Miaka 55 ya BAKWATA: Tujikumbushe Historia Yake na Yaliyotokea October - December 1968

Wacha uwongo wewe mzee. Waisalmu wenye kutaka kusoma wanajuwa mahali pa kupata elimu siyo lazima wakasome chuo kinachoitwa cha Kiislamu.

NECTA unailamumu bure. Ulitaka wakupe alama "B" wakati umepata "F"? Zitaje hizo shule za Kiislamu unazofikiri zilionewa tuzijadili hapa.
 
Mkuu umeliweka vizuri sana. Ika huyu mujahidina Mohamed Said atabisha tu kwa vile kichwa chake kilishajaa bangi ya udini
 
Katika mambo ya hovyo wewe mzee unafanya ni kuwa mwanaharakati wa kiislamu. Tanzania huna nafasi, nenda Somalia kajiunge na Al Shabab kama hawajakupoteza ndani ya Lisaa limoja.

Kweli mtu mwenye akili anaweza akasema NECTA ni Parokia? Kwa taarifa yako shule za Kikristu kwenye mambo ya shule hazina mzaha. Usione St Francis Mbeya au Marian Bagamoyo wamemiliki top spot ya O-Level na A-Level kwenye mitihani ya NECTA kwa miaka 30 sasa ukadhani kuna upendeleo.

Nafahamu viongozi wa juu ambao ni Waislamu waliopeleka watoto wao huko St Francis na Marian. Walipeleka kwa vile wanajuwa thamani ya elimu. Tofauti na wewe unataka tuwe na Chuo Kikuu cha Madrassa. Hovyo
 
Mwinyi, kikwete, na sasa samia wote hawa ni marais waislamu sasa hapa mnaonewaje acha upotoshaji na uongo

Kuhusu elimu matokeo ya wanafunzi yanatolewa kwa number hapo waislamu wanaonewaje
 
Katika mambo ya hovyo wewe mzee unafanya ni kuwa mwanaharakati wa kiislamu. Tanzania huna nafasi, nenda Somalia kajiunge na Al Shabab kama hawajakupoteza ndani ya Lisaa limoja
Walishaona hana madhara, afu hizi harakati zake ni humu tu nje ya jf hana uzito wowote wa kutisha
 
Kwa maneno yako mwenyewe, kumbe Agha Khan alishagundua kiwa "Waislamu wa Tanzania HAWABEBEKI". Maana Rais Mwislamu Mwinyi kamkaribisha kiongozi wa dini ya Kiislamu Agha Khan. Naye Aga Khan kaitisha mkutano wa Waislamu ambao una mchanganyiko wa BAKWATA na EAMWS. Na kwenye mkutano huo HAKUKUWA na MKRISTU hata mmoja. Mumeshindwa KUELEWANA, bado Mohamed Said unawalaumu JK Nyerere na WAKRISTU.

Wewe ni mzee wa HOVYO
 
Mumepewa na B W Mkapa chuo cha TANESCO Morogoro ili kiwe Chuo cha Kiislamu. Niambie nini kinaendelea pale toka mupewe yapata miaka 20 sasa.

Mzee unalalamika sana mpaka unadhalilisha Uislamu
Stunex,
Mimi silalamiki na laiti ningekuwa hivyo ningepata sifa ya ulalamishi.

Mimi nina heshima yangu katika utafiti wa historia ya Tanzania.

Kitabu nilichoandika cha Abdul Sykes kimebadilisha historia ya Julius Nyerere na historia ya uhuru wa Tanganyika.

Utafiti wa tatizo la elimu kwa Waislam limeonyesha yale ambayo waliokuwa wakifanya hujuma wamefahamika.

Nimeweka Research Papers hapa nilizowasilisha vyuo vikuu ndani na nje ya mipaka yetu bahati mbaya hajatokea mtu kati yenu aliyetaka kujadili paper hizi.

Kilicho chepesi kwenu ni uandishi wa jeuri na kejeli.

Stunex,
Mohamed Said kalamu yake haijadhalilisha Uislam.

Picha kutoka Maktaba yake zimethibitisha ukweli wa aandikayo.

Nimekuwekeeni hapa video clips mtazame.

Jukwaa zima likawa kimya.

Nimekuwekeeni clip hapa nazungumza Ikwiriri katika Bibi Titi Festival mbele ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Majaliwa naeleza yaliyotokea nyumbani kwa Ally Sykes Mtaa wa Kipata Nyerere alipokwenda kutoa taarifa kuwa Waingereza wamekataa kusajili TANU kwa kisingizio kuwa chama hakina wanachama.

Hiki kilikuwa kikao cha watu wanne siku ile: Mama mwenye nyumba Bi. Zainab mke wa Ally Sykes. Huyu Ally Sykes kadi yake ya TANU No. 2, Abdul Sykes kadi ya TANU No. 3 na Julius Nyerere kadi ya TANU No. 1 ya Territorial President wa TANU.

Katika kikao hiki cha kujadili usajili wa TANU nikamleta Said Chamwenyewe.

Huyu ndiye Mohamed Said.

Waziri Mkuu alipozungumza kufunga Bibi Titi Festival alisema historia ya kweli isomeshwe wanafunzi wawajue wazalendo waliopigania uhuru wa Tanganyika.
 
Wewe ambae unajikuta unajua Sana unatuletea hadithi za abunuasi zisizokua kua na maana, unakuja kusema wali dhurumiwa ili iweje sasa🤔🤔 haya maandiko yako hayana maana hata kidogo kwenye ulimwengu tulio nao sasa hivi kakusanye wafia dini wenzio ukawahadithie hizo hadithi zako za abunuasi, tena unapaswa kuupuzwa kabisa huna maana
 
Hicho kitabu cha Abdul Sykes ni novel yako tu wewe, haiwezi kamwe ikabadilo historia ya Nyerere na uhuru wa Tanganyika.

Hata hao unaowalilia kama wazee wako mbona Nyerere aliwapa nafasi nyingi tu Serikalini mpaka umauti ulipowafika??

Ajabu unalalamika wewe lakini wao HAWAKUWAHI kulalamika hata Nyerere alipotoka madarakani.
 
Papasa,
Si rahisi kunipuuza na ndiyo sababu wewe hujaweza kufanya hivyo.

Uko hapa unanisoma.

Niandikayo si hadithi ni historia ambayo walijaribu watu kuifuta.

Leo kitabu changu kilichochapwa mwaka wa 1998 kiko toleo la nne kinakwenda la tano.

Kitabu kinajadiliwa hapa JF sasa zaidi ya miaka 10 na kimesababisha niwe Mwandishi Bora Jukwaa la Historia kwa miaka miwili mfululizo 2021 na 2022.

Kitabu changu kiko katika Cambridge Journal of African History kupitia mabingwa wa African History: John Iliffe, Jonathon Glassman na James Brennan.

Utanikuta vilevile ndani ya Dictionary of African Biography (DAB).

Jiulize imekuwaje?
Nini sababu ya haya yote?

Haya hayapatikani kwa kuandika hadithi kama unavyodai.

Uandishi wa riwaya una watu wake lakini mimi sikujaaliwa kuwa kwenye kundi hilo.

Haya yanapatikana kwa kuandika mambo yanayoongeza elimu katika duru za Vyuo Vikuu na kwengineko.
 
Stux...
Hakuna sababu ya kunitukana.
Hivyo utavuruga mjadala.

Tunaweza tukafanya mjadala wa heshima na adabu.

Huu mkutano wa Aga Khan haukuwa kati yake na EAMWS na BAKWATA.

Kikao hichi kilikuwa kati ya Aga Khan na BAKWATA.

Rejea ondoa ghadhabu katika kifua chako na usome upya.

EAMWS ilishapigwa marufuku na Tewa Said Tewa alialikwa kama kiongozi wa zamani wa EAMWS.
 
Historia ya kweli ni ipi?
 
Sijasoma yote ila Bakwata ...ni Taasisi?
Wako serious?

Wana katibu kabisa anaelipwa mishahara?
Au anajitolea?
Wana plans?
Source ya income?
Wana shule ngapi?
Vyuo?
Wana mkurugenzi wa elimu?
Wana vitabu au waandishi vitabu?
Bakwata yote ina PhD ngapi?

Nikipata majibu haya ndo ntakuja kuwachukulia serious..

Wana hata ripoti ya fedha na matumizi ya kila mwaka?
 
Kuwa na adabu. Jibu hoja zake kama huwezi kaa kimya.
Wacha jazba mzee wangu.Historia ya Tanzania imeandikwa na iko sahihi.Tatizo lako ni kutazama.kila kitu katika miwani ya Uislamu.
Unataka kuwa na hati miliki ya ukweli kuhusu Uhuru wa nchi yetu.Acha ushamba
 
Duh
 
Historia ya waislam eeeeeh?Tutajie wasome watano wazalendo waliosomeshwa bure na taasisi za Agha Khan
 
Stux...
Cambridge Journal of African History haichapi mapitio ya vitabu vya riwaya.

Inawezekana wewe unataabika na ukweli lakini walimu wa historia ya Afrika vyuo vingi wanaposomesha historia ya utaifa wa Tanganyika huanza na Kleist Sykes na Dr. Kwegyr Aggrey mwaka wa 1924.

Hapa huwaelekeza wanafunzi kusoma maisha ya wazalendo hawa wawili katika Dictionary of African Biography (Oxford University Press New York 2011) kisha huwaelekeza pia kusoma, Modern Tanzanians, (Tanzania Publishing House, Dar es Salaam 1973) kitabu alichohariri John Iliffe wasome, ''The Townsman Kleist Sykes,'' mwandishi Aisha ''Daisy'' Sykes.

(Unaweza kusoma historia hii Maktaba ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam East Africana: ''The Life of Kleist Sykes,'' Ref. No. JAN/HIST/143/15).

KIsha anawapa rejea ya kitabu cha Abdul Sykes (1998) wasome.

Hakuna mwalimu atakaegusa Historia ya TANU ya Kivukoni na vitabu vingine labda kwa kupita kuwaonyesha wanafunzi umuhimu wa kuandika ''Corrective History.''

Kuna mengine unayoandika nayanyamazia kwa kuwa si maudhui ya mjadala wetu.



 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…