Miaka 44 ya CCM inayoongoza nchi huku kikiwa kimekufa

Miaka 44 ya CCM inayoongoza nchi huku kikiwa kimekufa

Chagu wa Malunde

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
8,746
Reaction score
5,772
Jana chama cha mapinduzi kiliadhimisha miaka 44 tangu kianzishwe. Ni umri wa mtu mzima ambae anaenda kuzeeka.

Lakini CCM hii iliyoanzishwa wakati Mwl. Julius Nyerere akiwa mkuu wa nchi imebadilika. Maana sio ile ambayo watanzania tulizoea kuiona ikitetea, haki sawa kwa watanzania, kupinga ufisadi na kukemea viongozi wasiofaa kwa kuwavua na kuwafukuza uanachama.

Afadhali alipokuwepo Mwl Julius wanaCcm walikuwa na uoga wa kufanya madhambi maana yeye alikuwa hana msalie mtume. Leo hii chama CCM kimekuwa kama binadamu anayetembea lakini amekufa.

Mimi binafsi kama mtu nisiependa kuona mtu yoyote akivunja sheria. Sikutarajia kuona Chama cha mapinduzi hakijachukua hatua za kinidhamu kwa mkuu wa wilaya ya Arusha na wenzake ambae alicharaza viboko binadamu wenzake kama mbwa hadharani. Mbona kipo kimya? Ndio kusema dhana ya utawala bora haina umuhimu kwao?

Nilitegemea kusikia Katibu mkuu wa Ccm na mwenyekiti wake akikemea vitendo vya vyombo vya ulinzi na usalama kuwa wanaua raia wasio na hatia kwa kisingizio kuwa na kutotii bila shuruti.

Je Ccm hii ya leo inasimamia vizuri utelezaji wa ilani yake? Jibu ni kidogo sana, maana pamoja na kuwa wananchi wengi wanaaminishwa kuwa hali ni nzuri kwenye sekta ya afya,elimu na miundo mbinu,ukweli ni kuwa hali haiko hivyo.

Hospital na vituo vya afya havina madawa na watumishi. Wananchi wengi kipato chao ni duni na hawana uwezo wa kugharamia huduma za afya. Shule nazo zipo hoi maana hazina walimu na madarasa ni machache.

Kama chama makini nilitarajia kiwe kimewapa adhabu mawaziri, wakuu wa mikoa na wilaya ambao hawasimamii ilani ya chama kwa kuwasimamisha uanachama, lakini haya hayafanyiki.

Kwa ujumla CCM ipo hai kwenye macho ya watu lakini kiuhalisia imekufa maana haina sauti. Na ipo mikononi mwa wajanja wachache.
 
Mkuu sijui CCM wamekufanya nini asee, mbona umegeuka sana?

1. Ni ishu za uteuzi?
2. Upo kwa kazi maalumu, Umetumwa kuingiza watu chaka?
3. Pamoja na kuiponda CCM na serekali yake siku hizi, je bado unamkubali sana kimahaba JPM?
 
Utakuwa umeandikiwa.Huwezi kuwa na fikra chanya km hizi zinazosadifu ukweli halisi kwamba CCM Ni chama mfu.

Kitu kimoja hujaangaziay kwamba , kipo madarakani kwa nguvu ya majeshi, polisi, Jwtz, magereza, mgambo na watu wote waovu ndani ya nchi hii.

Bila majeshi CCM haipo.
 
Mkuu sijui CCM wamekufanya nini asee, mbona umegeuka sana?

1. Ni ishu za uteuzi?
2. Upo kwa kazi maalumu, Umetumwa kuingiza watu chaka?
3. Pamoja na kuiponda CCM na serekali yake siku hizi, je bado unamkubali sana kimahaba JPM?
Fanya tathimini ya nilichoandika utapata majibu.
 
Najaribu kufikiria chama hiki cha CCM kilikuwa kikisema kina wanachama millions 17 na wafuasi wapya millions 5 lakini kilikuwa kinasumbuliwa na CHADEMA , haitoshi wakatumia nguvu kuwatoa ndani bunge wanaki wenyewe. Ok sawa!! Waliweza lakini ndani ya bunge sasa unaweza kufikiri ni big brother la kule afrika kusini.

Logic zao ndogo ndani bunge hakuna cha ajabu, Magufuli lazima awe juu ya hawa Mandondocha. Yani sasa mpaka Mataga wanawakataa wabunge wao.

Kwasasa ccm wanatumia nguvu tu kuongoza!! Yani wanachama millions 17 wabunge hakuna.
 
Upinzani lege lege ndio utaiimarisha CCM kwa miaka mingine 40!
Ripota, hujawahi kuandika kitu humu ukapata hata like moja. Sijawahi kuona.
Unajisikiaje, watu wanakuonaje. Si jambo dogo hili.
Tafsir Ni mtu usiye na hoja hivyo watu wanakupuuza.

Kazi unayoiweza Ni kuripoti matukio toka vyombo vya habari tv na redio.Kwa hili nakupa kongole ripota wetu.
 
Upinzani lege lege ndio utaiimarisha CCM kwa miaka mingine 40!
Hakuna CCM. Kuna Dola.

Vyama vyote vya upinzani kazi yao kubwa ilikuwa ni kupambana na Dola maana CCM haipo.

Kikwete alipenda tupate Katiba mpya huku taifa likiwa na amani, upendo na masikilizano.

Ila kwa kuwa kuna Genge dogo la la Shetani linalopenda kuona damu. Ipo siku nchi hii katiba mpya yenye usawa itaandikwa baada ya mapigano na kumwaga damu kama ilivyotokea Zanzibar na Kenya.

Bado kitambo kidogo tu.
 
Ripota,hujawahi kuandika kitu humu ukapata hata like moja. Sijawahi kuona.
Unajisikiaje,watu wanakuonaje. Si jambo dogo hili.
Tafsir Ni mtu usiye na hoja hivyo watu wanakupuuza.

Kazi unayoiweza Ni kuripoti matukio toka vyombo vya habari tv na redio.Kwa hili nakupa kongole ripota wetu.
Ukitaka like nenda ITV Malumbano ya Hoja.

Jf like inakusaidia nini?

Nani anakujua?

Anyway ahsante kwa kongole ya ripota wa jf!
 
CCM ya leo![emoji1][emoji1][emoji1]
5390066.jpg
 
Ripota,hujawahi kuandika kitu humu ukapata hata like moja. Sijawahi kuona.
Unajisikiaje,watu wanakuonaje. Si jambo dogo hili.
Tafsir Ni mtu usiye na hoja hivyo watu wanakupuuza.

Kazi unayoiweza Ni kuripoti matukio toka vyombo vya habari tv na redio.Kwa hili nakupa kongole ripota wetu.
Achana naye mgonjwa wa bipolar disorder huyo Kama bodi wake mzee wa frustrations , mada zake huwa ni fupifupi pumba tupu huyo ni empty head tabulalasa kwelikweli .
 
Ripota,hujawahi kuandika kitu humu ukapata hata like moja. Sijawahi kuona.
Unajisikiaje,watu wanakuonaje. Si jambo dogo hili.
Tafsir Ni mtu usiye na hoja hivyo watu wanakupuuza.

Kazi unayoiweza Ni kuripoti matukio toka vyombo vya habari tv na redio.Kwa hili nakupa kongole ripota wetu.
Na habari za Mzee Mgaya sijui ni Nani yarabi huyu Mzee?.
 
Back
Top Bottom