ila baadae nilikuja kuondoa Hilo wazo)
Tukio hilo lilinifanya niwe na phobia na usafiri wa maji. Siwezi wala sintowahi kwenda Zanzibar kwa sababu yoyote ile.
Kwenda Kigamboni tu huwaga mpaka nifanye " Auto hypnosis" Au niwe intoxicated.
Tukio hilo lilinifanya niuchukie mkoa wa Bukoba and anything related to it ( Hali hii ilikoma ten years later and in fact I had a girlfriend called Kokushobila- A very very Bukobianic girl though she was born in Dar, but prior to that it was so really)
Ilinifanya niwachukie watu wote kutoka mkoa wa Singida kwa sababu Captain Jumanne Rume Mwiru ( RIP) , nahodha wa MV Bukoba alikua mtu wa Singida, alitajwa kuwa chanzo cha uzembe ulio sababisha ajali kwa kuzidisha mizigo na abiria kuliko uwezo wa chombo ( Hali hii iliisha na nilikuja kumsamehe kabisa Captain Rume)
In fact : 10 years later nilienda Hadi Mwanza nyumbani kwa Captain Rume nikiwa na Sheikh wa Bakwata wa wilaya ya Mwanza : ( Nilikuwa introduced kwa Sheikh huyu wa wilaya ya Mwanza na sheikh mkuu wa Bakwata wilaya ya Kinondoni)
Nilienda nyumbani kwa Captain Rume kwenye Kota za wafanyakazi wa Marine na Railway ziliopo Kata ya Pamba jijini Mwanza ( Karibu na Igogo na kwa Bibi Fisi)
Nilimwambia jinsi nilivyo mchukia mwanzo lakini pia nimemsamehe ( Bahati mbaya au nzuri hilo tukio lilimuathiri kisaikolojia pakubwa sana and he was indeed a Semi- Psychiatric case at that time) Ila alinielewa.Alinisimulia version yake of what happened that morning and actually I understood it. He was himself very sorry and very regretting . Nikawa na urafikia na watoto wake Hadija, Hassan, Hidaya, Rehema na Haji pamoja na last born wake Mustafa.. Up to now they are still a family friend. The last time Hassan was Police Officer in Tanga, Hadija and Hidaya were Teachers.
Tukio hili pia limenifanya nisome vitabu vingi sana about all Arts and Science : ( Nilitaka kujua sababu iliyo mfanya mtu alie toa wazo ile meli itobolewe juu baada ya kuwa imepinduka)
Pia tukio hili limenifanya nione maisha ya duniani hayana thamani wala maana yoyote ile..
Duniani tumekuja kwa ajili ya kustarehe .Ndio maana huwa nashangaa Sana kuona mtu kama Lissu analoteza muda wake na nguvu zake kupambania haki za hapa duniani( samahani kwa nilio wakwaza kuhusu Lissu)
Duniani tumekuja kwa ajili ya kustarehe na kufurahia. Make sure you live your life to the fullest. Be happy to the maximum. U never know pengine hii ndio pepo yako. Never postpone your happiness
JINSI NINAVYO ADHIMISHA SIKU HII..
Huwa Nina anza saa tisa kamili alfajiri( Ajali ilitokea saa kumi alfajiri) nafanya maombi maalumu ya kumkumbuka then nafanya meditation .. Halafu siku nzima sili, sili kwa siku tatu mfululizo nakunywa maji tu usiku yani Leo, tarehe 22 na tarehe 23)
Kwanini nafanya hivyo?.. NINAJITESA PAMOJA NAE. NINAJITESA PAMOJA NA NAFSI YAKE. NINA AMINI ALIONDOKA KWA MATESO MAKUBWA SANA BOTH PHYSICALLY AND PSYCHOLOGICALLY ..
NINAPO JITESA PAMOJA NAE, NINA IPA NAFSI YANGU A MENTAL & PSYCHOLOGICAL SATISFACTION KWAMBA NINA/NIME SHARE PAMOJA NA DADA YANGU MATESO NA MAUMIVU ALIYO YAPATA KWENYE TUKIO HILO..
( Katika harakati za kutafuta kujua actually what happened to my sister when she learned that the ship was sinking and she would go down with it, nilisoma vitabu vingi sana vya science, psychology na matukio halisi kwenye Historia ambayo watu walikuwa katika situation kama hiyo - kwamba you know you are going to die. Nilijifunza kuhusu kitu kinaitwa adrenaline. ( I know you about it) Nilienda Rwanda kwenye museum ya Genocide nikanunua na kusoma kitabu kimoja ambacho kinaelezea personal stories za survivors wa genocide. Nilijifunza kitu kimoja kikubwa sana. Survivors wengi walikuwa wanasema " TULIKUWA HATUOGOPI TENA KUFA, TULIKUWA TUNAJUA TUTAKUFA TU, ISHU ILI KUWA TUTAKUFAJE KWA PANGA AU RISASI). Sababu kubwa ikiwa ni adrenaline zilikuwa more active at that time.
So nilijipa moyo kuwa huenda hata my sister and all other victims of this tragedy baada ya kujiridhisha kwamba now they are going to leave this planet, adrenaline hormones zikawa activated wakawa hawaogopi tena and probably wakaanza na kuimba nyimbo za kumsifu Mungu ( kwa wakristu) au dua za kumshukuru Mungu ( kwa waislamu) huku wakifurahi kwamba sasa wanaachana na dunia hii yenye kila aina ya uovu na kwenda kuishi kwa Mungu.
Butterfly Effect Is Real : Tulkio moja Dogo linaweza kuzalisha matukio elfu ishirini makubwa Mara Mia zaidi ya tukio Hilo dogo
REST IN PEACE MY LOVELY SISTER.
MAY THE ALMIGHTY GOD CONTINUE TO REST YOUR SOUL IN ETERNAL PEACE.
MAY THE SOULS OF ALL PEOPLE WHO PASSED AWAY IN MV BUKOBA TRAGEDY CONTINUE TO REST IN PEACE..
AMEN