Miaka 60 ya JWTZ Tanzania iwekeze kwenye kinu cha nyuklia

Miaka 60 ya JWTZ Tanzania iwekeze kwenye kinu cha nyuklia

Naangazia mada yangu kwa muktadha wa kutoa maoni kwa tume maalumu ya mipango ya nchi.
Ni wakati muafaka wa kufikiri na kufanyia kazi kwa haraka.

Tanzania kupitia JWTZ ifanye uwekezaji huu muhimu na kwa haraka ili tujitosheleze kwa nishati lakini pia tujiwekeze kiulinzi.

Zama za kutegemea URUSI NA MAREKANI zinaelekea ukingoni.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!!
Kujenga miferji ya maji taka imetushinda tutaweza nyuklia
 
Kama vile wanavomiliki hospitali basi wamiliki pia vyuo vikuu hususani masuala ya engineering za kila namna .
 
Naangazia mada yangu kwa muktadha wa kutoa maoni kwa tume maalumu ya mipango ya nchi.
Ni wakati muafaka wa kufikiri na kufanyia kazi kwa haraka.

Tanzania kupitia JWTZ ifanye uwekezaji huu muhimu na kwa haraka ili tujitosheleze kwa nishati lakini pia tujiwekeze kiulinzi.

Zama za kutegemea URUSI NA MAREKANI zinaelekea ukingoni.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!!
Unadhani kinu cha nukilia ni sawa na Tanesco ambayo kila sehemu umeme unavuja! Nishati hiyo haihitaji machawa, inahitaji watu makini ambao muda wote wapo mtamboni hakuna nimefiwa naenda kuzika, mshikaji sijui kanipigia simu! Utaua watu wote mikoa inayokuzunguruka, sisi bado saaana.
 
Naangazia mada yangu kwa muktadha wa kutoa maoni kwa tume maalumu ya mipango ya nchi.
Ni wakati muafaka wa kufikiri na kufanyia kazi kwa haraka.

Tanzania kupitia JWTZ ifanye uwekezaji huu muhimu na kwa haraka ili tujitosheleze kwa nishati lakini pia tujiwekeze kiulinzi.

Zama za kutegemea URUSI NA MAREKANI zinaelekea ukingoni.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!!
Acheni michezo, sisi bado kwa hilo , leo hata basi bado tunaagiza sembuse kuanzisha na kutunza icho kinu, tutafika ila sio leo na wala kesho na sio jambo la kukimbilia kabla ya kujipanga
 
Jeshi linatakiwa kuwekeza kwenye Teknolojia za kisasa hasa kwenye siraha na vitu vingine vya kijamii kama tuonavyo kwa majeshi ya nchi zilizo fanikiwa sio mambo ya kuvunja tofali kwa kichwa na kutuonesha siraha zilizopitwa na wakati kwenye sherehe za kitaifa
 
Huu uzi ngoja nimtag mwanangu genius,ngoma ngumu mzanaki mzee wa kutokupindisha mambo,mzee wa kuninyooshea
Aje auone

Ova
GENTAMYCINE
 
Unajua operating cost za kinu cha nuclear, safety standards, technical know-how, gharama za ujenzi hata wa kinu kidogo?

Unajua si kila kinu kinaweza zalisha weapons grade Uranium? Chenye uwezo kina gharama kubwa zaidi na teknolojia ya ziada ya kurutubisha?

Na unajua kwamba nchi inayounda silaha za nuclear inapigwa vikwazo? Maana Tanzania ni signatory wa Non-Proliferation Treaty (NPT).

Na unajua kuwa si kazi ya JWTZ kufua umeme? Ni kazi ya Wizara ya Nishati.

Nyinyi ndio mlimshauri yule jamaa akope trilioni 11+ kujenga SGR ya kubebea wasafiri badala ya kuimarisha reli ya kubeba mizigo.
Kinu cha nuclear unakijua weweeee?kama mnataka kinu nenda mwenge pale Kwa wachonga vinyago
Nchi imejaa vilaza kila sekta waliopitishwa madarasa kwa imani na madesa, huo uwezo wa kuendesha mtambo wa nyuklia wataweza vipi wakati hata simple power station za diesel au maji zinawashinda
Miaka 60 ya jeshi ndo kwanza wananunuliwa mabasi.
Watu Hawajui Masuala Ya Kimataifa Na Ulimwengu Unavyokwenda
Kama Wangetaza Sunami Ilipopiga Kinu Cha Nuclear Japan
Serikali Ilipopambana Sana Kukipooza Kisilipuke Kilitikisa Uchumi Wa Nchi Yao Kwa Gharama Kubwa Mpaka Japan Ikayumba
Sasa Huku Kwetu Mwafaa, Na Vikwazo Vyote

Nuclear Siyo Kama BwAwa La Mwalimu
 
Waulize TAEC Tanzania Atomic Emmission Commission wakwambie kama ni rahisi kwa nchi yetu.
Inawekekana sema jeshi lenyewe limekaa kama tawi la CCM, Rwanda wameanza kidogo kidogo wao bado wanavunja matofali kwa meno siku ya muungano
 
Inabadilishe wabadilishe hulka kwanza. kule ukiingia wanakwambia kabisa huku 80% ni nguvu , 20% unatumia akili yako
 
Watu Hawajui Masuala Ya Kimataifa Na Ulimwengu Unavyokwenda
Kama Wangetaza Sunami Ilipopiga Kinu Cha Nuclear Japan
Serikali Ilipopana Kukipooza Kisilipuke Kilitikisa Uchumi Wa Nchi Yao Kwa Gharama
Sasa Huku Kwetu Mwafaa, Na Vikwazo Vyote
Pale Japan kuna maroboti yalipelekwa kwenye kinu yakaharibika kwa mionzi. Wajapani watu poa sana, watu wazima ambao wameishazaa tiyari ndio wakajitolea kwenda kufanya marekebisho kwenye kinu. Wakakataa vijana wasiende maana mionzi inasambaa na inaathiri hata mbegu za mwanaume na za mwanamke unakuta anazaliwa mtoto hana mikono.

Sasa mbongo gani mwenye 50 yrs ajitolee kuingia kwenye hatari na tulivyo wabinafsi. Japan kuna kesi nyingi za watu kujiua kwa aibu wakigundulika wamekwepa kodi kidogo tu.
 
Naangazia mada yangu kwa muktadha wa kutoa maoni kwa tume maalumu ya mipango ya nchi.
Ni wakati muafaka wa kufikiri na kufanyia kazi kwa haraka.

Tanzania kupitia JWTZ ifanye uwekezaji huu muhimu na kwa haraka ili tujitosheleze kwa nishati lakini pia tujiwekeze kiulinzi.

Zama za kutegemea URUSI NA MAREKANI zinaelekea ukingoni.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!!
Wana bunduki SMG zenye magazine ya risasi 30, Wakati Rwanda Uganda wana SMG ya magazine ya risasi 90.

Nyuklia Bado sana kwa nchi inayopambana na kampeni ya NYUMBA NI CHOO NA CHOO MASHULENI.

Bado sana CCM ipo buzy na WIZI WA KURA uchaguzi wa serikali za mitaa, na general election mwakani!!

Kifupi, ni ununuzi wa magari na anasa nyingine nyingi sio investment kwenye jeshi kwa kiwango hicho

Wacha tuendelee na vyoo vya misaada mashuleni kwanza 🤔🤔🤣😂🤣😂
 
Back
Top Bottom