Miaka 50 Ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, Bado Kuna Maswali Bila Majibu -1


Kwa hiyo uache uongo wa kutamba kuwa eti "mimi ndio nilokiweka humu JF", wakati umekibandika leo hii na wenzako wamekiweka humu toka 2010.

Hiyo link nimeifunguwa na ulichokiandika ni hiki hapa:


Hahahahah hahaha, sasa unatamba umekisoma kitabu chake halafu hata hujui kaa mwandishi ndio huyo huyo? huo kama si upunguani ni nini.

Halafu unasema Okelo ana kitabu? hivi Okelo alikuwa anajuwa kuandika?

Hahahahahaaaaaaaaaaaaaaaaaahaha, una uwezo wa kukibomoa kitabu cha Dr. Harith Ghassany? kwa kipi zaidi ulichonacho cha historia ya Zanzibar? Ikiwa hata Makomred Huwajui.

Jee, unamjuwa Komred Toni?
 
Mkuu Pasco

Kuna viporo vingi sana vinakusubiri majibu kutoka kwako hili tuendelee na Mnakasha.
I will leave no stone unturned!. Viporo vyote vitajibiwa!, naona watu povu linaanza kuwatoka, tena wengine wanaanza kuyapandisha!, saa hizi nalala, kesho sina kazi, nitazipangua hoja moja baada ya nyingine!, hakibaki kitu hapa!.
Pasco
 

Nangoja Pasco ajibu swali ulilomuuliza.
 
Last edited by a moderator:
I will leave no stone unturned!. Viporo vyote vitajibiwa!, naona watu povu linaanza kuwatoka, tena wengine wanaanza kuyapandisha!, saa hizi nalala, kesho sina kazi, nitazipangua hoja moja baada ya nyingine!, hakibaki kitu hapa!.
Pasco

Unao uwezo huo?

Nangoja uje kujibu viporo vyangu huko juu. Halafu ujibu na hili:

Mara yako ya kwanza kwenda Zanzibar ilikuwa lini na kwa sababu zipi?
 

Wacha ukanjanja wako! Jee baada ya Mapinduzi ilibidi Zanzibar ijiunge tena UNO? Uhuru ulikuwa uhuru na Mapinduzi ni mapinduzi hakuna kitakachofuta chengine.
Muungano wa Tanzania ulikuwa wa Jamhuri mbili zenye viti umoja wa Mataifa na kile cha Zanzibar kilisimikwa siku hiyo unayoiponda.
 
Last edited by a moderator:

Nimesema hizi mada kuhusu Mapinguzi ya Zanzibar, ziko 5 -series, hii ni ya kwanza. Sijamuita yoyote mrongo, nimesema wameandika urongo!. Kama jina la anayeandika urongo ndio mrongo.. them wewe wasema.

Nilimjibu vizuri Maalim Mohamed Said, nawaomba msiupindue uzi huu ili series ya pili niwaletee urongo wa Dr. Ghassany. Urongo wa Maalim tumeishauchambua sana humu hatuna haja kuurudia, kwa faida yako pitia haya majibu yangu kwa makini!.
[/COLOR]
 
Unao uwezo huo?

Nangoja uje kujibu viporo vyangu huko juu. Halafu ujibu na hili:

Mara yako ya kwanza kwenda Zanzibar ilikuwa lini na kwa sababu zipi?
Zanzibar nimekuwa nakuja tangu mtoto nikisoma primary tukiwa na marafiki wa kizenji shuleni kwetu tukisoma nao bara, wakati wa likizo tukija kwao Zenzi wana hoteli kubwa enzi hizo!.

Nipongia uandishi tukaja ziara rasmi Zenzi tukapokelewa kwa kelele za kuitwa machogo!, tango hapo nimefanya zaidi ya sarri 100 Zanzibar!, nimeishalala Mwembe Madema!, nimeishaondolewa Zenj under escort na kupigwa marufuku nisikanyage tena!. Baadaye ban ikaondolewa!. Enzi za ujana pia nilishiriki sana na ndugu zetu sisi si ni dugu moja!.
Wiki ijayo nakuja kukaa siku 10 Zanzibar kushherekea Mapinduzi Matukufu na mimi ni wale Chapa Ng'ombe wa Kanda ya Ziwa, ugonjwa wetu unajulikana!. Wengi wa wabara sasa wakija Zenji ni kuja kuponda maraha, huu uzi unakoelekea siko, nikona vipi, nitaumalizia baada ya kutoka huko, sije endelea sana nikajikuta vile vichupa vya tindikali ndivyo vinanisubiri!. Hapo Zenj mpaka nina nyumba ya kufikia, anytime, nikiamua kulala hoteli ni kwa raha zangu tuu!. Zanzibar kwangu, Waarabu wangu, Wahadimu wangu, Watumbatu pia wangu!, na nyinyi bara yenu!.
Tunajenga nyumba moja Tanzania, kwa nini mnataka tugombee fito?. Kiukweli tukiona vipi, tunaamua tuu Nchi Moja, Serikali Moja!.
Pasco.
 
Huu ndio msimamo wa ASP 23 April 1960.
Sir
..........................
8.(a) It is the ASP strong opinion that as far as possible the new constitution should be based both in composition and function, on the British Constititution which has worked so successfully in Britain. No attempt should be made to adapt it local conditions.....................To adapt it before it is first applied will be tantamount to operating a case before ascertaining the disease. With this in view we beg to submit the following:-
i)position of present Dynasty. The Sultan of Zanzibar is a Constitutional monach.He is the head of our state,above and outside politics- the unifying factor in the constitution and ASP accepts the principle that the present dynasty should be safegurded and guaranteed...........

We honour to be,
Sir,
Your obedient servants
End of qoute
Huu ndio msimamo rasmi wa ASP kuhusu mfumo wa utawala.
With this
 
Pasco kuwa muungwana. Hata sie lugha hizo twaziweza. Ushemeji hauelemei upande mmoja. Kuwa na adabu.
La ushemeji, si nimesema ninge!, au hasira na kumbadili dini mtu?!. Mbona wabara wengi wamesilimishwa kwa ajili hiyo!. Bara Zanzibar dugu moja!. Hata mitaa yako hapo Gerezani, tumepita sana tuu, wakati huo nikiwa RTD, walikuwa wanakuja wenyewe!. Ujana nao una ushetani wake, basi tuu saa hizi ungekuta labda niliishasilimishwa zamani nikiitwa Mkwe!. Basi tuu!.
Pasco.
 
Mkuu Maalim Mohamed Said, asante nakushukuru, nimemfahamu komred Victor Mkello, sasa tunaweza kurejea kwenye mada?!.
Pasco
 
Mkuu Maalim Mohamed Said, kiukweli nilitumwa!, nimeimbishwa na sasa naenda kumuuliza alienituma kama tuendelee na huu mnakasha au tuufunge maana hatukutegemea mtu kama wewe ungeingia humu na ukiingia pahali, shughuli yake pevu!.

Ni kweli sina moja ninalojua ndio maana nimeuliza?!.

Pia ni kweli siwajui kabisa komred Salim Jinja wala komred Badawiy Qullatein, naomba unieleweshe wanahusika na nini katika mada yangu kuu ya uzi huu!. Ndio hao waliomsindikiza Shamte kule UNO au ndio waliopeleka yale malipo ya miaka kadhaa mbele au ndio waliofanya nini haswa maana mada yangu kuu hapa ni jinsi kiti cha Zanzibar kilivyopotea kule UNO hadi sasa Zanzibar kubaki jina tuu ikiitwa nchi ili hali kiuhalisia sio nchi bali ni sehemu tuu ya JMT yenye mamlaka yake kamili kushughulikia mambo yake ndani. Ingekuwa ni Nyumba, ni yale madogo madogo ya jikoni, chumbani na maliwato,yale makubwa ya kibarazani na sebuleni ni wenyewe!.
Pasco.
 
Pasco,
Hapo chini ni mimi nafanya mahojiano ya TV na Salim Rashid
kuhusu mapinduzi ya Zanzibar.

Alosema hayana tofauti na haya ninayokuambia wewe.
Naamini unamjua Salim Rashid na nafasi alizoshika Zanzibar.

Mkuu Maalim Mohamed Said, kiukweli nimekuona kwenye hayo mahojiano ya TV na Salim Rashid, tena kwa vile na mimi huwa nafanya vipindi vya TV, nakiri hao wenzetu wataalumu kweli!, huwezi hata kuona vipaza sauti au japo hata kivuli cha kamera!.

Na jinsi mnavyoonekana kiukweli mmependeza, kanzu zinang'aa kweli kweli!, hivi hizi kanzu ni za hapa kweli hizi sio zile za kutoka Uarabuni?!. Ila hilo zulia hata kwa macho tuu naliona ni Persian!. Naomba unikumbushe kidogo hivi Salim Rashid ni nani vile?!, katika mukhtadha wa mnakasha huu kuhusu kiti cha Zanzibar, Salim Rashid aliplay role gani vile?!.
Endelea kutuelimisha!
Pasco
 

kubwa zima umeishiwa hoja unaanza kuharisha na kubana pua eti "kanzu za wapi? sijui zulia la persian" sikiliza we kama vp waambie mods waufunge tuu hu uzi!!! eeenhhhh si maji shingoni,
 
Pole Pasco, kumbuka hapa unapambana na watoto hadi vitukuu wa waliodai kunyang'anywa tonge mdomoni mwaka 1964...loo! hiyo ghadhabu yao utaiweza? Kuna watu wameamua ku"rewrite history" based on sources zilizotawaliwa na visasi, they will stop at nothing; watakubeza, watakutukana na watakulaani kwani chuki zao haziwezi kuwapa mwanya wa kufanya vinginevyo. Porojo za Ghassany na ngano za Mohamed? No, not worth my time and effort. Nakumbuka Sultani kijana Jamshid bin Abdullah alivyoduwaa baharini na boti lake asijue akimbilie wapi baada ya Kenyatta kumwekea ngumu kukanyaga Malindi, Kenya hadi Nyerere alipompa hifadhi ya muda Tanganyika...am out.
 
Last edited by a moderator:
Umenikumbusha, muasisi na baba wa taifa huru la Zanzibar ni Mganda Okello ingawa wazenji wamemsahau tu!
 
Nani alie muua Karume? Kwanini Nyerere alimtishia kuwa asipokubali Muungano atawaacha vijana wamshughulikie?...
 

Pasco,
Sasa umehama kwenye mjadala wa mapinduzi ya Zanzibar umeamua kututukana?

Jua kitu kimoja.
Unapotukana kama hivyo unamtukana mama yako.

Huenda hii ikakushinda kuelewa.
Ikiwa utashindwa kufahamu sema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…