Miaka 60 ya JWTZ Tanzania iwekeze kwenye kinu cha nyuklia

Tena siku hizi ni mambo nadogo tu hayo, huna haja ya kinu kama yale yakizamani, siku hizi ni (SMRs) tu, inaweza kuwa kila mtaa kama. Matumizi yenu makubwa, unaongezea nyingine pembeni yake (modular).

Ukubwa sawa na gari kama trailer ya freezer. Inafua nguvu za mega watt 300.
 
Mtu unakaa Dar, maji yanatoka mara moja kwa wiki, nyumbani umejaza madumu ya njano ya kutunzia maji. Na hapo ni Dar es salaam, jiji kubwa. Vijijini ndio usiseme, sehemu nyingine hawajawahi kuona maji ya bomba. Halafu leo upo kwenye daladala ya mbagala rangi tatu, unawaza tuwe na kinu cha nyukilia?
 
unawazungumzia hawa hawa wazee wakuvunja matofali?
 
Elimu bora yenye kuleta ushindani kwanza kabla ya kinu cha nyuklia.
 
Labda mzinga wa nyuki
 
Hiyo ndio minyororo ya kuikata miaka 60+ ya uhuru wa kweli
 
Yaani ufanye mradi wa nyuklia alafu uwe chini ya jeshi??? Unatafuta vikwazo vikali na kama

Usiogopeshe Kaka
 
kwa mawazo haya tusingekuwa na SGR au Ndege zetu
 
Mabaki ya uraniam baada ya kuzalisha ni tatizo kubwa liloifanya Ujerumani kuachana na uzalishaji umeme kwa kutumia vinu vya nyuklia. Mabaki hayo yanakuwa na mionzi zaidi na hatari kwa wanadamu kwa zaidi ya miaka 1000 na mahali salama pa kuhifadhi ni sida kubwa. Jana nilimshangaa Waziri Doto akizungumza kama mtu asiyejua tatizo hilo!😳
 
Ni wajerumani wangapi walioathirika kwa hilo?
 
Uli
Ni wajerumani wangapi walioathirika kwa hilo?
Uliza swali la maana, vinginevyo unonyesha jina lako "Jingalao" lilivyokukaa! Wenzetu huchukua tahadhari , wewe unafikiria mpaka maafa yatokee na athari mbaya ndio hatua zichukuliwe? Wao wanafunga vinu vilivyopo sasa na hawatajenga vingine!
 
JWTZ iwekeze kwenye Nuclear Reactor na TANESCO wafanye kazi gani?!🤣🤣🤣🤣🤣

Jinga lao ni Jinga lao tu😂

Yote haya ni makosa ya Magufuli kuwatoa Maporini na kuja kuwapa Wazifa Mjini.
 
Uli

Uliza swali la maana, vinginevyo unonyesha jina lako "Jingalao" lilivyokukaa! Wenzetu huchukua tahadhari , wewe unafikiria mpaka maafa yatokee na athari mbaya ndio hatua zichukuliwe? Wao wanafunga vinu vilivyopo sasa na hawatajenga vingine!
Jibu swali ndugu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…