zomba
JF-Expert Member
- Nov 27, 2007
- 17,240
- 3,930
Asante kwa links hizo, kumhusu Dr. Ghassany, naomba fungua hii link hapa, soma tarehe ya hii thread, angalia nilisema nini kumhusu Dr. Ghassany, by the time nachangia hapa nilikuwa nimeishasoma kitabu siku nyingi na nilipewa na dada yenu, Mtoto wa Kiarabu hapo Zanzibar!, tena mnabahati sisi haturuhusiwi kuoa zaidi ya mara moja!, ningembadili dini na leo hii ningekuwa shemeji yenu!. Muungano wa Tanganyika na Zanzibar; Una Faida gani na kwa ...
Leo nimekiweka ili wengi zaidi wakisome, ili nitakapoanza kukibomoa, tuweze kwenda sambamba.
Pasco
Kwa hiyo uache uongo wa kutamba kuwa eti "mimi ndio nilokiweka humu JF", wakati umekibandika leo hii na wenzako wamekiweka humu toka 2010.
Hiyo link nimeifunguwa na ulichokiandika ni hiki hapa:
Hata mimi hii ya 3 ndio naisikia rasmi. Kuna mwandishi sijui kama ndio huyo huyo Ghasany eti alifanya mahojiano na vibarua wakata mikonge wa Tanga walikodiwa wakapandishwa mitumbwi Bagamoyo wakaenda kuipindua serikali halali ya Zanzibar. Sasa leo ndio naisikia hii ya majeshi ya uvamizi ya Tanganyika Rifles!.
Mimi nimefuta kidogo ujinga kwenye somo la historia, karibu historia kubwa ya Mapinduzi ya Zanzibar iliandikwa na waandishi wakizungu.
Nyingine nilisoma kitabu cha Okelo. Hao wasomi wa Umma wanaojidai walishiri wameandika nini?.
Nani aliyeshiriki mapinduzi hayo ameandika kilichotokea haswa?. Kila ninachosoma kuhusu Mapinduzi ya Zanzibar najikuta naachwa na maswali mengi kuliko majibu.
Jambo moja la hakika ni kuwa Mapinduzi yale yalitokea, watu walichinjwa na majambia na waliowawa kinyama.
Hivyo licha ya kuwepo kundi linaloyatukuza Mapinduzi yale, pia lipo kundi la wahanga wa mapinduzi hayo ambalo wamekuwa wakiumia na kugumia maumivu ya makovu ya Mapinduzi yale kwa miaka mingi, sasa ndio wanapata nafasi angalau ya kuanza kupumua na kutoa nje frustrations zao na machingu yao kwa kuusingizia Muungano.
Muungano huu ni dhima iliyofungwa na Mwl. Julius Kambarage Nyerere na Sheikh Abedi Amani Karume ambao wote waneshatangulia mbele ya haki. Wote wenye kuubeza Muungano kwa nia ya kuuvunja, laana ya waasisi wake itawashukia.
Lazima tukubali Muungano una matatizo. Turekebishe matatizo hayo na kusonga mbele kuwa nchi moja!.
Pia ianzishwe Tume ya ukweli upatanisho na maridhiano ili Wanzanzibari waambiane ukweli wa kilichotokea ile Januari 11,1964. Waponyeshe makovu ya Mapinduzi yale kwa kuombana misamaha, washikane mikono wapeane pole na kupatana kufungua ukurasa mpya wa Zanzibar mpya.
Kwa fikra zangu naamini waandishi kama kina Ghasany ni vizalia vya wahanga wa Mapinduzi yale hiyo anawakilisha kizazi cha wahanga wenye machungu na Mapinduzi yale, ili kupunguza machungu hayo, hasira zao wabazielekeza kwenye Muungano kama scapegoat wa kujifariji!,
Hahahahah hahaha, sasa unatamba umekisoma kitabu chake halafu hata hujui kaa mwandishi ndio huyo huyo? huo kama si upunguani ni nini.
Halafu unasema Okelo ana kitabu? hivi Okelo alikuwa anajuwa kuandika?
Hahahahahaaaaaaaaaaaaaaaaaahaha, una uwezo wa kukibomoa kitabu cha Dr. Harith Ghassany? kwa kipi zaidi ulichonacho cha historia ya Zanzibar? Ikiwa hata Makomred Huwajui.
Jee, unamjuwa Komred Toni?