Miaka 60 ya JWTZ Tanzania iwekeze kwenye kinu cha nyuklia

Naangazia mada yangu kwa muktadha wa kutoa maoni kwa tume maalumu ya mipango ya nchi.
Ni wakati muafaka wa kufikiri na kufanyia kazi kwa haraka.

Tanzania kupitia JWTZ ifanye uwekezaji huu muhimu na kwa haraka ili tujitosheleze kwa nishati lakini pia tujiwekeze kiulinzi.

Zama za kutegemea URUSI NA MAREKANI zinaelekea ukingoni.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!!
Tena siku hizi ni mambo nadogo tu hayo, huna haja ya kinu kama yale yakizamani, siku hizi ni (SMRs) tu, inaweza kuwa kila mtaa kama. Matumizi yenu makubwa, unaongezea nyingine pembeni yake (modular).

Ukubwa sawa na gari kama trailer ya freezer. Inafua nguvu za mega watt 300.
 
Naangazia mada yangu kwa muktadha wa kutoa maoni kwa tume maalumu ya mipango ya nchi.
Ni wakati muafaka wa kufikiri na kufanyia kazi kwa haraka.

Tanzania kupitia JWTZ ifanye uwekezaji huu muhimu na kwa haraka ili tujitosheleze kwa nishati lakini pia tujiwekeze kiulinzi.

Zama za kutegemea URUSI NA MAREKANI zinaelekea ukingoni.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!!
Mtu unakaa Dar, maji yanatoka mara moja kwa wiki, nyumbani umejaza madumu ya njano ya kutunzia maji. Na hapo ni Dar es salaam, jiji kubwa. Vijijini ndio usiseme, sehemu nyingine hawajawahi kuona maji ya bomba. Halafu leo upo kwenye daladala ya mbagala rangi tatu, unawaza tuwe na kinu cha nyukilia?
 
Elimu bora yenye kuleta ushindani kwanza kabla ya kinu cha nyuklia.
 
Naangazia mada yangu kwa muktadha wa kutoa maoni kwa tume maalumu ya mipango ya nchi.
Ni wakati muafaka wa kufikiri na kufanyia kazi kwa haraka.

Tanzania kupitia JWTZ ifanye uwekezaji huu muhimu na kwa haraka ili tujitosheleze kwa nishati lakini pia tujiwekeze kiulinzi.

Zama za kutegemea URUSI NA MAREKANI zinaelekea ukingoni.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!!
Labda mzinga wa nyuki
 
Unajua operating cost za kinu cha nuclear, safety standards, technical know-how, gharama za ujenzi hata wa kinu kidogo?

Unajua si kila kinu kinaweza zalisha weapons grade Uranium? Chenye uwezo kina gharama kubwa zaidi na teknolojia ya ziada ya kurutubisha?

Na unajua kwamba nchi inayounda silaha za nuclear inapigwa vikwazo? Maana Tanzania ni signatory wa Non-Proliferation Treaty (NPT).

Na unajua kuwa si kazi ya JWTZ kufua umeme? Ni kazi ya Wizara ya Nishati.

Nyinyi ndio mlimshauri yule jamaa akope trilioni 11+ kujenga SGR ya kubebea wasafiri badala ya kuimarisha reli ya kubeba mizigo.
Hiyo ndio minyororo ya kuikata miaka 60+ ya uhuru wa kweli
 
Yaani ufanye mradi wa nyuklia alafu uwe chini ya jeshi??? Unatafuta vikwazo vikali na kama

Unadhani kinu cha nukilia ni sawa na Tanesco ambayo kila sehemu umeme unavuja! Nishati hiyo haihitaji machawa, inahitaji watu makini ambao muda wote wapo mtamboni hakuna nimefiwa naenda kuzika, mshikaji sijui kanipigia simu! Utaua watu wote mikoa inayokuzunguruka, sisi bado saaana.
Usiogopeshe Kaka
 
Mtu unakaa Dar, maji yanatoka mara moja kwa wiki, nyumbani umejaza madumu ya njano ya kutunzia maji. Na hapo ni Dar es salaam, jiji kubwa. Vijijini ndio usiseme, sehemu nyingine hawajawahi kuona maji ya bomba. Halafu leo upo kwenye daladala ya mbagala rangi tatu, unawaza tuwe na kinu cha nyukilia?
kwa mawazo haya tusingekuwa na SGR au Ndege zetu
 
Mabaki ya uraniam baada ya kuzalisha ni tatizo kubwa liloifanya Ujerumani kuachana na uzalishaji umeme kwa kutumia vinu vya nyuklia. Mabaki hayo yanakuwa na mionzi zaidi na hatari kwa wanadamu kwa zaidi ya miaka 1000 na mahali salama pa kuhifadhi ni sida kubwa. Jana nilimshangaa Waziri Doto akizungumza kama mtu asiyejua tatizo hilo!😳
 
Ni wajerumani wangapi walioathirika kwa hilo?
 
Uli

Uliza swali la maana, vinginevyo unonyesha jina lako "Jingalao" lilivyokukaa! Wenzetu huchukua tahadhari , wewe unafikiria mpaka maafa yatokee na athari mbaya ndio hatua zichukuliwe? Wao wanafunga vinu vilivyopo sasa na hawatajenga vingine!
 
JWTZ iwekeze kwenye Nuclear Reactor na TANESCO wafanye kazi gani?!🤣🤣🤣🤣🤣

Jinga lao ni Jinga lao tu😂

Yote haya ni makosa ya Magufuli kuwatoa Maporini na kuja kuwapa Wazifa Mjini.
 
Uli

Uliza swali la maana, vinginevyo unonyesha jina lako "Jingalao" lilivyokukaa! Wenzetu huchukua tahadhari , wewe unafikiria mpaka maafa yatokee na athari mbaya ndio hatua zichukuliwe? Wao wanafunga vinu vilivyopo sasa na hawatajenga vingine!
Jibu swali ndugu
 
Back
Top Bottom