Miaka Miwili ya giza, uchawa, unafiki na mateso kwa Watanzania

Miaka Miwili ya giza, uchawa, unafiki na mateso kwa Watanzania

Watu ka wewe ndiyo ile isiyotumia akili. Nani kakuambia Ben alipotezwa? Muulize Dj kengeza. Mnataka kutuaminisha ili mwisho wa siku mje mseme eti Rais Samia na yeye alikuwa Makamu wa Rais anajua na yeye hafai.
Tujiulize maswali(hii inawahusu wenye akili timamu tu)
-Kwanini polisi hawafanyi/hawakufanya upelelezi kuhusu kupotea kwa Ben Saanane? Je wanamlinda au walikuwa wakimlinda nani, Jiwe au Mbowe?
-Polisi kuficha CCTV camera footages za tukio la Lissu walikuwa wanamlinda Jiwe au Mbowe?
- Ni mamlaka ya Jiwe au ya Mbowe iliyahakikisha polisi waliokuwa wakilinda eneo la viongozi aliposhambuliwa Lissu wasiwepo lindoni(the area is guarded 24/7) na kwanini hawahojiwi wala wahusika wa kupanga ratiba za polisi wa zamu hawatoi maelezo? Anayelindwa na kadhia hiyo ni Jiwe au Mbowe?
-Kwanini mauaji yote(political related) yaliyofanywa kipindi cha utawala wa Jiwe polisi hawakutafanyia upelelezi? Ni Jiwe au ni Mbowe aliyeamuru polisi wasifanye upelelezi kuhusu hayo mauaji?
 
Ndani ya miaka hii miwili watanzania wameshuhudia na kupitia katika kipindi kigumu pengine kuwahi kutokea Tanzania. Ni kipindi ambacho huenda kinyozi wa saluni amefunga ofisi yake si chini ya mara 5 kwa wiki, Ni kipindi ambacho tumeshuhudia kuibuka watu wanaoitwa chawa! Ni kipindi ambacho kimeua , kutesa na kudhulumu maelfu ya wananchi hususan wa daraja la chini kiuchumi kwa aidha tozo, miundombinu mibovu (ajali) huduma mbovu na sera mbovu za afya, na usimamizi mbovu wa huduma zitolewazo na serikali.Ni kipindi ambacho tumeshuhudia uzembe na ufisadi kurejea kwa kasi serikalini, Ni kipindi ambacho watanzania wameshuhudia ulambaji wa asali pengine kuliko awamu yoyote ile, Ni kipindi ambacho tumeshuhudia wanafunzi wakikaa chini bila madawati huku viongozi wakila maisha kwa ziara,semina za pongezi na hafla za anasa! N.k

Kwa mambo yanayoendelea hapa nchini kwa sasa, Ni wazi kwamba wananchi hawana tena imani chini ya uongozi wa awamu hii ya sita. Kila unapoenda ni lawama na hali ya kutoridhika na utendaji wa serikali.

1: Uchumi wa Tanzania Umeporomoka. Laiti kama uongozi ungekuwa thabiti hakika uchumi ungekuwa wa kati daraja la juu tofauti na hali ilivyo sasa ambapo Tanzania imeporomoka kutoka nafasi yake ya 8 kati ya nchi 10 zenye uchumi bora Africa mpaka nje ya top 10 na kuzidiwa na vinchi kama Ghana na Angola

2: Laiti kama uongozi ungekuwa imara nidhamu na uwajibikaji kazini ungekuwepo. Leo hii tunashuhudia wananchi wakihoji kuhusu hali ya umeme nchini pasipokuwa na majibu au majibu yenye uwalakini. Lakini pamoja na hayo bado viongozi wamebaki wakiwa maofisini pasipo kuwajibika kwa namna yoyote.

3: Kwa miaka kadhaa Tanzania imekuwa ikiifanya juhudi kubwa kujikwamua kiuchumi kwa kuanzisha miradi mikubwa na ya kimkakati. Licha ya kwamba tangu awamu ya sita iingie madarakani hakuna mradi wowote wa kimkakati ulioanzishwa bali pia hata ile miradi iliyokuwa ikiendelea imekuwa ikisuasua

4: Serikali ingekuwa makini hakika Umeme usingekuwa wa mgao. Tangu Rais Samia aingie madarakani hali ya upatikanaji wa umeme nchini imekuwa mbaya sana. Hali hii imepelekea kurejea kwa mgao wa umeme ambao watanzania wengi walishausahau tangu miaka kadhaa iliyopita.Hali inayopelekea kuwatesa wananchi hususan wale wanaotegemea umeme kujipatia vipato katika shughuli zao za kila siku.

5: Hali ya upatikanaji wa maji imekuwa ya kusuasua.Kwa miezi kadhaa hususan katika jiji la Dar es salaam pamekuwa na mgao wa maji.Hali iliyopelekea kukosekana kwa maji kwa muda mrefu katika maeneo mengi.Hali ambayo hakuwahi kushuhudiwa hapo awali.

6: Tozo zisizokuwa na tija na zilizoua uchumi wa wengi.Serikali ya awamu ya sita imedhulumu na kunyang'anya kwa nguvu fedha za wananchi kwa kigezo cha tozo katika miamala ya simu.Mama mjane anapomtumia mgonjwa wake hospitali kwa ajili ya matibabu anakatwa fedha ambayo kimsingi haikuwa ya biashara. Kwa mujibu wa report kutoka Vodacom hivi karibuni miamala ya simu imepungua kwa asilimia zaidi ya 30!.Hili si jambo la kupuuza hata kidogo kwa uchumi wa nchi.Ni sawa na kutoa fedha mfuko wa kushoto na kuhamishia Kulia.

7: Kupanda kwa bei ya Mbolea.Mara tu baada ya awamu ya sita kuingia madarakani bei ya mbolea ilipanda karibu mara mbili ya bei ya awali.Hii ni imepelekea uchumi wa watanzania wengi ambao ni masikini na wanategemea kilimo kudhoofika.

8: Kupanda kwa bei ya mafuta ya kupikia
9: Kupanda kwa bei ya mafuta ya petrol
10: Kupanda kwa bei ya bidhaa za ujenzi kama cement,Nondo n.k
11: Teuzi za viongozi wasiokuwa na weledi kwa kigezo cha favour/Undugu/Kujuana (Mf. Riziwani Kikwete,Nape Nauye n.k) Tanzania ina vijana wasomi na wenye upeo mpana wa kifikra. Lakini cha kushangaza teuzi zimekuwa hazina matumaini ta kuipeleka Tanzania kule tunapotarajia.

12: Ukosefu wa uzalendo na ubadhirifu miongoni mwa watumishi wa umma.Siku si nyingi tumeshuhudia kiongozi mkuu wa serikali akiwaasa watumishi wake wale kwa urefu wa kamba zao.Hii inaashiria kwamba hata kiongozi mkuu anashiriki katika ulaji huo. Hali hii ni hatari kwa rasilimali za nchi.

13: Wananchi hususan wa hali ya chini kukosa nafasi katika nchi yao. Siku si nyingi tumeshuhudia wafanyabiashara ndogondogo maarufu kama machinga wakinyanyaswa kwa kuhamishiwa katika maeneo yasiyokuwa tija kwao. Vuta nikuvute hii imepelekea hali ya unyonge na sintofahamu miongoni mwao na kupelekea kuongezeka kwa umasikini miongoni mwa watanzania

14; Mikopo isiyokuwa na tija kwa taifa.Tangu Tanzania ipate uhuru viongozi wake wote walisisitiza kufanya mambo yetu kwa fedha zetu wenyewe bila kutegemea wahisani. Tanzania imebarikiwa rasilimali za kila aina.Mito, Maziwa, Bahari, Madini kama Tanzanite,Mbuga za wanyama, Gesi n.k Inashangaza Sana kuona kiongozi badala ya kusisitiza au kubuni namna ya kuzitumia rasilimali hizi ziweze kuwa na tija kwa watanzania,Badala yake tumekuwa tukijivunia mikopo!

15: Kuongezeka kwa gharama za uunganishaji umeme kutoka 27,000 iliyokuwepo mpaka zaidi ya 300,000 ya hivi sasa.Hali hii imepunguza mno kasi ya usambaaji wa umeme

16: Muingiliano baina ya mihimili kwa kigezo cha uchama.Inasikitisha kuona kiongozi wa mhimili mmoja anakosa uwezo wa kuikosoa na kuurekebisha mhimili mwingine kwa kuhofia kibarua chake.hili tumelishuhudia baada ya kuona spika wa bunge la JMT kujiuzulu baada ya kuhoji kuhusu mikopo na tozo.

17: Safari zisizokuwa na tija wala umuhimu kwa taifa.Tumeshuhudia safari nyingi mno za nje ya nchi,Safari hizi zimekuwa zikiigharimu nchi fedha nyingi.Safari za vikao visivyokuwa na tija kama mkutano wa kujadili athari za gesi ya ukaa sidhani kama ina tija hususan kwa nchi ambazo bado uchumi wake ni mdogo.Ni sawa na mzazi anayemiliki baiskeli kwenda kuhudhuria kikao cha adha wanayopitia wamiliki wa magari kwa tairi zao kukosa ubora.

18: Kukosekana uhuru na ukandamizaji wa demokrasia. Tunaweza kusema kwamba pia hata katika awamu zilizopita hili lilikuwepo, Lakini hili la sasa limekuja kwa namna tofauti.Wakati mwingine baba anaweza kumpa mtoto adhabu ya kulima shamba,Mtoto akalia na kulaumu sana,Lakini shamba hilohilo baadaye likaleta chakula mezani wote wakala na kufurahia. Ila tofauti iliyopo sasa,Hakuna chakula kinachokuja mezani!

19: Kushughulikia zaidi mambo yasiyokuwa na tija kwa wananchi kuliko yale yenye umuhimu na tija kwa watanzania. Imekuwa jambo la kawaida kwa awamu hii kujihusisha zaidi na makongamano,Semina elekezi,Birthday Party pamoja na hafla mbali mbali badala ya kujikita katika kufufua na kubuni miradi ya kimaendeleo itakayosaidia kuwapunguzia wananchi mzigo wa umasikini na kuinua uchumi.Hafla ya machifu na watemi si muhimu kama hafla ya utiaji saini mradi wa uchimbaji na usambazaji wa gesi ya Mtwara!

20: Kukosekana ajira. Ubunifu na uibuaji wa miradi mipya si tu umekuwa na tija kiuchumi Bali umekuwa ukiajiri vijana wengi.Kukosekana kwa ubunifu na sera mbovu za serikali zimesababisha kukoseka kwa ajira miongoni mwa vijana wengi

21: Kuongezeka matukio ya uhalifu.
Mara tu baada ya awamu ya sita kushika hatamu sote tumeshuhudia jinsi wimbi la uhalifu lilivyoongezeka.Sio tu matukio ya wizi na ujambazi bali mpaka uchomaji wa masoko kama Kariakoo, mchikichini n.k wizi mauaji na utekaji nyara vimeongezeka kwa kasi mno. Hii inaonyesha udhaifu katika usimamizi wa majeshi yetu ya ulinzi na usalama

22: Kuongezeka gharama za simu
Kutokana na kodi za miamala Kuongezeka kampuni za simu zimejikuta zikilazimika kupandisha gharama za muda wa maongezi na huduma zinginezo za simu kama vile huduma za vifurushi ili kuweza kubalance gharama za uendeshaji. Hali hii imesababisha mzigo mzito kwa wananchi hasa ukizingatia mawasiliano ni nyenzo muhimu sana katika shughuli zao za kila siku

23: Kutoa vipaumbele kwa mambo ya hovyo na yasiyo na tija kwa taifa hususan kwa wakati huu.Hapakuwa na ulazima kutumia gharama kubwa na uwekezaji katika kutumia kodi za wananchi kiongozi mkuu wa serikali kusafiri na kutumia muda mwingi kutengeneza filamu wakati fedha hiyo haina uhakika wa kurudi.Mfano fedha hiyo ingewekezwa kwenye timu maarufu zinazoshiriki ligi za ulaya ingekuwa na tija na matokeo zaidi na Rais angepata muda kutekeleza majukumu mengine ya kiserikali kuliko kupoteza muda mwingi kusafiri.

Hakika ni mambo mengi ambayo yamekuwa yakifanyika kinyume na matarajio ya watanzania wengi ambao waliwaamini viongozi wao na kuwaweka madarakani huku wakiwa na matumaini makubwa ya kuondokewa na maradhi, ujinga na umasikini ambao ndio maadui wakuu wa taifa kama ilivyobainishwa na Mwl Nyerere badala yake watanzania hao ambao wengi ni masikini na wameteseka kwa umasikini kiasi cha kusahau tarehe zao za kuzaliwa huku wakishuhudia wale waliowachagua wakikata keki ikulu!
Chama chochote cha siasa hasa viongozi wao kama wapo humu...Aisee hizi ndo hoja za kuchukua,waachane na mambo ya kazi ya Boda ni laaana,Vicoba si kitu.....Mzee hongera sana .
 
Ninakiwanda changu hapa cha kufyatua tofari!

Karibu kila siku napata hasara ya mfuko mmoja wa cement mpaka miwili kwa siku

Umeme unakuacha tayari mashine inatafuna mchanga wa kufyatulia, umeme huooo!!

Ukirudi inabidi uweke mfuko mwingine tena kwenye huo udongo, baada ya masaa mawili matatu umeme huooo! Hasara tena!

Hivi kweli, nitawapendaje sasa hawa viongozi wanaonitafutia umasikini wa lazima?

At least hujapata hasara ya kukatwa mguu au kupotezwa au jamaa yako kupotezwa na kulea mayatima na wajane kuwasaidia
 
Bora huyu kuliko huko tulipotoka ilikua jahanamu ile (escape from sobibor)

IMG_9244.jpg

[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]
 
Watu ka wewe ndiyo ile isiyotumia akili. Nani kakuambia Ben alipotezwa? Muulize Dj kengeza. Mnataka kutuaminisha ili mwisho wa siku mje mseme eti Rais Samia na yeye alikuwa Makamu wa Rais anajua na yeye hafai.

KENGE nyingine hii ndugu wanaBodi.
 
Wewe ni mpumbavu!

Kabla ya hao kina ben una habari kama kuna watu waliuawa kwa kurushiwa bomu kwenye mkutano wa chadema pale soweto arusha?

Mwangosi yuko wapi?
Ulimboka yuko wapi?
Inasikitisha sana kuona watu wanajadili petty issues huku wakisahau watoto wao wanakaa chini, wanasahau migao ya umeme, maji gharama za maisha kupanda, tozo n.k.Hii ndiyo Tz
 
Nilikuwa naangalia mechi ya Madrild ilikuwa usiku kama saa tano na dakika hivi,jamaa akabadlisha chanel akaweka Itv,Nikamuona mama anatangaza kifo cha JPm,nililia Sana alafu nikajikaza nikachukua Boda mpaka home.
Nikakimbilia kwenye Begi langu kuitafta Rasimu ya katiba inasemaje pale kiongozi/Rais anapfariki kabla ya kumaliza kuhudumu Muda wake,Nikaona wameandika anayechukua nafasi yake ni Makamu wake wa Rais,Machozi yakaanza kunitoka tena,wakati huo sio namlilia JPM nikawa naililia Tanzania,Namuuliza Allah kwanini umemchukua huyu ukamuacha huyu?.
Nilishaona kwamba kwa uongozi wa anayekuja Nchi itapotea,kutaibuka visasi,Uzalimu,Rushwa na mengine ya Hovyo.Na kweli yaani Mama Tangu aingie madarakani mwaka wa pili sasa mvua zimenyesha mara 2tu njaaa imetamalaki kila kitu ni hovyoo.
Mungu amrehemu na amlaze mahali pema peponi.
 
Back
Top Bottom