Pasco,
Dk. Harith Ghassany tukizungumza kwa simu yeye akiwa Maryland, Washington
mimi nikiwa Ngamiani Tanga nilimpa fikra zangu za siku za mwisho za
Kassim
Hanga kabla hajauliwa.
Ghafla akanambia anataka kunirekodi ili maneno yangu ayatumie katika kitabu.
Alifanya hivyo.
Pasco ikiwa umekisoma kitabu utayakumbuka haya meneno yangu hapo chini:
''Kuwa
Hanga ndiye aliyekuwa kinara wa Mapinduzi ya Zanzibar hili si jambo
lenye utata tena. Ikiwa hivyo ndivyo
Hanga hatoweza kuutua mzigo wa roho
zilizopotea katika mapinduzi hayo.
Ikiwa
Hanga atalaumiwa kwa vifo vya maelfu ya Wazanzibari nani alaumiwe
kwa umauti uliomfika
Hanga tena kwa kuuliwa kishenzi kwani hapana neno
zaidi ya hilo linaloweza kutosheleza kuelezea jinsi Hanga alivyouliwa.
Kichekesho kikubwa ni kuwa wale waliopoteza roho kwa hiyo kutangulia mbele
ya haki, yao yalikuwa yamekwisha. Lakini kwa wale wajane na mayatima
waliobakia nyuma wakihangaika, kifo cha Hanga na wenzake katika wale
waliofanikisha mapinduzi kuuliwa kwao kulikuwa muujuza wa aina yake,
uchawi usioelezeka nani fundi wake.
Ilikuwa vigumu kueleza. Ingeeleweka vyema endapo kisasi cha kuitoa roho
ya
Hanga kingetimizwa kutoka katika mikono ya maadui zake waliopinduliwa.
Haikuwa hivyo.
Wale wajane na mayatima walililipiziwa kisasi na watu waliokuwa maadui
wakubwa wa waume na baba zao waliopinduliwa. Vipi
Hanga kiongozi mkuu
wa mapinduzi aje kuwa adui wa mapinduzi yenyewe kiasi cha kuwa hukumu
ya kumtosheleza haikuwa kifo tu bali kifo cha kishenzi.
Fikra ya
Hanga ilikuwajealipokuwa peke yake ndani ya selo Ukonga Prison
usiku ukimpita bila ya hata lepe la usingizi akiwaza yanayomkabili. Nini kilikuwa
kikipitika katika ubongo wake wakati wauaji wake walipomtoa katika selo yake
na yeye akawakabili ilhali aikijua kuwa walikuwa wamekuja kuitoa roho yake.
Fikra yake ilikwenda wapi? Ilikwenda kwa
Sultan Jamshid bin Abdullah
aliyempindua na kwa masultani wengi waliopita ambao wameiaga dunia mikono
yao ikiwa haina damu au kwa
Abeid Amani Karume aliyeingia madarakani
kwa mapanga ya Wamakonde kutoka Tanganyika, wakata mkonge kutoka
Tanganyikawakifanya kazi mashamba ya Sakura na Kipumbwi? Fikra ya
Hanga ilielekea wapi? Kwa
Nyerere aliyemsaliti?
Hakika ni wazi hakutegemea mapinduzi aliyoyasisi yangemgeukia na kuwa
sababuya yeye kutolewa roho kwa kuuliwa kishenzi. Jambo la kusikitisha ni
kuwa hadi pale alipokamatwa na kuwekwa jela Ukonga na kufikishwa mbele ya
mkutano wa hadhara na kuadhiriwa na
Julius Nyerere tayari alikuwa
keshapoteza kila kitu achilia mbali dira ya mapinduzi aliyokusudia ingeongoza
Zanzibar.
Hanga hakuwa kamwe na uwezo wa kumfanya
Karume lolote kwani
Karume
tayari alikuwa chini ya mbawa za
Nyerere ngome ambayo
Hanga asingeweza
kuitikisa achalia mbali kuibomoa. Muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar
ilikuwa hirizi tosha ya kumkinga
Karume.
Katika mkasa wa kuuliwa kwa
Hanga ndipo msemaji mmoja akasema, Maiti
toka makaburini mwao walionyesha ujuzi wa kufanya miujiza na uchawi wao
kwani laiti kifo cha
Hanga kingesababishwa na wale waliopinduliwa kisasi
chake kingekuwa cha kutisha. Ilibidi
Hanga kwa miujiza ya maiti zile auliwe
na wale wale aliowaweka madarakani watu ambao hapakuwepo na sababu
ya wao kumuona adui.
Halikudondoka chozikwa kifo cha Hanga. Kila aliyepata mnongono wa kuuliwa
kwake alikuwa kimyakama vile ile taarifa ile ya kifo haimuhusu.''
Pasco,
Hii ni moja katika visa vingi vya kusikitisha katika historia ya mapinduzi ya
Zanzibar.
Maujai ya kishenzi, mateso na udhalilishaji ambao sina ujasiri wa kueleza hapa.
Sina ujasiri kwa kuwa hawa waliouliwa ndugu, jamaa na rafiki zao bado wa
hai.
Wasingependwa kukumbushwa machungu haya yaliyo wafika ndugu zao.
Nakuuliza
Bwana Pasco.
Kuna utukufu gani katika historia kama hii?
Na
Hanga hakuuliwa na Waarabu.
Ndiyo toka mwanzo nikakuonya kukuambia kuwa wewe huna makamo ya
kuzungumzia Mapinduzi ya Zanzibar.
Hii ndiyo sababu hadi leo hajapata mtu yoyote kutoka Zanzibar kuandika
chochote kuhusu kitabu
Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru.
Hata hao makomredi ambao wanahusishwa na mapinduzi hadi leo
hawajanyanyua kalamau.
Inawezekana kuwa Wazanzibari wengependa sana kusahau uovu
uliopita.
[TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD="class: tr-caption, align: left"]Kassim Hanga ni huyo aliyekaa chini ya jukwaa kavaa miwani. Aliyevaa sare ya polisi ni Hamza Aziz kushotoni
kwake ni Andrew Shija aliyevaa pama. Aliyekaa mbele ya Kassim Hanga ni Omari Londo. Nyerere ndiye huyo
katika ulingo akihutubia. Hapo ni Mnazi Moja. Baada ya mkutano huu Hanga alirejeshwa Zanzibar na huko
akauawa mwaka 1967 au 1968
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]