Pesa za Mapaka ni aina flani hivi ya mapato(maendeleo) ambayo hupatikana kishirikina kwa kuumiza binadamu wengine hasa ndugu wa karibu. Kwamba mtu unaenda kalumanzila ili akutengenezee dawa ya kupata pesa; Kalumanzila anakujibu pesa ipo nje nje usjali lakini ili uipate lazima utolee sadaka na sadaka yenyewe ni kumzezetisha au kumuua mwanao au mmeo au mkeo au mzazi wako.
Ukishamwaga hiyo damu kweli mapesa kedekede yanaingia kishirikina lakin unawekewa na mashart ya kuzitumia; mfano usile wala kuvaa chochote kizuri, ulalie gunia au mkeka, usijenge nyumba nzuri wala kununua gar kila mwaka umwage damu ya nduguyo mmoja nk nk. yaan almradi tu pesa ya mapaka unakuwa nayo lakini mmiliki unateseka badala ya kuifurahia; naam, Pesa za Mapaka!
Maendeleo yaliyofanywa na jiwe miaka mitano iliyopta hayana tofauti na pesa za mapaka, ni Maendeleo ya Mapaka. unajenga daraja huku unabomoa makazi ya watu tena kiupendeleo, unanunua ndege lakini mtumishi wa serikali anapiga mihayo kwa miaka mitano hakuna nyongeza ya mahahara, unajenga barabara huku unadhulumu hela za wakulima wa korosho, unabambikia waanyabiashara kesi za kilaghai za uhujumu uchumi na kuwatisha wakupe hela kinguvu, wanafunzi huwapi kabisa au unawapa mikopo kibaguzi, hospitalini dawa hakuna, wahudumu hakuna wananchi wanatekwa hovyo, maiti zinaokotwa fukweni mwa bahari, wengine wanakung'utwa marisasi mengi tu huku wengine wakivunjwavunjwa mikono na miguu, wengine wanatupwa magerezani na mahabusu kinyume cha sheria, mahakama zinanajisiwa, bunge linatekwa na kufanywa raba stampu; uhuru wa wananchi unafutwa kila sekta, demokrasia inabakwa mchana kweupe, taasisi nyeti za serikali kama polisi, takukuru na nyinginezo zinabakwa na kunajisiwa live juu chini kushoto kulia; yaani kiujumla maendeleo ya wananchi yanapatikana kwa gharama ya mateso na hata vifo vya wananchi wenyewe; naam ni Maendeleo ya Mapaka, ni maendeleo ya manyau.
Hii ni aina ya maendeleo ambayo hayaakisi kiwango na aina ya gharama zinazoingiwa ili kuyafikia maendeleo hayo, waarabu, wajerumani na waingereza walileta maendeleo Tanganyika lakini je kiwango cha gharama ya mateso waliyopitia mababu zetu zinastahili maendeleo hayo?!!
waafrika kusini waliyakataa maendeleo ya mapaka yaliyoletwa na makaburu, Namibia waLiyakataa, Msumbiji waliyakataa, Kenya, Afrika yote na dunian kote waliyakataa maendeleo ya mapaka, hata waamerika weusi waliyakataa na bado wanayakataa katakata maendeleo ya mapaka ya marekani...
Watanzania sisi ni nani hata tuyavumilie Maendeleo ya Mapaka ya jiwe?
Watanzania tuzikatae Pesa za Mapaka, Tuyakatae Maendeleo ya Mapaka ya jiwe
Tuseme sasa baaaaas
Tuseme niYeye