Miaka 61 ya Uhuru: Japo Tumefanikiwa sana kielimu, shule, vyuo na wasomi (Madaktari na Maprofesa kibao), mbona bado adui ujinga yupo? Tunakwama wapi?

Hakuna mahala tulipofanikiwa kwenye elimu. Toka uongozi wa mkapa kulikuwa na mkakati kabisa wa chini chini wa kushusha kiwango cha Elimu ama kwa kuelewa au bila kuelewa.
Elimu ya ukweli iliishia enzi za Makweta. Kipindi hicho watoto wote wanasoma shule Aina moja,kuanzia watoto wa viongozi,machief wa masikini wote ilikuwa shule moja. Na elimu iliyokuwa inatolewa ilikuwa Bora sana na ndio maana hata viongozi watoto wao tulichanganyikana nao kwenye hizo shule.
Enzi hizo mwanafunzi wa darasa la Saba alikuwa ana uwezo wa kuongea kiingereza vizuri tu hata masomo mengine walikuwa na uwezo pia. Muhimu enzi hizo walikuwa wanaandaliwa pia kujitegemea. Ilikuwa ukishindwa kuendelea na masomo lazima utatoboa kwenye stad zingine kama biashara,ufundi n.k.

Lakini elimu ya sasa mtoto wa form four hamna kitu. Hata mwandiko wake tu kama wa darasa la 5 wa zamani. Pia hawa wa sasa akishindwa tu darasani au hata akimaliza chuo,hana uwezo wa kujitegemea na kujiajiri ndio hawa panya rod na wengine. Na hiyo yote ndio maana nimesema elimu inashushwa makusudi ili familia kubwa zenye uwezo waendelee kuwatawala watoto wa masikini ambao hawajasoma shule nzuri. Viongozi wanajenga madarasa mengi lakini watoto wao wanawapeleka kusoma nje. Huko wanapata elimu Bora kuliko hawa walioshushiwa elimu.

Na ndio maana ni vigumu kwa sasa kwa waliohitimu vyuo bongo kupata ajira nje ya nchi. Tofauti na zamani akina Mseven,Kabila na wengine wamepitia vyuo vyetu walikuwa bora. Pia ndio maana ni vigumu kupambana na nchi jirani kama Kenya kwenye ajira.

Pia hizi shule binafsi kwetu zimechangia sana zimeharibu sana elimu yetu. Ksbb wao wanamfundisha mwanafunzi kukariri sio kuelewa. Pia mwanafunzi wetu ndani anafundishwa namna ya nyingi ya kupata mafanikio tu katika maisha ,ndio maana wengi utasikia somea hii ksbb ina ajira baadae.

HATUJAFANIKIWA KWENYE ELIMU KABISA. KUFANIKIWA KWA ELIMU KIGEZO CHAKE NI WAHITIMU WA VYUO VYETU KUJITAFUTIA AU KUPATA AJILA NJE YA NCHI BILA SHIDA. YAANI MHITIMU AJIUZE KIAJILA NJE YA MIPAKA YA TZ KAMA ILIVYO KWA WAKENYA,NIGERIA,GHANA N.K

NB; UKIKUTANA NA MBONGO NJE YA NCHI KAMA DUBAI NI MUOGA HATARI. YAANI KILA WAKATI ANAOGOPA ANAONA KAMA ATAVUNJA SHERIA YA HUKO. WAKATI HUO HUO KUTANA NA M-NIGERIA,YUKO HURU SANA KSBB NYINGI KWANZA ELIMU,PILI WANAFUNDISHWA SANA NCHINI MWAO NAMNA YA KUJITEGEMEA PIA KIKUBWA WANAFUNDISHWA SANA SHERIA ZA KIMATAIFA. UKIWA NCHI NYINGINE UISHIJE. NA NDIO MAANA WANIGERIA WAMETAPAKAA ULAYA NA AMERICA NA KWINGINEKO KWENYE FURSA NZURI. NA WANA MAFANIKIO MAKUBWA SANA. SISI HATUNA HATA HIYO NDOGO TU KUFUNDISHWA SHERIA NAMNA TU KIDOGO UISHIJE UKIWA NCHI NYINGINE.
 
Kwanza wasomi wengi wamegundua pesa ni bora kuliko elimu na hivyo kuamua kutumia elimu yao kujipatia pesa kwa kila njia (wizi,ufisadi,uongo na uchawa),watu wanaakili nzuri lakini pesa mbele.pili demokrasia nzuri hakuna ambayo ingewasaidia watu wote kuwa huru kuhoji na kushindana kwa hoja kwa uhuru. Nashauri itungwe sheria ya kuwalazimisha wagombea wote wa Urais,ubunge na udiwani kuwa na mdahalo wa live mbele ya wananchi mara 3 katika muda wa kampeni ili tushindanishe hoja na kuangalia hisia zao wakiwa pamoja.
 
Paskali kabla hujauliza wenye PhD wanalisaidiaje taifa kwa elimu yao, jiulize kwanza wewe swali hili..inakuwaje pamoja na elimu yako ya masters bado unadhani ccm inao uwezo kutatua kero za watanzania, je ilikuwa sawa kwa mtu aliyeelimika kama wewe kugombea uongozi kupitia ccm?
Safi sana tuanzie na hili. Kwa walioelimika wote kuanzia Paskal Mayala tukianzia kwenu kuikataa ccm iliyodumaza mifumo yetu yote kuanzia elimu.
 
Ukiachana na wale maadui watatu aliowataja baba wa Taifa yaani ujinga , umaskini na maradhi .

Sasa ameongezeka adui mwingine " UCHAWA" , huyu amekula akili za watu mpaka pamoja na elimu zao wanashindwa kusaidia Taifa kwa kuendekeza kujipendekeza kwa wenye mamlaka kwa manufaa yao.
 
Wanabodi,
Makala ya Jumapili ya leo.
View attachment 2442731View attachment 2442732
Juzi, Ijumaa, Tanzania tumeadhimisha miaka 61 ya Uhuru wa Tanzania, na kiukweli tumefanikiwa sana katika mambo mengi ya kisisasa, kiuchumi na kijamii, ila pia lazima tukubali, hapa tulipo, sipo mahali tungepaswa tuwe, tulipaswa kuwa mbali zaidi ya hapa tulipo!, hivyo “Kwa Maslahi ya Taifa” ya leo, inatafakari kwa juu juu, tulipaswa kuwa wapi na kujiuliza, jee tunakwama wapi?.

Tulipopata uhuru ile 1961, tulikuwa tunakabiliwa na maadui wakuu watatu wa taifa, hivyo tukatangaza vita dhidi ya adui ujinga, umasikini na maradhi. Leo miaka 61 ya uhuru, sio tuu maadui hao wangalipo, bali tumeongeza maadui wengine wawili, tumeongeza adui rushwa na ufisadi ambao hawakuwepo wakati tunapata uhuru.

Adui Ujinga.
Wakati tunapata uhuru, nchi yetu ilikuwa na majimbo, elimu ilikuwa ni ya kulipia, hivyo ni watoto wa kutoka majimbo yenye mazao ya biashara, yakiongozwa na kahawa, hivyo watu wa Bukoba, Kilimajaro, Arusha na Mbeya, ndio watoto wao walisoma kwasababu wazazi wao waliweza kulipa karo ya shule. Jimbo la Nyanza, lenye mikoa ya kanda ya ziwa, wao walikuwa na Pamba, Tanga wakasomeshwa na Katani. Mikoa isiyokuwa na mazao ya biashara kama Singida, Dodoma, Mikoa ya Kusini na Pwani, wao waliokolewa na kusomeshwa na Waseminari.

Hivyo makabila kama Wahaya, Wachagga na Wanyakyusa wengi kupata fursa za kujiendeleza kielimu na kuonekana kama makabila haya wana akili sana, kutokana na uwezo wa kulipiwa karo.

Rais wa Tanganyika, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, kwa kulijua hili, akatangaza elimu bure, kuanzia darasa la kwanza, hadi chuo kikuu, hii ikafungua fursa za elimu kwa Watanzania wote, na tuliendelea kufanya mitihani inayotungwa Cambridge, Uingereza. Hata baada ya kuanza elimu bure, bado waliopasi wengi mitihani hiyo, bado walikuwa ni watoto wa makabila yale yale.

Tukaachana na mitihani ya wazungu, tukaanzisha Baraza letu la mitihani, tukatunga wenyewe mitihani rafiki, lakini bado waliopasi wengi ni kutoka makabila yale yale!. Ili watu wa makabila yote wapate fursa sawa za kujiendeleza, serikali ya Nyerere ikaamua kuweka viwango tofauti tofauti vya ufaulu kwa baadhi ya mikoa, na kwa mikoa mingine viwango vikashushwa mpaka chini ya alama 50% ili kila Mtanzania aweze kuingia sekondari. Hii ikasaidia saidia watoto wa makabila yote kuingia sekondari.

Kwa yale makabila ya hali ya chini sana kama Wahadzabe na Wataturu, hawa hawakujua shule, hawaongee lugha ya Kiswahili na wanaishi maporini, serikali iliwakamata kwa nguvu watoto wa familia hizo, na kuwapeleka kwa nguvu shule za bweni na kusomeshwa chini ya ulinzi.

Japo wote hawakufaulu hata kiwango cha chini kabisa, bado serikali iliwaingiza sekondari kwa nguvu kwenye shule za bweni, mwanzo ilianza na Ilburu, wenzao wakawa wanawaona na kuwatorosha wote, ndipo serikali ikawapeleka Shule ya Sekondari ya Pugu, hapo walisoma mpaka kidato cha 4, japo wote hawakufaulu, lakini angalau walijua kusoma, kuandika na ustaarabu wa kuvaa nguo.

Serikali ikawarudisha kujiunga na jamaa zao, kwa kuwapa na zawadi za nguo nyingi za kuwavisha jamii nzima, wakawaacha kijijini kwao, baada ya mwezi, wakaenda kuwatembelea kukagua maendeleo yao, walishangaa, sio tuu zile nguo walizikuta pale pale walipowaacha, bali hata nguo za wale waliosomeshwa na kustaarabika, nao walizivua pale pale na kuziacha pale pale, na kuvaa mavazi yao ya asili!.

Juhudi za Awamu ya kwanza kupambana na adui ujinga ziliendelea kwa kuanzisha elimu ya watu wazi, kisomo cha ngumbaru, na kuibadili mitaala ya elimu kuwa na elimu ya kujitegemea na kuanzisha vyuo vya ufundi nchi nzima. Elimu ya mkoloni ililenga kupata makarani, baada ya uhuru tukaanzisha elimu ni kazi, elimu ya kujitegemea, ili lengo la kuelimika sio tuu ili kuajiriwa bali kujiajiri.

Kuna kipindi, nchi ya Tanzania ndio ilikuwa nchi kiongozi barani Afrika kwa literacy level ya watu wanaojua kusoma na kuandika. Hiki kiwango kwa sasa kimeshuka, sijui tunakwama wapi?.

Kwa sasa karibu kila kata ina shule ya sekondari, kila mkoa kuna vyuo vya ufundi stadi. Tulipopata uhuru, tulikuwa na chuo kikuu kimoja tuu, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kwa jina maarufu UDSM, na fani ya kwanza ni sheria, sasa tuna vyuo vikuu vingi na fani nyingi, tunatoa wahitimu wengi, tuna maprofesa na madaktari wa Ph.D wa kutosha, kutoka vyuo vikuu vya kuheshimika na kueleweka hadi vyuo vikuu vya mtandaoni, ambayo vinatoa Ph.D hata kwa darasa la saba kama Ph.D ya Mhe. Joseph Kasheku Msukuma.

Na majuzi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kimemtunuku Rais Samia, shahada ya heshima ya udaktari wa Falsafa, iitwayo Honoria Causa, hivyo Rais Samia sasa ni Dr. Samia Suluhu Hassan, japo kikawaida madakitari wa Honoria Causa, hawapaswi kutumia jina la Dr, lakini kwa Tanzania, jina hilo limetumika kwa Dr. Jakaya Kikwete na Dr. Reginald Mengi, hivyo hakuna ubaya jina hilo likitumiwa na Rais Samia, kuwa sasa atambuliwe rasmi kama Rais Dr. Samia Suluhu Hassan, na nashauri lile jina la Mama Samia, sasa life, libaki ofisini kwake, nyumani kwenye familia yake na kwa watu wake wa karibu. Nami nijiunge na Watanzania wenzagu kumpongeza Rais Samia kutunukiwa Ph.D ya heshima, hongera sana Rais wetu Samia kutunukiwa udakitari wa falfasa, ni heshima kubwa kwako na kwa taifa kwa ujumla. Swali hawa ma Ph.D tulionao wa kumwaga, jee wanalisaidiaje taifa letu kusonga mbele?. tunakwama wapi?.

Naomba kwa leo niishie hapa, wiki ijayo nitaangazia miaka 61 ya uhuru kwenye mapambano dhidi ya adui umasikini, kiukweli kabisa Watanzania wengi bado ni masikini, jee tunakwama wapi?.

Nawatakia heri ya Uhuru na Jamhuri.

Paskali
Ma Professa kama Mwigulu anaechanganya deni la makampuni binafsi na deni la serikali.
 
Walioelimika ndo hawa wanaigeuza nchi kuwa soko la China badala ya kuwa wazalishaji malighafi kwa Kilimo?
Hao walioelimika wanashindwa kuleta Uwekezaji mkubwa wa Kilimo kwenye Nchi inayolimika Kila Wilaya na wanaendelea kung'ng'ania VIWANDA vya YEBO YEBO ambavyo ni mabomba ya hela yetu kwenda China??
Wasomi wasifu Ujenzi wa VIWANDA kwenye Nchi isiyo na Malighafi...
 
Inawezekana ule ujinga wa kutojua kusoma na kuandika umetoka, nadhani tafsiri ya ujinga iende mbele zaidi ya kujua kusoma na kuandika.

Kusoma na kuandika ni tools za kuondoa ujinga, baada ya kuwa na hizo tools, kama taifa, Sasa tujue ni ujinga gani tunao ili tukaufute.
 
Kwa bahati mbaya sana wanaoitwa wasomi ndio wamegeuka wajinga kuliko wale ambao hawajaenda shule kabisa! Ukitaka kupima ujinga wa wasomi wetu, fuatilia mambo yanayofanywa na wanasiasa wasomi walioko ndani ya CCM. Utashangaa kuona mtu ana vyeti vya usomi na anajua wapi jina la Dr. litumike, lakini anamwita mama Samia Dr!

Kwa maneno marahisi ni ngumu kutofautisha msomi na mtu ambaye hajaenda shule kabisa. Hii ni dhahiri kuwa tuna majengo ya kutolea elimu, lakini elimu inayotolewa ina ubora hafifu sana.
Umenikumbusha kisa cha dada mmoja muhitimu wa PhD muhimbili alipomugomea rais Mwinyi.
 
Naomba utukumbushe, mdada, msomi, kamgomea rais wa nchi?!. Sio lazima kumtaja jina ila tukumbushe kisa.
P
 
Tafsi ya kawaida ya MSOMI ni hali ya kukabiliana na matatizo na kuyachanganua kwa mapana na si, vinginevyo.
kama tukishidwa kujua nadharia hii ni vyema tungepunguza idadi ya Dr na prof,kwa maana ya uhaba wao kulitumia vizuri maarifa waliyo yapata.
Kuleta madhara kwenye jamiii zetu na Taifa kwa ujumla
 
Wanabodi,
Makala ya Jumapili ya leo.
View attachment 2442731View attachment 2442732
Juzi, Ijumaa, Tanzania tumeadhimisha miaka 61 ya Uhuru wa Tanzania, na kiukweli tumefanikiwa sana katika mambo mengi ya kisisasa, kiuchumi na kijamii, ila pia lazima tukubali, hapa tulipo, sipo mahali tungepaswa tuwe, tulipaswa kuwa mbali zaidi ya hapa tulipo!, hivyo “Kwa Maslahi ya Taifa” ya leo, inatafakari kwa juu juu, tulipaswa kuwa wapi na kujiuliza, jee tunakwama wapi?.

Tulipopata uhuru ile 1961, tulikuwa tunakabiliwa na maadui wakuu watatu wa taifa, hivyo tukatangaza vita dhidi ya adui ujinga, umasikini na maradhi. Leo miaka 61 ya uhuru, sio tuu maadui hao wangalipo, bali tumeongeza maadui wengine wawili, tumeongeza adui rushwa na ufisadi ambao hawakuwepo wakati tunapata uhuru.

Adui Ujinga.
Wakati tunapata uhuru, nchi yetu ilikuwa na majimbo, elimu ilikuwa ni ya kulipia, hivyo ni watoto wa kutoka majimbo yenye mazao ya biashara, yakiongozwa na kahawa, hivyo watu wa Bukoba, Kilimajaro, Arusha na Mbeya, ndio watoto wao walisoma kwasababu wazazi wao waliweza kulipa karo ya shule. Jimbo la Nyanza, lenye mikoa ya kanda ya ziwa, wao walikuwa na Pamba, Tanga wakasomeshwa na Katani. Mikoa isiyokuwa na mazao ya biashara kama Singida, Dodoma, Mikoa ya Kusini na Pwani, wao waliokolewa na kusomeshwa na Waseminari.

Hivyo makabila kama Wahaya, Wachagga na Wanyakyusa wengi kupata fursa za kujiendeleza kielimu na kuonekana kama makabila haya wana akili sana, kutokana na uwezo wa kulipiwa karo.

Rais wa Tanganyika, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, kwa kulijua hili, akatangaza elimu bure, kuanzia darasa la kwanza, hadi chuo kikuu, hii ikafungua fursa za elimu kwa Watanzania wote, na tuliendelea kufanya mitihani inayotungwa Cambridge, Uingereza. Hata baada ya kuanza elimu bure, bado waliopasi wengi mitihani hiyo, bado walikuwa ni watoto wa makabila yale yale.

Tukaachana na mitihani ya wazungu, tukaanzisha Baraza letu la mitihani, tukatunga wenyewe mitihani rafiki, lakini bado waliopasi wengi ni kutoka makabila yale yale!. Ili watu wa makabila yote wapate fursa sawa za kujiendeleza, serikali ya Nyerere ikaamua kuweka viwango tofauti tofauti vya ufaulu kwa baadhi ya mikoa, na kwa mikoa mingine viwango vikashushwa mpaka chini ya alama 50% ili kila Mtanzania aweze kuingia sekondari. Hii ikasaidia saidia watoto wa makabila yote kuingia sekondari.

Kwa yale makabila ya hali ya chini sana kama Wahadzabe na Wataturu, hawa hawakujua shule, hawaongee lugha ya Kiswahili na wanaishi maporini, serikali iliwakamata kwa nguvu watoto wa familia hizo, na kuwapeleka kwa nguvu shule za bweni na kusomeshwa chini ya ulinzi.

Japo wote hawakufaulu hata kiwango cha chini kabisa, bado serikali iliwaingiza sekondari kwa nguvu kwenye shule za bweni, mwanzo ilianza na Ilburu, wenzao wakawa wanawaona na kuwatorosha wote, ndipo serikali ikawapeleka Shule ya Sekondari ya Pugu, hapo walisoma mpaka kidato cha 4, japo wote hawakufaulu, lakini angalau walijua kusoma, kuandika na ustaarabu wa kuvaa nguo.

Serikali ikawarudisha kujiunga na jamaa zao, kwa kuwapa na zawadi za nguo nyingi za kuwavisha jamii nzima, wakawaacha kijijini kwao, baada ya mwezi, wakaenda kuwatembelea kukagua maendeleo yao, walishangaa, sio tuu zile nguo walizikuta pale pale walipowaacha, bali hata nguo za wale waliosomeshwa na kustaarabika, nao walizivua pale pale na kuziacha pale pale, na kuvaa mavazi yao ya asili!.

Juhudi za Awamu ya kwanza kupambana na adui ujinga ziliendelea kwa kuanzisha elimu ya watu wazi, kisomo cha ngumbaru, na kuibadili mitaala ya elimu kuwa na elimu ya kujitegemea na kuanzisha vyuo vya ufundi nchi nzima. Elimu ya mkoloni ililenga kupata makarani, baada ya uhuru tukaanzisha elimu ni kazi, elimu ya kujitegemea, ili lengo la kuelimika sio tuu ili kuajiriwa bali kujiajiri.

Kuna kipindi, nchi ya Tanzania ndio ilikuwa nchi kiongozi barani Afrika kwa literacy level ya watu wanaojua kusoma na kuandika. Hiki kiwango kwa sasa kimeshuka, sijui tunakwama wapi?.

Kwa sasa karibu kila kata ina shule ya sekondari, kila mkoa kuna vyuo vya ufundi stadi. Tulipopata uhuru, tulikuwa na chuo kikuu kimoja tuu, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kwa jina maarufu UDSM, na fani ya kwanza ni sheria, sasa tuna vyuo vikuu vingi na fani nyingi, tunatoa wahitimu wengi, tuna maprofesa na madaktari wa Ph.D wa kutosha, kutoka vyuo vikuu vya kuheshimika na kueleweka hadi vyuo vikuu vya mtandaoni, ambayo vinatoa Ph.D hata kwa darasa la saba kama Ph.D ya Mhe. Joseph Kasheku Msukuma.

Na majuzi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kimemtunuku Rais Samia, shahada ya heshima ya udaktari wa Falsafa, iitwayo Honoria Causa, hivyo Rais Samia sasa ni Dr. Samia Suluhu Hassan, japo kikawaida madakitari wa Honoria Causa, hawapaswi kutumia jina la Dr, lakini kwa Tanzania, jina hilo limetumika kwa Dr. Jakaya Kikwete na Dr. Reginald Mengi, hivyo hakuna ubaya jina hilo likitumiwa na Rais Samia, kuwa sasa atambuliwe rasmi kama Rais Dr. Samia Suluhu Hassan, na nashauri lile jina la Mama Samia, sasa life, libaki ofisini kwake, nyumani kwenye familia yake na kwa watu wake wa karibu. Nami nijiunge na Watanzania wenzagu kumpongeza Rais Samia kutunukiwa Ph.D ya heshima, hongera sana Rais wetu Samia kutunukiwa udakitari wa falfasa, ni heshima kubwa kwako na kwa taifa kwa ujumla. Swali hawa ma Ph.D tulionao wa kumwaga, jee wanalisaidiaje taifa letu kusonga mbele?. tunakwama wapi?.

Naomba kwa leo niishie hapa, wiki ijayo nitaangazia miaka 61 ya uhuru kwenye mapambano dhidi ya adui umasikini, kiukweli kabisa Watanzania wengi bado ni masikini, jee tunakwama wapi?.

Nawatakia heri ya Uhuru na Jamhuri.

Paskali
Paskali asante kwa mada nzuri na imenipa kutafakari kiasi. Matokeo ya kutafakari kwangu nimeona pana shida moja kubwa kwamba kupiga vita adui ujinga kulihusisha eneo moja tu kusoma na kuandika na maeneo mengine yakaachwa. Hili la kuhimiza kusoma na kaundika halikuja kwa bahati mbaya ilipangwa kwa matarajio kuwa watu wakijua kusoma na kauandika ni rahisi kutafuta na kutumia maarifa. Sasa waliosoma na kujua kuandika wamebaki na kujua kusoma na kuandika tu hawatumii silaha zao; wanaozitumia 90% wanazitumia vibaya. Hapa ndipo tatizo lilipo, tukijinasua hapo tutafanikiwa vinginevyo vita ya kupiga ujinga ni endelevu na kibaya sana binafsi
 
Hatujakwama. Ni kwamba binadamu wapya wanazaliwa kila siku, na wanazaliwa wakiwa wajinga (yaani hawajui kitu) na wakiwa maskini (yaani hawamiliki mali yoyote).

Kwa hiyo kazi ya kupiga vita ujinga na umaskini ni kazi ya kudumu. Haina mwisho.
 
Back
Top Bottom