Miaka 50 ijayo wajukuu wetu watatulaani kwanini tulimnyonga Lissu, kama DRC wanavyolaani kuhusu kumuua Lumumba.

econonist

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
25,522
Reaction score
40,795
Habari Wana JF

Leo nilikuwa natafakari ni jinsi gani watu wa DRC walivyomuua Waziri Mkuu wao wa Zamani Patrice Lumumba mwaka 1961. Ukiangalia zile picha za video wakati Lumumba anakamatwa utashangaa sana. Kwanza, Lumumba aliwaomba jeshi wasimpige wamkamate tu, ila akatokea mwanajeshi Mmoja nyuma yake na kumtwanga Kofi. Pili, hata walipompandisha kwenye karandinga ya jeshi, bado walimfunga kamba kama mbuzi au ng'ombe. Walimkamata kwa kumdhalilisha. Tatu, wakongo wengi walishangilia kuanzia wananchi wa DRC hadi askari wenyewe. Ilikuwa ni sherehe kubwa kwamba Lumumba amekamatwa.

Ila Leo baada ya miaka 65, wakongo wa sasa ndio wanalaaani mababu zao kwanini walimuua Lumumba kipindi kile. Na wengine wanadhani kumuua Lumumba ilikuwa mwanzo wa matatizo ya DRC wanayokumbana nayo mpaka Leo. Lumumba anaheshimika sana Leo DRC kuliko kipindi kile wanamkamata miaka 65. Watu wazima wengi wa kizazi kile waliomkamata Lumumba na kushangilia, wametangulia mbele za haki na wengine ni wazee sana kama wapo hai Leo. Wakati wanafanya yale maamuzi hawakuwa na ufahamu wanafanya nini, na walikuwa wanafanya maamuzi kwa chuki na kumkomoa Lumumba.

Tanzania ya Leo inataka kufanya kosa kama la wakongomani mwaka 1961. Tunataka kumuua Lissu kwa kumnyonga kwa makosa ambayo hata hayaeleweki. Kuna watanzania wengi wapo kwenye mfungo wa Mwaipopo wakitaka Lissu anyongwe. Serikali nayo (kupitia Kingai) itafurahia sana Lissu akinyongwa. Wapo wanachama wa CCM ambao wao hawajali kama Lissu amefanya uhaini au la, wao wanataka anyongwe tu. Swali linakuja, kwanini tunamchukia Lissu kiasi hicho? Na je tukimuua Nini kitatokea mbele?

Tukishamnyonga Lissu, maana hatuoni umuhimu wake Leo, miaka 65 ijayo, kile kizazi kitatuona kama tulikuwa watu wa ajabu sana. Yani sisi Leo tunaweza kujiona tupo sahihi na ni wajanja ila miaka 65 ijayo tutaonekana tulikuwa kizazi cha vichaa na wasiojitambua. Yani tulimnyonga Lissu, ila Mafisadi tukawakumbatia na kuwaabudu, tulimnyonga Lissu ila waliowafukuza wa Masai kwenye eneo lao la asili tukawakumbatia. Tulimnyonga Lissu ila waliouza bandari tukawakumbatia, tulimnyonga Lissu ila walioharibu mchakato wa Katiba na kutuingiza kwenye hasara ya Trilioni Moja ndio tunawaona wa maana. Tulimnyonga Lissu ila walioteka na kuwaua watanzania wenzetu mafichoni tuliwashangilia na kuwaona mashujaa. Tulimnyonga Lissu ila tukawaogopa na walioua watanzania 500 (ingawa idadi ni kubwa).

Chonde chonde, watanzania tusirudie makosa ya wa DRC miaka ya 65, kwa kufanya maamuzi ya chuki na kumkomoa mtu Mmoja , kwa kudhania akiondoka yeye basi mambo yatakuwa sawa. La hasha, mambo yatakuwa mabaya Zaidi. Maana DRC baada ya kumuua Lumumba kupitia Moise Tshombe wa Katanga, walidhani wamemaliza tatizo. Ila huyo Tshombe akaja akauawa, Kasavubu akapinduliwa, Mobutu akaongoza nchi kwa mtutu wa bunduki na ndipo vikundi vy waasi vikaibuka mpaka Leo Kongo haijatulia.

Tuna muda wa kujisahihisha na tujisahihishe yasije kutukuta makubwa.
 
Nafikiri Lisu amefanya poa sana kuexpose mapungufu ya kesi.

Kama kilichotokea mahakamani ni ambacho tumesoma online Lisu hakutakiwa kua mahabusu from week one aliyokamatwa.

Kesi ikarefushwa. Let's see
 
Mie kaburi langu nitaacha wosia waeke viboko vingi sana kwa juu..
 
Wakongo wamepata Laana ya Lumumba.
Miaka 66 ya uhuru nchi Imetapakaa.
1. Waasi.
2. Wasaliti
3. Vita.
4. Magonjwa
5. Damu nk

Laana ya Lumumba itawatesa vizazi vyote.
 
Habari Wana JF

Leo nilikuwa natafakari ni jinsi gani watu wa DRC walivyomuua Waziri Mkuu wao wa Zamani Patrice Lumumba mwaka 1961. Ukiangalia zile picha za video wakati Lumumba anakamatwa utashangaa sana. Kwanza, Lumumba aliwaomba jeshi wasimpige wamkamate tu, ila akatokea mwanajeshi Mmoja nyuma yake na kumtwanga Kofi. Pili, hata walipompandisha kwenye karandinga ya jeshi, bado walimfunga kamba kama mbuzi au ng'ombe. Walimkamata kwa kumdhalilisha. Tatu, wakongo wengi walishangilia kuanzia wananchi wa DRC hadi askari wenyewe. Ilikuwa ni sherehe kubwa kwamba Lumumba amekamatwa.

Ila Leo baada ya miaka 65, wakongo wa sasa ndio wanalaaani mababu zao kwanini walimuua Lumumba kipindi kile. Na wengine wanadhani kumuua Lumumba ilikuwa mwanzo wa matatizo ya DRC wanayokumbana nayo mpaka Leo. Lumumba anaheshimika sana Leo DRC kuliko kipindi kile wanamkamata miaka 65. Watu wazima wengi wa kizazi kile waliomkamata Lumumba na kushangilia, wametangulia mbele za haki na wengine ni wazee sana kama wapo hai Leo. Wakati wanafanya yale maamuzi hawakuwa na ufahamu wanafanya nini, na walikuwa wanafanya maamuzi kwa chuki na kumkomoa Lumumba.

Tanzania ya Leo inataka kufanya kosa kama la wakongomani mwaka 1961. Tunataka kumuua Lissu kwa kumnyonga kwa makosa ambayo hata hayaeleweki. Kuna watanzania wengi wapo kwenye mfungo wa Mwaipopo wakitaka Lissu anyongwe. Serikali nayo (kupitia Kingai) itafurahia sana Lissu akinyongwa. Wapo wanachama wa CCM ambao wao hawajali kama Lissu amefanya uhaini au la, wao wanataka anyongwe tu. Swali linakuja, kwanini tunamchukia Lissu kiasi hicho? Na je tukimuua Nini kitatokea mbele?

Tukishamnyonga Lissu, maana hatuoni umuhimu wake Leo, miaka 65 ijayo, kile kizazi kitatuona kama tulikuwa watu wa ajabu sana. Yani sisi Leo tunaweza kujiona tupo sahihi na ni wajanja ila miaka 65 ijayo tutaonekana tulikuwa kizazi cha vichaa na wasiojitambua. Yani tulimnyonga Lissu, ila Mafisadi tukawakumbatia na kuwaabudu, tulimnyonga Lissu ila waliowafukuza wa Masai kwenye eneo lao la asili tukawakumbatia. Tulimnyonga Lissu ila waliouza bandari tukawakumbatia, tulimnyonga Lissu ila walioharibu mchakato wa Katiba na kutuingiza kwenye hasara ya Trilioni Moja ndio tunawaona wa maana. Tulimnyonga Lissu ila walioteka na kuwaua watanzania wenzetu mafichoni tuliwashangilia na kuwaona mashujaa. Tulimnyonga Lissu ila tukawaogopa na walioua watanzania 500 (ingawa idadi ni kubwa).

Chonde chonde, watanzania tusirudie makosa ya wa DRC miaka ya 65, kwa kufanya maamuzi ya chuki na kumkomoa mtu Mmoja , kwa kudhania akiondoka yeye basi mambo yatakuwa sawa. La hasha, mambo yatakuwa mabaya Zaidi. Maana DRC baada ya kumuua Lumumba kupitia Moise Tshombe wa Katanga, walidhani wamemaliza tatizo. Ila huyo Tshombe akaja akauawa, Kasavubu akapinduliwa, Mobutu akaongoza nchi kwa mtutu wa bunduki na ndipo vikundi vy waasi vikaibuka mpaka Leo Kongo haijatulia.

Tuna muda wa kujisahihisha na tujisahihishe yasije kutukuta makubwa.
In fact,
waTanzania wote wanafurahia sana umoja, amani na usalama wa taifa lao kulindwa kwa nguvu na gharama zote chini ya serikali sikivu ya CCM.

Na wanafurahia sana,
pale maadui wa umoja, amani na usalama wao wanapoadabishwa kwa mujibu wa sheria za nchi.

Kila moja ni shahidi,
jinsi ambavyo waTanzania wote hufurahia pale sheria za nchi na katiba yao vinapotekelezwa kwa maneno na vitendo, bila kumuonea mkiuka sheria hizo huruma, kumuonea haya wala aibu.🐒

Mungu Ibariki Tanzania
 
Habari Wana JF

Leo nilikuwa natafakari ni jinsi gani watu wa DRC walivyomuua Waziri Mkuu wao wa Zamani Patrice Lumumba mwaka 1961. Ukiangalia zile picha za video wakati Lumumba anakamatwa utashangaa sana. Kwanza, Lumumba aliwaomba jeshi wasimpige wamkamate tu, ila akatokea mwanajeshi Mmoja nyuma yake na kumtwanga Kofi. Pili, hata walipompandisha kwenye karandinga ya jeshi, bado walimfunga kamba kama mbuzi au ng'ombe. Walimkamata kwa kumdhalilisha. Tatu, wakongo wengi walishangilia kuanzia wananchi wa DRC hadi askari wenyewe. Ilikuwa ni sherehe kubwa kwamba Lumumba amekamatwa.

Ila Leo baada ya miaka 65, wakongo wa sasa ndio wanalaaani mababu zao kwanini walimuua Lumumba kipindi kile. Na wengine wanadhani kumuua Lumumba ilikuwa mwanzo wa matatizo ya DRC wanayokumbana nayo mpaka Leo. Lumumba anaheshimika sana Leo DRC kuliko kipindi kile wanamkamata miaka 65. Watu wazima wengi wa kizazi kile waliomkamata Lumumba na kushangilia, wametangulia mbele za haki na wengine ni wazee sana kama wapo hai Leo. Wakati wanafanya yale maamuzi hawakuwa na ufahamu wanafanya nini, na walikuwa wanafanya maamuzi kwa chuki na kumkomoa Lumumba.

Tanzania ya Leo inataka kufanya kosa kama la wakongomani mwaka 1961. Tunataka kumuua Lissu kwa kumnyonga kwa makosa ambayo hata hayaeleweki. Kuna watanzania wengi wapo kwenye mfungo wa Mwaipopo wakitaka Lissu anyongwe. Serikali nayo (kupitia Kingai) itafurahia sana Lissu akinyongwa. Wapo wanachama wa CCM ambao wao hawajali kama Lissu amefanya uhaini au la, wao wanataka anyongwe tu. Swali linakuja, kwanini tunamchukia Lissu kiasi hicho? Na je tukimuua Nini kitatokea mbele?

Tukishamnyonga Lissu, maana hatuoni umuhimu wake Leo, miaka 65 ijayo, kile kizazi kitatuona kama tulikuwa watu wa ajabu sana. Yani sisi Leo tunaweza kujiona tupo sahihi na ni wajanja ila miaka 65 ijayo tutaonekana tulikuwa kizazi cha vichaa na wasiojitambua. Yani tulimnyonga Lissu, ila Mafisadi tukawakumbatia na kuwaabudu, tulimnyonga Lissu ila waliowafukuza wa Masai kwenye eneo lao la asili tukawakumbatia. Tulimnyonga Lissu ila waliouza bandari tukawakumbatia, tulimnyonga Lissu ila walioharibu mchakato wa Katiba na kutuingiza kwenye hasara ya Trilioni Moja ndio tunawaona wa maana. Tulimnyonga Lissu ila walioteka na kuwaua watanzania wenzetu mafichoni tuliwashangilia na kuwaona mashujaa. Tulimnyonga Lissu ila tukawaogopa na walioua watanzania 500 (ingawa idadi ni kubwa).

Chonde chonde, watanzania tusirudie makosa ya wa DRC miaka ya 65, kwa kufanya maamuzi ya chuki na kumkomoa mtu Mmoja , kwa kudhania akiondoka yeye basi mambo yatakuwa sawa. La hasha, mambo yatakuwa mabaya Zaidi. Maana DRC baada ya kumuua Lumumba kupitia Moise Tshombe wa Katanga, walidhani wamemaliza tatizo. Ila huyo Tshombe akaja akauawa, Kasavubu akapinduliwa, Mobutu akaongoza nchi kwa mtutu wa bunduki na ndipo vikundi vy waasi vikaibuka mpaka Leo Kongo haijatulia.

Tuna muda wa kujisahihisha na tujisahihishe yasije kutukuta makubwa.
Jamhuri ndiyo ilimshitaki lakini bado mahakama haijatoa hukumu hadi tarehe 6 November je, Jamhuri au mahakama? Ukiangalia mwenendo wa kesi, TAL Hana makosa ya uhaini kwa kuwa alikuwa ni mwenyekiti wa chama na alitoa kauli ile mbele ya watia Nia ya kugombea nafasi ya uongozi katika uchaguzi mkuu na Chadema imeona kuwa bila katiba mpya hakuna uchaguzi.NRNE sasa tuone mahakama itaonesha wazi namna itakavyotoa hukumu kwa haki . Ikiwa itazingatia uhuru wa kutoa maoni na uhuru wa kufanya siasa basi TAL hatanyongwa na ataachiwa huru.
 
Back
Top Bottom