Miaka 55 ya BAKWATA: Tujikumbushe Historia Yake na Yaliyotokea October - December 1968

Miaka 55 ya BAKWATA: Tujikumbushe Historia Yake na Yaliyotokea October - December 1968

Mzee Kuna mgogoro upi unaohusisha taasisi ya Kiislamu ambao haukuchochewa na Wakiristo?
Uzalendo...
Mgogoro ambao nimefanya utafiti na kuandika research paper: "Islam and Politics in Tanzania," (1989)ni wa EAMWS ambao ulichochewa na serikali.

Sina mwingine ninaoufahamu.
 
Hiyo dhuluma Iko kwenye akili zenu lakini haina uhalisia, kama kweli ingekuepo Tanzania isingekua shwari kwa jinsi waislamu mnavyopenda shari

Papasa,
EAMWS ilivunjwa na serikali mwaka wa 1968 Ili kuzuia isijenge Chuo Kikuu.
 
Papasa,
EAMWS ilivunjwa na serikali mwaka wa 1968 Ili kuzuia isijenge Chuo Kikuu.
Kwani wameendelea kuzuiwa kujenga vyuo tangu huo mwaka 🤔🤔 Mzee achana na hizo habari za mwaka 68, tangu huo mwaka hadi Leo wamepita viongozi wangapi wa kiislamu kwenye serikali wamefanya nini kwa ajili ya dini yenu 🤔 kwenye suala la Elimu ya kidunia nyie hamjalitilia maanani Sana afadhali hata sasa hivi kuna ka muamko kidogo, hiyo dhana ya kusema mnadhurumiwa haina maana huo muda mnao tumia kulalama mngetumia kufanya maendeleo
 
Hakuna elimu isiyokuwa ya dunia, usijidanganye.

Pitia uzi vizuri utapata jibu la swali lako.
 
Kwani wameendelea kuzuiwa kujenga vyuo tangu huo mwaka 🤔🤔 Mzee achana na hizo habari za mwaka 68, tangu huo mwaka hadi Leo wamepita viongozi wangapi wa kiislamu kwenye serikali wamefanya nini kwa ajili ya dini yenu 🤔 kwenye suala la Elimu ya kidunia nyie hamjalitilia maanani Sana afadhali hata sasa hivi kuna ka muamko kidogo, hiyo dhana ya kusema mnadhurumiwa haina maana huo muda mnao tumia kulalama mngetumia kufanya maendeleo
Papasa,
Mbona ghafla umeghadhibika?

Maraisi Waislam hawakuchaguliwa na wananchi kuja kuudumia Uislam.

Wangefanya hivyo wangesababisha vurugu nchini.

Ingekuwa hatujatia maanani elimu EAMWS isingetaka kujenga Chuo Kikuu mwaka wa 1968.

Hapa unelalama ni wewe mimi nakueleza historia ya kweli kumekuwa na njama ndani ya serikali kuwazuia Waislam wasipate elimu.

Waislam wamefanya maandamano mwaka wa 2012 kupinga hujuma za NECTA dhidi ya shule za Kiislam.

Katika miaka ya 1970 OIC ilitaka kujenga Chuo Kikuu serikali ikakataa kutoa kibali.

Huna unachokijua.
 
Uzalendo...
Mgogoro ambao nimefanya utafiti na kuandika research paper: "Islam and Politics in Tanzania," (1989)ni wa EAMWS ambao ulichochewa na serikali.

Sina mwingine ninaoufahamu.
Unapat
Uzalendo...
Mgogoro ambao nimefanya utafiti na kuandika research paper: "Islam and Politics in Tanzania," (1989)ni wa EAMWS ambao ulichochewa na serikali.

Sina mwingine ninaoufahamu.
Hiyo research paper inapatikana wapi?
 
Unapat

Hiyo research paper inapatikana wapi?
Uzalendo....
Kwanza Reseach Paper hii ni Sehemu ya Tatu ya kitabu cha Abdul Sykes.
Research Paper yenyewe ni hiyo hapo chini:
Islam and Politics in Tanzania (1989) Al Haq International (Karachi)

Nakuwekea nyongeza:
Sheikh Hassan bin Ameir - The Moving Spirit of Muslim Emancipation in Tanganyika (1950 – 1968) (Paper presented at Youth Camp Organised by Zanzibar University, World Assembly of Muslim Youth (WAMY) and Tanzania Muslim Students Association (TAMSA) 27th February – 4th March 2004).
 
Ukiona mpaka umri huu mtu anaongelea udini ujue huyo mtu amekosa maarifa
Ed...
Hapana siwezi kuongelea udini.
Naongelea tatizo la kweli linalosibu nchi yetu.

Wajuzi wa mambo wanaponisoma hawaoni hivyo wanaona tatizo tulilonalo.
Haiwezekani watu wakabadili historia ya nchi akaja mtu kuisahihisha akaitwa mdini.

Mdini ni yule aliyeibadili historia kwa hofu ya imani yake.

Iangalie historia ya uhuru wa Tanganyika iliyokuwa inasomeshwa kote nchini na iiangalie historia ya uhuru Tanganyika kama ilivyo katika kitabu cha Abdul Sykes.
Ukiona mpaka umri huu mtu anaongelea udini ujue huyo mtu amekosa maarifa
1703532145077.png
 
TUJIKUMBUSHE HISTORIA YA BAKWATA OCTOBER HADI DECEMBER 1968 SEHEMU YA KWANZA

"... ikadhihirika kuwa serikali ilikuwa imepania kuivunja EAMWS kwa kuwatumia Waislam wachache walioteuliwa kwa kazi hiyo.

Lengo likiwa ni kuanzisha taasisi mpya ambayo serikali itaweza kuiamuru.

Ieleweke hapa kuwa kama tulivyokwisha eleza hapo nyuma, serikali nzima ya Tanzania ilikuwa mikononi mwa Wakristo na watendaji hawa walikuwa wapo chini ya Kanisa.

Hii ilikuwa na maana kuwa kilichotakiwa kuwepo ilikuwa taasisi ya Kiislam ambayo Kanisa itaweza kuiamuru.

Hii ilikuwa ni jambo lazima lifanyike ili kuwadhibiti Waislam kama nguvu inayoweza kuleta mabadiliko ya siasa.

Baada ya kuelewa hali hii ndipo sasa tunaweza kuuangalia kile kilichoitwa ‘’mgogoro’’ wa EAMWS’’ ambao ulidumu kwa miezi mitatu ya mwisho ya mwaka wa 1968.

Ilituweze kuuelewa vyema kisa kizima cha ‘’mgogoro’’ ni muhimu kwanza kuelewa chanzo chake, hadhi za wahusika wakuu na nafasi zao katika ‘’mgogoro’’ ule.

Mwisho, ni muhimu kuweka bayana na kuchambua nafasi ya Julius Nyerere, serikali yake, chama cha TANU na vyombo vya dola katika ‘’mgogoro’’ ule.

Hii itasaidia kuelewa kama kweli ulikuwepo ‘’mgogoro’’ katika EAMWS, au ‘’mgogoro’’ ulibambikizwa na watu katika TANU, serikali na ndani ya Waislam wenyewe ili kuwadhoofisha Waislam kwa nia ya kuwa usije Uislam ukawa na nguvu katika Tanzania hivyo kuwawezesha Waislam kushika madaraka ya nchi."

(Kutoka kitabu cha Abdul Sykes 1998).

Mleta mada serikali ilikuwa sahihi kuvunja Hicho kitu kinaitwa Eamws kama kweli huo ukikuwa mradi wa kitapeli wa Agha Khan kiongozi wa dini ya kishia akiwalaghai waislamu walio wengi wa Tanzania ili wajiunge na shule zake za Agha Khan waliipe mihela kibao

Akipojitia kuanzisha hiyo Taasisi ya waislamu ya Afrika mashariki kusaidia Waislam mojawapi lengo likiwa elimu na afya nk serikali ikafanya tathmini ilipoomba usajili kuwa je watanzania wangapi wamesomeshwa bure primary au sekondary shule za Agha Khan au kutibiwa bure hospital za Agha Khan wakakuta hakuna
Shule na hospitali zake zilikuwa kwa ajiki ya wahindi waislamu wa madhehebu ya Shia Usmailia na wahindi wengine sio waafrika ngozi nyeusi

Serikali ikaona utapeli wa Agha Khan wakafuta hiyo taasisi Tanzania
Uliza hata humu wangapi waislamu waliosomeshwa bure au kutibiwa bure taasisi za Agha Khan ziwe shule au kutibiwa bure hospitali za Agha Khan baada ya yeye kunyimwa usajili au kufutiwa?
Ila kitu cha ajabu kuna waandishi wajitia jutetea uislamu Mohamed Said akiongoza hutetea sana kuwa ohhh hiyo Agha Khan alikuwa na malengo mazuri na waislamu OK alizuiliwa kusajili hiyo taasisi serikali ok serikali ilifuta hiyo taasisi lakini haikumzuia kusomesha waislamu bure shule zake za Agha Khan wala kuwatibu waislamu bure hospital za Agha Khan

Mbona hilo hakulifanya hadi leo ? Lengo lake si lilikuwa kusaidia waislamu? Mbona hadi leo hakuna kusoma bure au kutibiwa bure taasisi za Agha Khan kwa waislamu?

Binafsi katika watu wapotosha historia wasioenda ndani sana Mohamed Said anaongoza muongo mno na hayuko deep kwenye analysis za hoja zake
Uzuri yuko hai hivyo ni vizuri ajue uongo waje akiwa hai

Agha Khan alikuwa tapeli alitaka kutapeli waislamu wa Afrika Mashariki akastukiwa na nchi zote za Africa Mashariki kote kuna mabaraza ya nchi zao ya waislamu siyo Tanzania pekee iliyogoma kote serikali Afrika Mashariki zilimpiga teke Agha Khan aondoke na utapeli wake wa kutaka kutapeli waislamu

Tanzania tuna viongozi wakubwa kibao waislamu hakuna hata mmoja aliyesoneshwa bure na Taasisi ya Agha Kan
 
Yehoda,
Hili lilikuwa moja ya mabango katika maandamano dhidi ya NECTA chini ya uongozi wa Dr. Ndalichako.

Unasemaje?

Kuna maandamano yalifanywa kumkataa Aga Khan au Aziz Khaki au Mufti Sheikh Hassan bin Ameir.

Waislam waliikubali BAKWATA?

Huna unachokijua kuhusu historia ya Waislam.

Isome kwanza ndiyo uje kujadili.
Wahusika wakuu wako kimya hawana mdomo wa kujadili haya.

Wanaogopa.
Unajibu wewe usiyohusika.

1703534374854.png
 
Attachments

  • 1703534282053.png
    1703534282053.png
    222.6 KB · Views: 7
Yehoda,
Hili lilikuwa moja ya mabango katika maandamano dhidi ya NECTA chini ya uongozi wa Dr. Ndalichako.

Unasemaje?

Kuna maandamano yalifanywa kumkataa Aga Khan au Aziz Khaki au Mufti Sheikh Hassan bin Ameir.

Waislam waliikubali BAKWATA?

Huna unachokijua kuhusu historia ya Waislam.

Isome kwanza ndiyo uje kujadili.
Wahusika wakuu wako kimya hawana mdomo wa kujadili haya.

Wanaogopa.
Unajibu wewe usiyohusika.

Waislamu wengi wakati ule elimu kichwani ilikuwa sifuri

OK huyo Aghakhan wakati huo hakupingwa na waislamu tupe majina ya watu mashuhuri waislamu ambao enzi hizo Agha Khan aliwasomesha bure hizo shule zake kabla ya kuleta ulaghai wake kuwa ana lengo la kusaidia waislamu wasome nani aliwasonesha bure? Kabla huo ulaghai wake wa kulaghai waislamu wasiosoma?

Weka majina yao

Tuhakiki kuwa kweli Agha Khan alikuwa na nia nzuri na waislamu waafrika ngozi nyeusi kuwasomesha
 
Ukiona mpaka umri huu mtu anaongelea udini ujue huyo mtu amekosa maarifa
Ed...
Hapana siwezi kuongelea udini.
Naongelea tatizo la kweli linalosibu nchi yetu.

Wajuzi wa mambo wanaponisoma hawaoni hivyo wanaona tatizo tulilonalo.
Haiwezekani watu wakabadili historia ya nchi akaja mtu kuisahihisha ikaitwa mdini.

Mdini ni yule aliyeibadili historia kwa hofu ya imani yake.

Iangalie historia ya uhuru wa Tanganyika iliyokuwa inasomeshwa kote nchini na iiangalie historia ya uhuru Tanganyika kama ilivyo katika kitabu cha Abdul Sykes.
 
Waislamu wengi wakati ule elimu kichwani ilikuwa sifuri

OK huyo Aghakhan wakati huo hakupingwa na waislamu tupe majina ya watu mashuhuri waislamu ambao enzi hizo Agha Khan aliwasomesha bure hizo shule zake kabla ya kuleta ulaghai wake kuwa ana lengo la kusaidia waislamu wasome nani aliwasonesha bure? Kabla huo ulaghai wake wa kulaghai waislamu wasiosoma?

Weka majina yao

Tuhakiki kuwa kweli Agha Khan alikuwa na nia nzuri na waislamu waafrika ngozi nyeusi kuwasomesha
Yehoda,
Mimi si mtu wa ubishani wa staili hiyo yako ya kutoa matusi kuwa ''Waislam ni sifuri kichwani.''

African Association iliasisiwa mwaka wa 1929 na hawa: Kleist Abdallah Sykes, Mzee bin Sudi, Ali Said Mpima, Zibe Kidasi, Suleiman Majisu, Ibrahim Hamisi na Cecil Matola, Raikes Watts na Raikesi Kusi.

Waislam hawa unaowatukana mwaka wa 1933 wakaunda Al Jamiatul Islamiyya Fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika).

Vyama vote hivi viwili vilitumika kupambana na ukoloni wa Muingereza.
Safari ya kwanza ya Nyerere UNO dhifa ya kumuaga Nyerere ilifanywa ndani ya jengo hili la Al Jamiatul Islamiyya Fi Tanganyika.

Mkusanyaji wa fedha za safari ya Nyerere alikuwa Iddi Faiz Mafungo Mweka Hazina wa Al Jamiatul Islamiyy fi Tanganyika na Mweka Hazina wa TANU kadi yake ya TANU ni no. 24.

1703541386324.png

Kulia ni Haruna Iddi Taratibu, Saadan Abdu Kandoro, Julius Nyerere, Sheikh Mohamed Ramiyya na Iddi Faiz Mafungo wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika.​

Sasa tunaweza kuendelea na Aga Khan
Ilibidi tufahamiane kwanza:

Tuanze na makala hiyo hapo chini kisha In Shaa Allah tutaendelea na mengine ikiwa utapendezewa na sharti kuwa hutawatukana wazee wangu waliopigania uhuru wa nchi yetu kwa hali na malii zao:

AGA KHAN PATRON WA EAMWS ALIPOKUTANA NA VIONGOZI WA BAKWATA MIAKA YA 1980
Nakusudia In Shaa Allah kuweka hapa makala mbili au tatu hivi kueleza yaliyotokea baada ya miaka mingi na Aga Khan aliyekuwa Patron wa EAMWS kujaribu upya kusaidia Waislam wa Tanzania lakini safari hii kupitia BAKWATA.

Naamini yapo mafunzo makubwa kwetu na Waislam na wananchi kwa ujumla wataielewa historia ya BAKWATA na viongozi wake.

Aga Khan si mgeni Tanzania na waliomuingiza nchini ni Waislam katika miaka ya 1930 kwa ajili ya kutoa misaada kwa Waislam.

Katika miaka ya 1930 baba yake huyu Aga Khan wa sasa Shah Karim Al Hussein, Sir Sultan Mohamed Shah alitembelea Tanganyika na katika mradi mmoja wapo aliofika kuuangalia ulikuwa ujenzi wa shule ya Al Jamiatul Islamiyya School, Mtaa wa Agrrey na New Street uliokuwa ukijengwa na Waislam chini ya Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika.

Katika hafla ile mwanafunzi aliyesoma risala mbele ya Aga Khan alikuwa Abdul Sykes.

(Miaka mingi baadae Abdulwahid Sykes sasa kijana na mwanasiasa akajachaguliwa kuwa mjumbe katika Bodi ya Elimu ya Aga Khan).

Aga Khan alivutiwa sana na juhudi zile walizoonyesha Waislam wa Tanganyika za kutaka kujiendeleza katika elimu na akatoa fedha zilizowezesha kumaliza ujenzi wa shule yote kwa ukamilifu wake.

Aga Khan akatoa changamoto kwa Waislam wa Afrika Mashariki kuwa Muislam akichanga shilingi moja kwa ajili ya maendeleo ya umma yeye ataoa shilingi moja vilevile juu yake.

Huu ulikuwa sasa wakati wa East African Muslim Welfare Society (EAMWS).

Kitendo hiki cha Aga Khan kilikuwa msaada mkubwa kwa Waislam kwani wakati wa ukoloni ni Ukristo pake yake ndiyo ulikuwa na fursa ya kupata misaada kutoka nje.

Ushirikiano huu wa Aga Khan na Waislam wa Tanganyika uliendelea vizuri sana.
Aga Khan kupitia EAMWS alijenga shule nyingi hadi kufikia sasa kutaka kujenga Chuo Kikuu cha Kiislam chini ya usimamizi wa Mufti Sheikh Hassan bin Amir, Tewa Said Tewa na Aziz Khaki aliyekuwa mwakilishi wa Aga Khan Tanzania.

Hii ilikuwa mwaka 1968 baada ya Tanganyika kuwa huru.

Aga Khan na EAMWS kutaka kujenga chuo kikuu hapo ndiyo matatizo yakaanza baina ya Nyerere na uongozi wa EAMWS.

Kisa hiki ni maarufu hapana haja ya kukirejea.

Sasa tuingie kwenye kisa chenyewe.

Miaka mingi ikapita na mwishowe Nyerere akatoka madarakani na serikali ikashikwa na Ali Hassan Mwinyi.

Kwa takriban miaka 20 Aga Khan hakupata kutia mguu Tanzania.
Katika utawala wa Mwinyi Aga Khan akaja Tanzania.

Katika mazungumzo na Rais Mwinyi, Rais Mwinyi akaomba msaada wa Aga Khan katika nyanja tatu - Elimu, Kilimo na Afya.

Aga Khan akamueleza Rais Mwinyi kuwa Aga Khan walikuwapo Tanzania miaka ya nyuma wakisaidia katika elimu kupitia EAMWS.

Hili suala la elimu likamgusa sana Aga Khan kiasi cha yeye alipomaliza mazungumzo na Mwinyi akamwamrisha Katibu wa Elimu wa Aga Khan Tanzania, Riyaz Gulamani awakaribishe viongozi wa Waislam wa iliyokuwa EAMWS pamoja na viongozi wa BAKWATA katika chakula cha jioni ili wajadili maendeleo ya Waislam.

Katika viongozi wa EAMWS walioalikwa katika hafla ile alikuwa Tewa Said Tewa.
Kutoka BAKWATA walioalikwa walikuwa Sheikh Mkuu wa BAKWATA Hemed bin Jumaa, Adam Nasibu aliyekuwa katibu wa BAKWATA, Mustafa Songambele mzee wa CCM na mwanakamati katika BAKWATA na Waislam wengineo.

Kutoka EAMWS aliyealikwa alikuwa Tewa Said Tewa.

Baada ya chakula Aga Khan akawaeleza nia yake ya kuwaita na akawataka watoe wanachotaka wafanyiwe na Aga Khan katika elimu.

Hapa ndipo ''drama,' ilipoanza.

Akasimama kiongozi mmoja wa BAKWATA na mzee wa CCM, Mustafa Songambele, akamwambia Aga Khan, ''Serikali ya Tanzania inawatosheleza Waislam katika elimu na hawahitaji msaada kutoka kokote.''

Mustafa Songambele...

Naomba nisimame hapa.

Mkasa huu kwa mara ya kwanza alinihadithia Riyaz Gulamani.
Sikuamini kama inaweza kuwa kweli.

Kisa hiki nikaja kuhadithiwa tena na Tewa Said Tewa kama vile alivyonihadithia Riyaz Gulamani.

Hapo ndipo nikaamini kuwa kisa kile hakika kilitokea na Mzee Tewa akanipa na jina la huyo aliyesema maneno yale.

Tuendelee.

Aga Khan kwa upole kabisa akajibu kuwa jana yake alikuwa na Rais na yeye kaomba msaada wa elimu.

Hapo sasa ndipo likazuka zogo baina ya viongozi wa BAKWATA na Waislam wengine mbele ya mgeni Aga Khan.

Kufupisha mkasa.

Kabla hajaondoka kufuatia yale aliyosikia na aliyoshuhudia, Aga Khan akamwambia Riyaz, ''Inaelekea hawa ndugu zetu bado hawajawa tayari lakini ushauri wangu ni kuwa uache mlango wetu wazi.

Siku yoyote watakapokuwa tayari basi tutatoa msaada.''
 
Papasa,
EAMWS ilivunjwa na serikali mwaka wa 1968 Ili kuzuia isijenge Chuo Kikuu.
Mumepewa na B W Mkapa chuo cha TANESCO Morogoro ili kiwe Chuo cha Kiislamu. Niambie nini kinaendelea pale toka mupewe yapata miaka 20 sasa.

Mzee unalalamika sana mpaka unadhalilisha Uislamu
 
Kwani wameendelea kuzuiwa kujenga vyuo tangu huo mwaka 🤔🤔 Mzee achana na hizo habari za mwaka 68, tangu huo mwaka hadi Leo wamepita viongozi wangapi wa kiislamu kwenye serikali wamefanya nini kwa ajili ya dini yenu 🤔 kwenye suala la Elimu ya kidunia nyie hamjalitilia maanani Sana afadhali hata sasa hivi kuna ka muamko kidogo, hiyo dhana ya kusema mnadhurumiwa haina maana huo muda mnao tumia kulalama mngetumia kufanya maendeleo
Huyu mzee ana uraibu wa dini, na uraibu huu ni mbaya kuliko hata madawa ya kulevya. Mohamed Said ni religious fanatic. Huyu akiambiwa vaa mabomu kajilipue kwenye kadamnasi, atavaa tu. Kila kitu maishani mwake anakiangalia kwa udini
 
Back
Top Bottom