Miaka 50 Ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, Bado Kuna Maswali Bila Majibu -1


Umetokota, oops, umechemsha!
 
By Yombayomba


Usikimbie, kamwite huyo aje ajibu hapa mmechangia kiasi gani? hizi hadithi ohh koti likikubana so what, mbona chupi ikimbana hasemi?


Naona Yombayomba ushauri wangu umekuingia na umemsoma tena Jussa kwa "utuvu" na umeamua kutokuendelea nami.

Kama una lingine, tafadhal.

Ritz, kwa heshima na taadhima, mkaribishe gahwa kwa halwa ya Gidemi ile ya Loz huyu kijana, naona mate yamemkauka.
Yombayomba, Ahlan Wasahlan Wamarhaba. Tafadhal, Tafadhal, Tafadhal.
 

Ahlan Wasahlan Akh l'Karim gombesugu.

Amma kwa hakika umenipa maneno matamu na mema na nimefarijika sana. Hususan na mualiko wako wa kunikaribisha chadema, laiti ingalikuwa si majukumu niliyonayo ya hapa na pale ningelijikita zaidi kwenye siasa, ila kwa sasa, siasa kwangu ni ushabik wa kutetea pale kwenye haki. Iwe kwa chadema au CCM au CUF au NCCR au kwingineko.

Ingawa hapa nilipo mimi ni mwanachama hai wa CCM tokea ilipoanzishwa 5-2-1977, kuna mengi hayakidhi matakwa niyatakayo ndani ya CCM, lakini busara zinaniambia ni bora ning'ang'ane kuyabadili nikiwa ndani ya CCM kuliko nikiwa nje ya CCM. Kwani huko nje ya CCM nahisi kuna mengi zaidi ambayo hayakidhi matakwa yangu.

Msemo wa "Zimwi likujualo halikuli likakwisha" umeniathiri zaidi katika hili.

Ahsantum wa Baraka Llahu Fik wa Fi Jammia L'muslimin.
 
Usikimbie, kamwite huyo aje ajibu hapa mmechangia kiasi gani? hizi hadithi ohh koti likikubana so what, mbona chupi ikimbana hasemi?

Kweli jf kuna vituko zomba wakukukimbia wewe au unatania?mjomba wangu pasiko siku 4 hapumui hapa iwe wewe?
 
Last edited by a moderator:

Huyu hafai hata kukaribushwa hiyo haluwa first class ya Gidemy.
 
Babu zetu ndio waliwauzia Waarabu watumwa, kwa shanga na vioo. Au hilo hulijui?

Aisee logic yako embuiangalie vizuri. Pasco anasema waarabu waliwauza babuzetu utumwani. Alafu wewe unwawatetea waarabu kwa kusema ni babuzetu ndio waliwauza babuzetu kwa waarabu kwakupewa vioo na shanga. Kwaiyo waarabu hawana makosa ila makosa ni ya hao babuzetu waliotumiwa na waarabu.

Utakuwa unawaabudu waarabu wewe
 
Huyo yombayomba alidhani hata Chit-Chat ati anakupiga mkwala haujui mziki wako.

zomba, huyu tutampa zile tende za kula gamia watoe maziwa.

Nilimpa ovyo utakuja kukimbia wewe humu watu wamejipanga kuna mipini ya haja.
 
Last edited by a moderator:
Haya Pasco. Mie mpaka unipe mji.

Majanga.
Hakuna mji wowote!, ukiamua kutaja taja, ukiamua kutotaja kwa sababu hujapewa mji usitaje,
simjui huyo kwenye picha wala anahusu nini!, "One can never miss what you never know!"
Ila pia kitendo cha kuomba nikupe mji, ni ishara njema ya good faith, nimekupa mji wa kwetu kule Mashokololokubangashee!.
Pasco.
 
Duh!mnawaogopa kiasi hicho?Ndo maana wakitoa amri wafuasi hamfikirii mara 2,kama Pasco ni mwandishi sioni ajabu kukutana nao.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Zomba, kiukweli hii rasimu ya pili ya Warioba imetenda haki bin haki na haswa kwa Wazanzibari hana budi kufanya maandamano kumpongeza, maana mimi ni miongoni mwa mwa wale watetezi wa muungano kamili wa nchi moja, serikali moja, rais mmoja!. Nilitamani sana Zanzibar iwe mkoa tuu wenye wilaya mbili kama Tandahimba tuu!.

Hili la muungano Mtukufu, saa hizi posti yako hii ni number #526 ikifanikiwa kunionyesha hata posti moja tuu, niliyosema au kuutaja Muungano Mtukufu, ndipo nitakujibu hapa, vinginevyo fuatilia mtiririko wa mada zangu, inayuhusu muungano ni ya 5 na ya mwisho. Mwezi Aprili wakati wa maandalizi ya Muungano, pia nitaleta mada 5 za Maswali kuhusu Muungano yaliyokosa majibu, japo naona kama Jaji Warioba, mengi ameisha yapatia ufumbuzi!.
Mtiririko wangu ni huu.


  • Part I-Miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar: Maswali Bila Majibu Part I
  • Part II-Jee nini Chanzo Halisi cha Mapinduzi ya Zanzibar na Nani Haswa Waipanga/Waliotekeleza
  • Part III -Nani ni Shujaa Halisi wa Mapinduzi ya Zanzibar!.
  • Part IV -Kwanini Abedi Amani Karume, Aliyakimbia Mapinduzi ya Zanzibar na hakushiriki?
  • Part V- Baadhi Matunda ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ni Muungano Adhimu!-"Mapinduzi Daima!"
Nasubiri tumalize hili tusonge mbele!.

Pasco.
 
Kama bunge ni tukufu na ndilo lilipitisha muungano,tuache double standard,muungano ni mtukufu hadi hapo itapokajulikana vingine.Nakubali pia kwamba mapinduzi ni matukufu.
 
Umetokota, oops, umechemsha!
Mkuu Zomba, hili la kutokota, huwa natokota mara kibao!, sambamba na kuchemsha, huwa nachemsha mara chungu nzima, ila pia katika kutokota huko, kuna wakati, nawatokotisha!, na katika kuchemka, kuna wakati nawachemsha!.
Miongoni mwa lugha zangu za kuchemsha ambalo imembidi Maalim Mohamed Said akae pembeni, ni hapa nilipomjulisha, akichangia yeye, kuna wafuasi wake hujitokeza kama mainzi wanavyozingea bucha ya utumbo!, wewe mwenyewe si ulishuhudia jana yale mainzi yalivyonisonga utafikiri yanagombea utumbo!. Ulifikia wakati nikajikalia pembeni, kuyaacha yakipishana mpaka yalipopungua, ndipo nikarejea, na kwa uzoefu wangu wa pilika pilika za mainzi, huwa ni mchana tuu, usiku yanatulia!, si unaona mida kama hii, mnakasha ni burdani kabisa!.
Pasco.
 
Mkuu Zomba kwa hili la msimamo wako kuhusu chama chako, nakuheshimu kwa hilo, kama ninavyomheshimu Mkuu Mchambuzi. Bhati mbaya sana mimi sina chama, kuhusu CCM, nilisema humu na huwa ninasema kila siku kuwa CCM kimechokwa, kimeoza kwa rushwa na ufisadi, kinanuka, kimevunda!, tegemeo na tumaini lote la ukombozi wa pili wa kweli wa Mtanzania limeelekezwa Chadema, tatizo Chadema hawajipanga, hivyo mimi ni miongoni mwa wachache humu tunaohubiri siasa za ukweli, "real politics" natukifikiria kiukweli "real thinking" kuishi kwenye ukweli "real life" kuwa 2015, bado ni CCM tena na huu ni ukweli mchungu, ila ukiwa realist, lazima uukubali mkweli huu mchungu tofauti na wenzetu wengi humu wanao amini "utopian politics" wakifikiria kwa "wishful thinking" na kuishi kwenye "dream life" kuwa 2015, Chadema itachukua nchi!.

CCM kweli ni li zimwi, in fact ni shetani, ila kwa 2015, hili ndilo zimwi tulijualo, na kwa vile ni shetani, in between the two devils, choose the lesser!, zimwi, shetani CCM, litachaguliwa tena kwa huku bara! na huko Zanzibar, wale ndugu zangu vibaraka wa Waarabu, kama kawa, watapokwa tena tonge mdomoni, yule mwenye ndoto za kukanyaga ikulu, itakuwa ndio basi tena!, maana 2015-2020 atakuwa kesha!.
Pasco.
Pasco.
 
Mkuu Ritz, fani yangu ni media, hivyo Mashekh wako hawa nimekaa nao kuzungumza nao ana kwa ana bahati mbaya enzi hizo, nilikuwa bado siko haya mambo ya mtandaoni, ila picha ninazo nimepiga nao ila pia bahati mbaya sana sina kawaida ya kutundika mapicha, kwa sababu sijapiga zile za kuonyeshea, hizo sio zangu. Hata huyu Sheikh Mkuu wa sasa pia nimefanya nae mazungumzo ya Anna kwa anna kwa vile tayari nilikuwa jf, niliyaleta humu, nisome hapa!.
Waislamu Chagueni Mgombea wa Dini Yoyote! - Mufti - JamiiForums au nisome hapa Sheikh Mkuu, Mufti Atoa Uhuru kwa Waislamu ..... - JamiiForums

Hivyo hao Masheik nimezungumza nao mwenyewe!. Ila hili la lafudhi ya Kiarabu, pia niao uwezo wa kuwabaini wale wanaozungumza lafudhi hii naturally kutokana na kubobea sana kwenye dini, na wale wanaizungumza lafudhi hii, au kuandika humu jukwaani kwa kuilazimisha kutoka na kuutukuza tuu Uarabu, na haswa wale Wamatumbi wenzetu wenye lafudhi ya kimatumbi kabisa ila, ili wajinasihibishe na Uarabu, basi ndio wanajikomba komba kuizungumza kwa kuandika lafudhi Kiarabu kwa kulazimisha kwa saana kupita hata hao Waarabu wenyewe!. Baadhi ya hizi lafudhi zinazoshuka humu,, mabata ushungu wallahi, ni burudani tupu!.
Pasco.
 

Kijana, mimi si katika Waabudu watu. Mimi ninaemuabudu ni mmoja tu, Allah. Tatizo linakuja pale kuna wanaoabudu mtu, tena si mtu wa ukweli, ni picha ya mtu, tena picha ya mzungu. Hao ndio wenye kusikitisha.

Mbona kuna babu zetu wengi nao walinunua Watumwa na kuwatumikisha? pitia hii nyuzi kuna mpaka picha zimewekwa humu. Usisikie kijana na usifikiri utumwa umekwisha, upo mpaka leo tena utashangaa hapa kwetu umeshamiri.
 

Umemaliza? hunipeleki huko. Swali langu hujajibu. Jee, mara yako ya kwanza kwenda Zanzibar ilikuwa lini na kwa sababu zipi?
 

Khawarizm,
Umetoa ya kumalizia mwaka. Yaani umetoa argument yako badala ya kui- backup na data au reference unampa pasco kibarua afanyie utafiti point za kui-backup argument yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…