Maendeleo yaliyofanywa na jiwe miaka mitano iliyopta hayana tofauti na pesa za mapaka, ni Maendeleo ya Mapaka. unajenga daraja huku unabomoa makazi ya watu tena kiupendeleo, unanunua ndege lakini mtumishi wa serikali anapiga mihayo kwa miaka mitano hakuna nyongeza ya mahahara, unajenga barabara huku unadhulumu hela za wakulima wa korosho, unabambikia waanyabiashara kesi za kilaghai za uhujumu uchumi na kuwatisha wakupe hela kinguvu, wanafunzi huwapi kabisa au unawapa mikopo kibaguzi, hospitalini dawa hakuna, wahudumu hakuna wananchi wanatekwa hovyo, maiti zinaokotwa fukweni mwa bahari, wengine wanakung'utwa marisasi mengi tu huku wengine wakivunjwavunjwa mikono na miguu, wengine wanatupwa magerezani na mahabusu kinyume cha sheria, mahakama zinanajisiwa, bunge linatekwa na kufanywa raba stampu; uhuru wa wananchi unafutwa kila sekta, demokrasia inabakwa mchana kweupe, taasisi nyeti za serikali kama polisi, takukuru na nyinginezo zinabakwa na kunajisiwa live juu chini kushoto kulia; yaani kiujumla maendeleo ya wananchi yanapatikana kwa gharama ya mateso na hata vifo vya wananchi wenyewe; naam ni Maendeleo ya Mapaka, ni maendeleo ya manyau.