zomba
JF-Expert Member
- Nov 27, 2007
- 17,240
- 3,930
Mkuu Maalim Mohamed Said, kwanza asante kutuwekea picha kuupendezesha huu mnakasha wa mengineyo, kiukweli upendezea na hilo vazi, sikujua kumbe na wewe pia?, huyo wa pili pia kapendezea na hiyo kanzu yake kama ya kule Arabuni, Omani!.
Karibu!.
- Kwanza simjui huyu ni nani wala sihitaji kumjua, ila ukiona anapaswa kujulikana, utamtaja kama nilivyosema siwajui makomred na ukawataja!.
- Unawasiwasi gani kuhusu hoja zangu za Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,hadi kunitaka nikuhakikishie kitu ili huo wasiwasi ukitoke?.
- Sijui ni kwanini umeniwekea hii picha, ila lengo la picha yoyote huwa nalifahamu!.
- Sishughulishi bongo yangu hata chembe kumjua ni nani na umemuweka ili iweje unless wewe ndio umtaje mwenyewe!, na usipomtaja, mada yangu bado itapata na huwa sipandishi mada na picha zozote!, zikiwemo ni bora zaidi ila mada zangu zote zahusu bongo sio macho, hivyo nimjue, nisimjue mada itapanda, umtaje usimtaje mada itashuka!.
- Nimeisha shindwa, ila simuombi yoyote kunisaidia kukitengua kitendawili hiki, kwa sababu mada yangu, haitegemei kitendawili hiki!, kiwepo kisiwepo, mada itashuka!.
- Namalizia kukuhakikishia kuwa sikuhakikishii kitu chochote ili nipandishe mada humu, nikimaanisha kupandisha kwangu mada humu, hakukutegemei wewe Mkuu Maalim Mohamed Said, hivyo nikuhakikishie as if nakubembeleza uje uchangie, nikianzisha uko free uje, kama ili uje ndio umenitaka nikuhakikishie kitu, sikuhakikishii chochote!, nikianzisha unaweza kuja, ukiona vipi unaweza usije!.
- Hata hivyo ukweli unabaki kuwa mimi Pasco wa jf, nakukubali sana wewe Maalim Maalim Said kuwa una "powers from within", hivyo ukichangia mada zozote, una mvuto mkubwa na kuipaisha na kuifanya ionekana ya maana hata kama haina maana!, japo saa nyingine, mvuto huo, huwavuta wengi na kupitiliza hadi kuinekana kama ni bucha ya utumbo, licha ya wanunuzi kitoweo cha utumbo kuisongea bucha, pia huzongwa na mainzi kibao!.
- Nkianzisha muendelezo wa mada hizi, nitafurahi ukiwepo, ila sio kwa kukubembeleza ili uwepo as if nakutegemea wewe, ukiwepo ni bora zaidi ila hata usipokuwepo mada itapanda tuu kwa sababu wewe sio tegemeo la kupanda kwa mada humu, usipokuja nitaikosa michango muhimu, ila pia yale mazonge ya ile mi inzi yatapungua!.
Pasco.
Umetokota, oops, umechemsha!
