Miaka 63 baba mdogo hajawahi kurudi nyumbani

Inauma Sana...hata sisi shangazi yetu alijifungua mwaka 1963! Naskia akawa anatoka kinyesi...jamii ikamtenga..akaona isiwe kesi...ndo hii sasa tunaita "fistula!
Tunajiulizaga sijui alipona au alikufa! Aliondoka na mwanaye[emoji24][emoji24]
Dah pole sana mkuu inasikitisha sana nadhani kipindi hicho tiba mbadala ilikuwa haijapatikana bado
 
Maisha haya wamejaa mambo mengi sana hasa ya utafutaji.

JE umeshawahi kupotezana na ndugu yako wa tumbo ,binamu yako,BA mkubwa au ba mdogo ,shangazi ,mama au Baba,bibi au babu ,mpwa rafiki yako au hata jirani yako,BA mkwe au ma mkwe unawasikia sikia tu wapo mahali fulani lakini kutokana na maisha yetu haya kitanzania umeshindwa kwenda kumtafuta huko mikoani alikokimbilia.

Binafsi baba yetu huwa anatuambia anaye kaka yake mkubwa ambae aliondoka nyumbani toka mwaka 1957 hadi sasa hajawahi kurudi ila ana watoto wapo WAKUBWA kama watano nao aliwaacha wakiwa wadogo...Kati yao watatu wapo Uingereza na wenyewe waliondoka mwaka tokea mwaka 1983 na hawajai kurudi tunasikia tu story mmoja yupo Kigoma na mmoja tunamsikiaga tu Tbc Taifa ila huyo wa kigoma ndo huwa anatutembelea.

Sababu za kuondoka nyumbani tunaambiwa ni kutafuta maisha ila tulishafanya kila njia kumtangaza kupata imeshindika tumetumia radio na magazeti hatujwahi kumpata..mtoto wake huyo anaekaa kigoma alimsikia babake kuwa yupo Singida akaanza pori kwa pori lakini wapi...Kuna mtu akamwambia yupo Ruvuma akaanza ardhi kwa ardhi lakini wapi...
Kubwa zaidi aliondoka akiwa hajawahi kupiga hata picha ,huwa tunatamani kumuona huyo dingi d lakini imeshindikana.

Hapa ina maana ba mdogo wetu huyu hajui hata sura ya ndugu zake ,hajawahi kuhudhuria msiba wa baba yake wala mama yake ...

Wengine huwa tunajisemea bado hai muda mwingine tunajisemea tu huyo alishachukuliwa na mbingu ...
Je una ndugu amewahi kuondoka nyumbani na hajawahi kurudi na kwa nini ,sababu za kuondoka nyumbani ni nini ?
Njia gani umewahi kutumia ili kufanikiwa umpate?

Je ni kweli kuwa kuna dawa za kuwarudisha watu waliopotea au kuondoka nyumbani ?

Unajisikiaje kusikia ndugu yako kukimbia nyumbani

Je kuwa mlowezi ni laana?
Je tutumie chanjo kama iliyompata Osama kwa kutafuta vinasaba?
mama yangu alikuwaga na mjomba wake sasa ni marehemu akiondoka kwao kijijini mikese morogoro, mama akiwa bado mtoto mdogo, alienda tanga ila hakuwa na mawasiliano na kwao, hadi mama akakua na sisi tukazaliwa alirudi kwa kurudishwa mimi nikiwa niko sekondari tayari

tena kurudishwa kwenyewe ni kuwa alikuwa anaumwa sasa watu wa huko wakaona huyu mtu atatufia wakatafuta ndugu zake , wakampata kakaake wakamtumia nauli kaka ke akaenda huko tanga akakabidhiwa ndugu yake akamrudisha morogoro.
hakukaa sana akafariki,

imagine aliondoka miaka ya 1980s mwanzoni, akajakurudi miaka ya 2000 mwishoni
 
Mimi baba mdogo wangu nahadithiwa tu sikuwahi kumuona nilikuwa bado sijazaliwa, alikuwa akiishi Uganda akifanya biashara. Kipindi kile Idd Amin amechukua nchi, sasa baada ya hhali kuwa mbaya alikuwa ana mke wake na mtoto mdgo akiwa na miaka miwili akawambia watangulie yeye atakuja baada ya siku mbili afanye utaratibu wa kuuza mali zake ili aondoke.
Wakatangulia wakafika salama na wafanyabiashara watanzania wenzake.
Yeye hakuwahi kurudi, mpaka leo wakassume kuwa aliuawa.
 
Duh pole sana mkuu ndio maisha lakini ila sijajua nini kinapelekea mtu kuondoka home na kupotelea huko mbali kwenye miji ya watu pasipo kukumbuka kurudi home
 
Mimi baba mdogo wangu nahadithiwa tu sikuwahi kumuona nilikuwa bado sijazaliwa, alikuwa akiishi Uganda akifanya biashara. Kipindi kile Idd Amin amechukua nchi, sasa baada ya hhali kuwa mbaya alikuwa ana mke wake na mtoto mdgo akiwa na miaka miwili akawambia watangulie yeye atakuja baada ya siku mbili afanye utaratibu wa kuuza mali zake ili aondoke.
Wakatangulia wakafika salama na wafanyabiashara watanzania wenzake.
Yeye hakuwahi kurudi, mpaka leo wakassume kuwa aliuawa.
Duh huu uzi unauzunisha sana aisee
 
Nina kaka yangu naambiwa aliondoka nyumbani miaka ya 1978 kwenda SA kutafuta maisha lakn baadae kutaja kuambiwa kuwa alishahamia nchini Malawi na ameoa huko. Tulianza Kumfuatilia lakn tulipofika Malawi mji aliokuwa anakaa wakasema alishahama na hawajui amehamia wapi.

Huyo brother mpaka leo hii sijawahi kumtia machoni na mbaya zaidi baba zetu wote pamoja na shangazi walishafariki na hajui kama hao ndg zake hawapo hai tena. Inaumiza sana haya maisha haya
 
Maisha haya wamejaa mambo mengi sana hasa ya utafutaji.

JE umeshawahi kupotezana na ndugu yako wa tumbo ,binamu yako,BA mkubwa au ba mdogo ,shangazi ,mama au Baba,bibi au babu ,mpwa rafiki yako au hata jirani yako,BA mkwe au ma mkwe unawasikia sikia tu wapo mahali fulani lakini kutokana na maisha yetu haya kitanzania umeshindwa kwenda kumtafuta huko mikoani alikokimbilia.

Binafsi baba yetu huwa anatuambia anaye kaka yake mkubwa ambae aliondoka nyumbani toka mwaka 1957 hadi sasa hajawahi kurudi ila ana watoto wapo WAKUBWA kama watano nao aliwaacha wakiwa wadogo...Kati yao watatu wapo Uingereza na wenyewe waliondoka mwaka tokea mwaka 1983 na hawajai kurudi tunasikia tu story mmoja yupo Kigoma na mmoja tunamsikiaga tu Tbc Taifa ila huyo wa kigoma ndo huwa anatutembelea.

Sababu za kuondoka nyumbani tunaambiwa ni kutafuta maisha ila tulishafanya kila njia kumtangaza kupata imeshindika tumetumia radio na magazeti hatujwahi kumpata..mtoto wake huyo anaekaa kigoma alimsikia babake kuwa yupo Singida akaanza pori kwa pori lakini wapi...Kuna mtu akamwambia yupo Ruvuma akaanza ardhi kwa ardhi lakini wapi...
Kubwa zaidi aliondoka akiwa hajawahi kupiga hata picha ,huwa tunatamani kumuona huyo dingi d lakini imeshindikana.

Hapa ina maana ba mdogo wetu huyu hajui hata sura ya ndugu zake ,hajawahi kuhudhuria msiba wa baba yake wala mama yake ...

Wengine huwa tunajisemea bado hai muda mwingine tunajisemea tu huyo alishachukuliwa na mbingu ...
Je una ndugu amewahi kuondoka nyumbani na hajawahi kurudi na kwa nini ,sababu za kuondoka nyumbani ni nini ?
Njia gani umewahi kutumia ili kufanikiwa umpate?

Je ni kweli kuwa kuna dawa za kuwarudisha watu waliopotea au kuondoka nyumbani ?

Unajisikiaje kusikia ndugu yako kukimbia nyumbani

Je kuwa mlowezi ni laana?
Je tutumie chanjo kama iliyompata Osama kwa kutafuta vinasaba?
Mkuu mbona hiyo mikasa ni mingi tu.
Kuna babu yangu mdogo aliondoka makwetu mara baada ya uhuru na hakurudi miaka yote hadi karibia miaka 15 iliyopita.
Alienda mikoa ya kaskazini na tulikuwa wala hatujawahi kumwona.
Baba yangu alikuwa amezeeka na anaumwa, huyo babu mdogo ndio naye akarudi, na alikaa na baba yangu muda mdogo tu, baba yangu akafariki.

Baba yangu ndio alikuwa mrithi wa ukoo kutoka kwa baba yake ambaye ndo babu yangu.
Babu yangu ujanani mwake alimmege ardhi mdogo wake ambaye ndiyo huyu babu mdogo aliyepotea kwa miongo baada ya uhuru.

Huyu babu mdogo alipotoka huko alikotoka kaanza na kesi, anataka ardhi aliyopewa na kaka yake, babu yangu.
Ardhi ile sasa inakaliwa na ndugu wengine walioilima na kuiendeleza na inapendeza, wao waliachiwa na baba zao ambao walishatangulia mbele za haki.
Kimsingi sasa wanaokalia ardhi ya babu mdogo ni baba zangu wadogo, lakini mimi sasa hivi ndio dingi wa ukoo.

Sasa hapo patamu.
Babu mdogo anakuja mbogo anataka mie kiongozi wa ukoo niwatoe baba zangu wadogo kwenye ardhi waliyoiendeleza kwa miaka zaidi ya 40!

Imebidi nimueleze kwa upole tu kuwa hii si kesi yangu, waamuzi wa kesi yake wote walikwisha kufariki!
Hivyo nikamshauri atafute kapori , afyeke na aanze kulima.
Katika umri wa miaka 70 huo tayari ni mtihani.
 
kaz kweliii
 
Kuna jamaa aliondoka kijijini miaka ya 90 mwanzoni. Hakwenda mbali. Alikwenda mkoa wa jirani tu. Tangu muda huo hajawahi kurudi nyumbani. Ndugu wanakufa na kuzikwa, yeye yupo tu huko mkoa jirani. Aliacha mwanamke na watoto wadogo kijijini. Watoto wakwishakuwa wakubwa, wameoa na wana watoto pia. Yeye nasikia huko aliko alioa mke mwingine na ana watoto wengine. Mke wake wa kijijini alizaa watoto wengine na wahuni wa kijijini.
 
Hahaha mimi nilidhani ukiisha kua mtu mzima ni sharti sasa ujitafutie maisha yako?!

Hivi ukitoka Kagera ukahamia Dar es Salaam, kuna ulazima wa kurudi Kagera?!

Kufanikiwa au kutofanikiwa kwenye maisha haya kuna asilimia sawa, uwe kwenu au uhame kwenu.

Sasa mtu aliyeondoka Mbeya akaamua kuishi Mwanza ana ulazima gani wa kurudi Mbeya, kama Mwanza anaishi awezavyo?!
Mi nadhani kama una muhitaji mtu wewe ndiye unapaswa kumtafuta, yeye halazimiki kumtafuta yeyote, labda kama naye ana wahitaji nyie.

Maisha popote, na aina ya maisha huchagua muhusika, au maisha humchagulia, sasa akirudi nyumbani huko akiwa mzee au kijana kuna faida gani kwenu au kwake?!

Wazazi wawengi wamehamia Dar es Salaam kutokea mikoa mingine, wamejenga na kuwa na watoto wakiwa Dar es Salaam, wengi hawaendi mikoani waliko toka hadi mauti kuwakuta na kuzikwa Dar es Salaam, lakini haimaanishi wameishi maisha magumu.

Unaishi wapi nadhani ni chaguo la muhusika.

Shida au raha ni sehemu ya maisha, hakuna guarantee yoyote kwenye maisha.

Mki walaumu mnawaonea, maisha sio mchezo wa kuigiza au ni kamali, unaweza kufanikiwa au kukosa kabisa.

Amini Mungu yupo labda utafanikiwa.
 
Inauma Sana...hata sisi shangazi yetu alijifungua mwaka 1963! Naskia akawa anatoka kinyesi...jamii ikamtenga..akaona isiwe kesi...ndo hii sasa tunaita "fistula!
Tunajiulizaga sijui alipona au alikufa! Aliondoka na mwanaye😭😭
Hii imeniumiza sana sijui alimwambia nn mwanae alipoulizia kuhusu ndugu zake. Mngejaribu kumtafuta hata huyo mwanae nahisi hata mama mtu atafarijika sana.
 
Maisha haya wamejaa mambo mengi sana hasa ya utafutaji.

JE umeshawahi kupotezana na ndugu yako wa tumbo ,binamu yako,BA mkubwa au ba mdogo ,shangazi ,mama au Baba,bibi au babu ,mpwa rafiki yako au hata jirani yako,BA mkwe au ma mkwe unawasikia sikia tu wapo mahali fulani lakini kutokana na maisha yetu haya kitanzania umeshindwa kwenda kumtafuta huko mikoani alikokimbilia.

Binafsi baba yetu huwa anatuambia anaye kaka yake mkubwa ambae aliondoka nyumbani toka mwaka 1957 hadi sasa hajawahi kurudi ila ana watoto wapo WAKUBWA kama watano nao aliwaacha wakiwa wadogo...Kati yao watatu wapo Uingereza na wenyewe waliondoka mwaka tokea mwaka 1983 na hawajai kurudi tunasikia tu story mmoja yupo Kigoma na mmoja tunamsikiaga tu Tbc Taifa ila huyo wa kigoma ndo huwa anatutembelea.

Sababu za kuondoka nyumbani tunaambiwa ni kutafuta maisha ila tulishafanya kila njia kumtangaza kupata imeshindika tumetumia radio na magazeti hatujwahi kumpata..mtoto wake huyo anaekaa kigoma alimsikia babake kuwa yupo Singida akaanza pori kwa pori lakini wapi...Kuna mtu akamwambia yupo Ruvuma akaanza ardhi kwa ardhi lakini wapi...
Kubwa zaidi aliondoka akiwa hajawahi kupiga hata picha ,huwa tunatamani kumuona huyo dingi d lakini imeshindikana.

Hapa ina maana ba mdogo wetu huyu hajui hata sura ya ndugu zake ,hajawahi kuhudhuria msiba wa baba yake wala mama yake ...

Wengine huwa tunajisemea bado hai muda mwingine tunajisemea tu huyo alishachukuliwa na mbingu ...
Je una ndugu amewahi kuondoka nyumbani na hajawahi kurudi na kwa nini ,sababu za kuondoka nyumbani ni nini ?
Njia gani umewahi kutumia ili kufanikiwa umpate?

Je ni kweli kuwa kuna dawa za kuwarudisha watu waliopotea au kuondoka nyumbani ?

Unajisikiaje kusikia ndugu yako kukimbia nyumbani

Je kuwa mlowezi ni laana?
Je tutumie chanjo kama iliyompata Osama kwa kutafuta vinasaba?

Hata sisi kuna babu zetu wawili (kaka zake bibi mzaa mama) waliondokaga miaka ya 60 kwenda kutafuta maisha. Mmoja alirudi mwaka wa 2007 akiwa hoi bin taaban, kazeeka na kuchoka ile mbaya. Alisema alikuwa anafanya vibarua Zambia, hakuoa, wala hakuwa na mtoto. Ikabidi awe anaishi nyumbani kwa bibi na tunamtunza mpaka mauti ilipomfikia.

Kaka yake aliyeondoka naye mpaka kesho hatujamsikia na sie wengine hata sura hatumjui. Mdogo mtu aliporudi alisema waliachana huko Zambia miaka ya 70 mwenzie akisema anaenda kutafuta kazi kwenye ujenzi wa TAZARA. Baada ya kuwa hakurudi walikokuwa baada ya reli kuisha, yeye akajua kaka yake alirudi home reli ilipofika bongo. Ndo kilichomsukumaga naye kusema arudi japo alikawia kurudi mpaka uzeeni.

Akina mama walifuatiliaga enzi hizo TAZARA kujua kama alifanya vibarua huko, haikuwezekana kupata taarifa zozote.

Naimani wasiojulikana wangekuwepo enzi hizo tungewasingizia ndo wamewapoteza.
 
Nina mjomba wangu katokomea kusaka Hazina ya Mjerumani, wala hayupo mbali ila ni miaka 16 sasa hataki kurudi kwenye familia yake.
Miaka ya mwanzo alikuwa akija na kuondoka ila walipozidi kumkejeli basi akaona hawa wendawazimu, kapotea mazima.
 
Back
Top Bottom