Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Kwa heshma ya Karume na Mama Fatma, please lets spare them, please usiwageuze ni subject of discussion ya uzi huu!, mada uko thread ya kwanza, unamajibu jibu, huna kaa kimya!.
Naona nikatembelee threads nyingine, hapa hakuna kitu!.
And next time nakuomba mkuu Zomba, ukikuta thread ina maswali, kama unamajibu, changia!, kama huna, itoshe kupitia tuu na kujisomea!. Sio lazima kuchangia kila thread!. Issue nyingine ni ngumu zinahitaji sio tuu kubwabwaja majibu bali research ndipo jibu lipatikane, mpaka sasa tunakwenda page ya tano bado sijaona jibu lolote la maana!.
Pasco.
Pasco,
Kumbe unavamia mambo wala huijui historia ya Zanzibar.
Umetumwa?
Mkapa akiwa juu ya jukwaa Zanzibar alitoa hotuba kisha akawakejeli Waarabu
wa Oman.
Wengi katika wale waliokuwa katika jukwaa kuu waliinamisha vichwa chini na
mmoja wapo ni Amani Karume na mkewe Bi. Shadya pamoja na waheshimiwa
wengine.
Jioni kwenye chakula cha usiku Mkapa akaelezwa kuwa wale uliokuwa unawakashifu
ni wazee wa wengi wa watu wa Zanzibar na mmojawapo ni babu yake First Lady.
Pasco fanya hii homework.
Tafuta habari za Salim Jinja...
Hii itakusaidia kuelimika.
Na huu nimekupa mfano mmoja tu.
Iko mingi.
Usitukimbize ati tusimtaje Abeid Amani Karume na Mama Fatma.
Wewe ni mbaguzi na ndiyo maana umepelekwa huko ili ujue kuwa hujui kitu.
Wewe unaimbishwa na unaitika unachoimbishwa.
Kama alivyoimbishwa Mkapa na akaimba na katika ile nyimbo yake akajikuta
anawatukana Wazanzibari wengi na wengine mawaziri katika serikali yake.
Jibu la Mkapa baada ya mkasa ule alisema,''Sitokuja kuielewa Zanzibar.''
Lakini Zanzibar si ngumu kuielewa ikiwa kichwa chako kimetulia.
Pasco wa kukaa kimya ni wewe usiejua kitu.
Tupe nafasi sisi tukupe darsa kuhusu historia ya Zanzibar.
Wewe huna moja unalojua.
Ukijifunga kwenye mapinduzi na ukadhani kuwa hiyo ndiyo historia ya Zanzibar...
Huyo Muarabu aliyekuwa anamtafuta Mkapa na ndiyo huyo Muarabu unaemsaka
wewe.
Huyo Muarabu hayupo Zanzibar na hatakuwapo kamwe.
Nakuachia na hili la Salim Jinja.
Ukimaliza hilo nitakupa darsa mimi mweyewe kuhusu makomredi na In Sha
Allah tutaanza na marehemu Badawiy Qullatein.
