Miaka inaenda sioni Future yangu. Nimekata tamaa!

Tatizo lako unapoteza muda mwingi kutafuta umaarufu hapa JF kwa kuandika makala zisizo na kichwa wala miguu. Jikite katika kutafuta hela, Achana kushindana na watu kama Erythrocyte au akina brazaj etc , wenzako wanalipwa na chadema!

πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€

Kasome hapa ukichoka kutafuta pesa

πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

Ukikataa tamaa kwani ndio unakuwa umefanikiwa ?

Pambana, mie sina mke, sina mtoto sina chochote na ni mkubwa kuliko wewe, ila napambana marufuku kukata tamaaa.. huwa tunakata tu kauli tu, na sio tamaa ya kufikia tunayotaka
Mi mwenyewe nasubiri nife ili nikate tamaa, ila kama sijafa NEHI
 
MIAKA IMEENDA SIONI FUTURE YANGU; NIMEKATA TAMAA!

Kwa Mkono wa Robert Heriel.

"Nina miaka 33, sina mke, sina mtoto, sina kiwanja, Kodi inanishinda, wala sio Kodi nyingi haifiki hata elfu 50 Kwa mwezi lakini inanitoa jasho kuilipa, chakula nakula Kwa mbinde Kama mvuta upinde. Mavazi yangu ni duni, sikutegemea mambo yawe hivi, tangu nikiwa Chuo nilifikiri ningefanikiwa mapema mara tuu nitakapomaliza shule. Lakini mambo yamekuwa mbali mno na matarajio yangu. Nikikuambia naendelea na mapambano ninakudanganya, nimekata matumaini.

Ona Mimi sio WA kukosa hata hela ya kununulia Dawa ya Meno, ona! Mimi sio WA kukosa sabuni ya kuogea na kufulia hata marapurapu ninayoyavaa! Ona! Mimi sio huyu! Labda Mimi wamenibadilishia. Mimi wakula mlo mmoja kweli!

Hapa sina pakwenda! Kodi nadaiwa miezi mitatu sasa. Mwenye nyumba kanipa notisi kesho kutwa nafurumushwa hapa. Loooh!!

Labda ungefikiri nilimuasi Mungu Kwa kutokwenda kwenye nyumba zake za ibada, lakini sivyo. Nilikuwa Muumini mwaminifu hapo awali kabla sijageuka muasi, uasi uliosababishwa na mambo yangu mengi kwenda mrama huku watumishi wakinitoza kila nifikapo kwenye nyumba za Ibada. Nikaasi nikasema kumbe kuabudu Napo ni mpaka ulipie. Nikaacha kwenda huu mwaka wa Saba sasa.

Nataka kuoa lakini Nani akubali Hali yangu dhalili na fukara. Wanawake wote wa mjini hutaka maisha ya magari, urembo na majumba ya kifahari. Nitawawezea wapi.

Usifikiri kuwa nilizembea kwenda huko vijijini, nilifika mpaka Makanya huko, nikateremkia Saidong mpaka Hanang huko ndani ndani, nikapandisha mpaka vijiji vya Singida mpaka nilipojikuta Kibati huko Turiani Morogoro, kote huko kutafuta mwanamke wa kijijini, lakini niliambulia patupu.

Si ungenilaumu Kama sikufika kule kwenu Handeni, nilifika kote huko mpaka Lushoto nikapandisha milima ya shambalai kote huko licha ya kuwa na wasichana wazuri lakini kote walikatalia. Ati walihitaji mwanaume kwenye wadhifa na Mali walau Mbuzi wawili tuu. Nikawaza Mimi haya kuku mmoja sina sembuse Mbuzi. Loooh! Nikamkumbuka Paka wangu mzuri wa madoa doa niliyemfuga anikamatie panya na mende waliokuwa wakinisumbua humu ndani lakini Paka Yule Kwa hila akanikimbia akaenda Kwa jirani yangu huyo hapo nje mwenye Geti la rangi ya kijivu.

Paka Yule huenda alichoka Kula Mlo mmoja, kila siku Panya tuu na hata akikosa panya angekula Mende. Nani angekubali mlo mmoja miaka nenda Kula Milo mmoja. Hata Mimi huenda nisingekubali Kama kuna nafasi ya Kula minofu.

Siku hizi Paka wangu namuona juu ya kuta za jumba la jirani yangu. Hunitazama Kwa jicho la Dharau na mara huachia mlio wa dhihaka. Basi hasira hunipandaga sana, naokotaga jiwe ili nimpige lakini Paka Yule hata hashtuki kunikimbia. Aaargrrrrrrrhii! Sitaki Kueleza haya.

Ningetaka niwe mganga wa jadi, nipige Ramli chonganishi nijipatie kipato. Wazo hilo likanipeleka mpaka Pangani huko nikajifunze elimu ya uganga na uganguzi. Niliishia kutapeliwa na hata nilipohitaji Utajiri wakaishia kuugeuza mwili wangu uwanja wa viwembe, ninachale Mimi mpaka sehemu nyeti.
Nafikiri hata siku Mungu akinijalia mara paap nikatusua maisha na kuoa, huyo mwanamke ataniona Mimi ni mlozi niliyebobea haswa. Tena angeniona Mali zangu niza ndagu.

Haya tuachane na hayo!

Embu niambie Rafiki yangu utanisaidia nini maana mambo yangu yameniendea mrama. Macho haya ni mapambo tuu hayaoni mbele.
"

Akasema akinitazama!

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Makanya, Kilimanjaro
Kumbe kuna watu hamko siriazi na maisha tafuta pesa bro mjini hapa kazi zipo nyingi za kufanya usilalamikie ugumu et kisa umesoma..What the hell have u written my fellow
 
Ambiere, uho nedho! Voneiwa!!
 
Abraar empowerment

Dunia haitupi mafanikio, dunia inatupa fursa. Vipi tutazifanya fursa kuwa mafanikio ni sisi wenyewe. Kila mmoja wetu na muono wake.

Kwa mahitaji yako ya kazi, mafunzo ya kazi yoyote kwa vitendo.

Kama umestaafu au unaweza kazi ya kufundisha fani yoyote kwa vitendo. Kama unaweza kujitolea (volunteer) ujuzi wowote au kwa kufundisha au kujifunza.

Kama umekwama unatafuta kazi yoyote ile.

Wasiliana na Abdul Ghafur, Msimamizi wa Madarasa ya Abraar (waja wema). Simu au WhatsApp +255625249605.

πŸ™πŸ™πŸ™πŸ™
 
Kumbe kuna watu hamko siriazi na maisha tafuta pesa bro mjini hapa kazi zipo nyingi za kufanya usilalamikie ugumu et kisa umesoma..What the hell have u written my fellow

Nambie wapi nizitafute,
Niajiri unipe hizo pesa sio uniambie nitafute tuu ukadhani nitakuona umenipa msaada
 
Mzee hii kitu hapo kwenu IPO?
Abraar empowerment

Dunia haitupi mafanikio, dunia inatupa fursa. Vipi tutazifanya fursa kuwa mafanikio ni sisi wenyewe. Kila mmoja wetu na muono wake.

Kwa mahitaji yako ya kazi, mafunzo ya kazi yoyote kwa vitendo.

Kama umestaafu au unaweza kazi ya kufundisha fani yoyote kwa vitendo. Kama unaweza kujitolea (volunteer) ujuzi wowote au kwa kufundisha au kujifunza.

Kama umekwama unatafuta kazi yoyote ile.

Wasiliana na Abdul Ghafur, Msimamizi wa Madarasa ya Abraar (waja wema). Simu au WhatsApp +255625249605.
rondellenmaskinnykoping-post-2021_09_21_09_06.jpg
 
Back
Top Bottom