Miaka Miwili ya giza, uchawa, unafiki na mateso kwa Watanzania

Mkuu kabla ya kuhitimisha hoja yako juu ya tathimini yako ulioifanya kwa miaka miwili juu ya mwenendo wa kiuchumi wa taifa letu, ebu tupe kwanza picha ya jumla kwa kulinganisha na nchi jirani. Nini tathimini yako juu mwenendo wa kiuchumi wa nchi na wananchi waliopo katika eneo la Maziwa Makuu, EAC pengine hata SADC.

Nafikiri unatambua nini ambacho kinaendelea nchini Kenya, hivi sasa, ambapo kwa kuwa katiba yao ipo rafiki na kuruhusu wananchi kupaza sauti zao bila ya kunyamazishwa na vyombo vyao vya dola.

Hali hii wala haipo kwao tu, ni mwenendo wa kiuchumi kwa dunia nzima hivi sasa. Hata kama haupendi kusikia ukweli, lakini ni bayana kabisa vita kati ya Urusi na Ukraine imetikisa uchumi wa dunia, na "multiplier effect" inazikumba nchi nyingi, na "major intensity" ipo katika nchi za Afrika.
Kwani ata kabla ya ayo ni lini Mtanzania aliishi maisha mazuri.Kinachozungumzwa hapa ni Ile nia ya serikali kuwaondoa Wananchi wake kutoka kwenye umasikini wa kutupwa.Magufuli alikuwa na mwelekeo mzuri ila uyu Mama anaturudisha nyuma,yaani ukiangalia madudu ya utawala wa JK na utawala wa Mama huoni tofauti.
Uwizi serikalini umerejea kwa kasi,nidhamu ya watumishi imekuwa ovyo,Umeme unakatika ovyoovyo nk.
 
Mbinafsi
Mchoyo
Mkanda
Mkabila

Mwl. Jkn alikimea vikali sana watu wakabila, na wabinafsi.
Kwani Bibi siyo Mkanda;Mkoa wa Pwani peke yake una Mawaziri 5 Tanga 3 na Zanzibar 5.Kwenye Mikoa ya kimkakati kama Mbeya kawapa Unaibu Waziri.Tabora ndiyo kabisa hamna ata Waziri mmoja.
(Naibu Waziri aingii kwenye vikao vya Baraza la Mawaziri)
 
Uzuri wa Uislam tuna nafunzo mema ya Kiislam kwenye kila hali:

Tunazuwia kwa kutumia mikono inapowezekana, isipowezekana tunatumia mdomo (kwa kuzuwia ki hekima) , isipowezekana, tunachukia ndani ya mioyo yetu.

Ukimya wakati mwengine ni hekima kubwa sana.
Basi kama ni hivyo Zanzibar ingekuwa inatisha kimaendeleo Afrika Mashariki!
 
Mm mwenyww namshanga anavyo fananisha angola na tanzaniaa

Hv anaijuwa angola kweli ,angola ni nchi ya tatu afrca kwa uchumi imara

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Mjomba hapo umetupiga kamba!
Angola ni ya ngapi?[emoji1787][emoji1787]
Na Egypt,Tunisia, Morocco na Algeria zipo namba ngapi!!
 
Acha mihemko mara nyingi mihemko huashiria uchache wa akili.

Hutununui ndege eti kwa sababu tuwe na national carrier. Kuna nchi nyingi tu tajiri duniani hazina mashirika ya ndege.

Umechunguza biashara ya ndege ukajua ikoje. Unajua Kenya airways hawapata faida tangu mwaka gani? Unajua kuwa South African Airways haijapata faida toka 2009 na shirika linaendeshwa kwa bail. Hili ni shirika lenye wabia wakubwa na wengi zaidi ni wazungu wa Uholanzi.

Unajua pia kwamba mashirika mengi makubwa ya ndege duniani kama KLM, British Airways, Air India na hata American Airlines yanachechemea kutokana na biashara ya ndege kuwa ngumu kwa sababu ya market competition?

Wewe unafikiri ndege ni kuwa nazo kama midoli kwasababu mwenzako anazo?

Tangu tununue ndege miaka kadhaa iliyopita umewahi kusikia tomepost faida yoyote ikatangazwa?

Miradi mingi ni hovyo kwa wanaojua ukweli ila kwa wajinga ni sawa kwakuwa wajinga huangalia mambo kwa nje tu.
Kwaiyo tusaidie wewe Mwerevu,sasa hayo Mashirika uliyoyataja yameisha toweka au bado yapo?na kama yapo unadhani kwanini serikali za nchi husika haziachi yakafa jumla pamoja na kuingiza hasara?
Ndege ni kichocheo cha Uchumi kwa maana ya kurahisisha usafiri wa abiria na Mizigo,ata kama inaingiza hasara lakini inasaidia sector zingine za Utalii,Kilimo,Madini nk.Ujasikia serikali ya Saudi Arabia wanataka kuanzisha Shirika lingine la Ndege nje ya Emirates?
 
Ukiona nchi kubwa matajiri wanahangaika na biashara ya ndege kwa hasara ujue nchi maskini zitateseka sana. Unajua mtaji wa kwanza wa shirika la ndege ni wasafiri wa nchini wanaokwenda nchi za nje, halafu ndio inafuata wasafiri kutoka nje wanaokuja nchini. Sasa sisi hatuna watanzania wengi wanaosafiri kwenda nje, kwa hiyo hatuna mtaji msingi na hii inafanya biashara yetu ya ndege kuwa ngumu zaidi ya wakenya, south africa na wengine. Je tuna uwezo wa kuendelea kulibeba shirika letu la ndege kwa ruzuku kwa miaka mingi isiyo na faida? Kenya na Afrika Kusini wamechoka ndio maana rais Ruto wa Kenya alipokwenda Marekani alitangazia wamarekani waje wawekeze Kenya Airways kwa masharti nafuu. Time will tell utajua namaanisha nini.
 
World economics shakes up! (very common issue)

Were the causes, but we enjoy in freedom we have, hatuishi kama panya buku!

Awali watu wakuwa wanapotea ovyo kama Ben saanane, iliogofya sana.
Wewe ni mpumbavu!

Kabla ya hao kina ben una habari kama kuna watu waliuawa kwa kurushiwa bomu kwenye mkutano wa chadema pale soweto arusha?

Mwangosi yuko wapi?
Ulimboka yuko wapi?
 
Kwaiyo tusaidie wewe Mwerevu,sasa hayo Mashirika uliyoyataja yameisha toweka au bado yapo?na kama yapo unadhani kwanini serikali za nchi husika haziachi yakafa jumla pamoja na kuingiza hasara?
Ndege ni kichocheo cha Uchumi kwa maana ya kurahisisha usafiri wa abiria na Mizigo,ata kama inaingiza hasara lakini inasaidia sector zingine za Utalii,Kilimo,Madini nk.Ujasikia serikali ya Saudi Arabia wanataka kuanzisha Shirika lingine la Ndege nje ya Emirates?
Wewe bawe haujui Saudi Arabia nini na emirates nini. Para darsa dogo...

Saudi Arabia wanamiliki shirika la ndege liitwalo Saudi Arabian Airlines, wanaanzisha shirika jipya liitwalo Riadh Air.

United Arab Emirates ndio wana shirika liitwalo Emirates.

Saudi Arabia na United Arab Emirates ni nchi mbili tofauti kabisa.
 
Umeme ulikatika wapi,tupe mifano ya maeneo umeme ulikuwa unakatika ovyo awamu ya tan😵nline media kama JF zilikuwa active,tuoneshe ata Uzi wa kuilalamikia kukatika umeme awamu ya tano.
Swali lako gumu, inamaana umeme haukukatika awamu ya tano?
 
Mengi umeandika Uongo kwanini ? Samia si malaika Ila Mama anajitahidi kwa nafasi yake
 
Freedom in poverty? Hata sasa watu wanapotea zaidi kwa vifo vinavyotokana na umeme kukatika ghafla huko mahospitalini, wengine wanapotea kwa njaa, wengine kwa hali ngumu ya maisha n.k wewe kama unaishi vyema usizungumzie wengine!

Watu wanateseka na migao ya umeme, bei ya vitu kupanda, watu wanashindia mlo mmoja wewe unaongelea huo upuuzi gani? Au hawa wengine sio watu?
Kabisa yani watu wamefumbwa macho ni vipofu zaidi ya Bartimayo
 
Mtanikumbuka kwa mazuri, RIP baba.
Hata familia za Ben Saanane na Azory Gwanda zinamkumbuka, nao pia ni Watanzania.
Screenshot_20230316-012242.jpg
 
Ndani ya miaka hii miwili watanzania wameshuhudia na kupitia katika kipindi kigumu pengine kuwahi kutokea Tanzania. Ni kipindi ambacho huenda kinyozi wa saluni amefunga ofisi yake si chini ya mara 5 kwa wiki, Ni kipindi ambacho tumeshuhudia kuibuka watu wanaoitwa chawa! Ni kipindi ambacho kimeua , kutesa na kudhulumu maelfu ya wananchi hususan wa daraja la chini kiuchumi kwa aidha tozo, miundombinu mibovu (ajali) huduma mbovu na sera mbovu za afya, na usimamizi mbovu wa huduma zitolewazo na serikali.Ni kipindi ambacho tumeshuhudia uzembe na ufisadi kurejea kwa kasi serikalini, Ni kipindi ambacho watanzania wameshuhudia ulambaji wa asali pengine kuliko awamu yoyote ile, Ni kipindi ambacho tumeshuhudia wanafunzi wakikaa chini bila madawati huku viongozi wakila maisha kwa ziara,semina za pongezi na hafla za anasa! N.k

Kwa mambo yanayoendelea hapa nchini kwa sasa, Ni wazi kwamba wananchi hawana tena imani chini ya uongozi wa awamu hii ya sita. Kila unapoenda ni lawama na hali ya kutoridhika na utendaji wa serikali.

1: Uchumi wa Tanzania Umeporomoka. Laiti kama uongozi ungekuwa thabiti hakika uchumi ungekuwa wa kati daraja la juu tofauti na hali ilivyo sasa ambapo Tanzania imeporomoka kutoka nafasi yake ya 8 kati ya nchi 10 zenye uchumi bora Africa mpaka nje ya top 10 na kuzidiwa na vinchi kama Ghana na Angola

2: Laiti kama uongozi ungekuwa imara nidhamu na uwajibikaji kazini ungekuwepo. Leo hii tunashuhudia wananchi wakihoji kuhusu hali ya umeme nchini pasipokuwa na majibu au majibu yenye uwalakini. Lakini pamoja na hayo bado viongozi wamebaki wakiwa maofisini pasipo kuwajibika kwa namna yoyote.

3: Kwa miaka kadhaa Tanzania imekuwa ikiifanya juhudi kubwa kujikwamua kiuchumi kwa kuanzisha miradi mikubwa na ya kimkakati. Licha ya kwamba tangu awamu ya sita iingie madarakani hakuna mradi wowote wa kimkakati ulioanzishwa bali pia hata ile miradi iliyokuwa ikiendelea imekuwa ikisuasua

4: Serikali ingekuwa makini hakika Umeme usingekuwa wa mgao. Tangu Rais Samia aingie madarakani hali ya upatikanaji wa umeme nchini imekuwa mbaya sana. Hali hii imepelekea kurejea kwa mgao wa umeme ambao watanzania wengi walishausahau tangu miaka kadhaa iliyopita.Hali inayopelekea kuwatesa wananchi hususan wale wanaotegemea umeme kujipatia vipato katika shughuli zao za kila siku.

5: Hali ya upatikanaji wa maji imekuwa ya kusuasua.Kwa miezi kadhaa hususan katika jiji la Dar es salaam pamekuwa na mgao wa maji.Hali iliyopelekea kukosekana kwa maji kwa muda mrefu katika maeneo mengi.Hali ambayo hakuwahi kushuhudiwa hapo awali.

6: Tozo zisizokuwa na tija na zilizoua uchumi wa wengi.Serikali ya awamu ya sita imedhulumu na kunyang'anya kwa nguvu fedha za wananchi kwa kigezo cha tozo katika miamala ya simu.Mama mjane anapomtumia mgonjwa wake hospitali kwa ajili ya matibabu anakatwa fedha ambayo kimsingi haikuwa ya biashara. Kwa mujibu wa report kutoka Vodacom hivi karibuni miamala ya simu imepungua kwa asilimia zaidi ya 30!.Hili si jambo la kupuuza hata kidogo kwa uchumi wa nchi.Ni sawa na kutoa fedha mfuko wa kushoto na kuhamishia Kulia.

7: Kupanda kwa bei ya Mbolea.Mara tu baada ya awamu ya sita kuingia madarakani bei ya mbolea ilipanda karibu mara mbili ya bei ya awali.Hii ni imepelekea uchumi wa watanzania wengi ambao ni masikini na wanategemea kilimo kudhoofika.

8: Kupanda kwa bei ya mafuta ya kupikia
9: Kupanda kwa bei ya mafuta ya petrol
10: Kupanda kwa bei ya bidhaa za ujenzi kama cement,Nondo n.k
11: Teuzi za viongozi wasiokuwa na weledi kwa kigezo cha favour/Undugu/Kujuana (Mf. Riziwani Kikwete,Nape Nauye n.k) Tanzania ina vijana wasomi na wenye upeo mpana wa kifikra. Lakini cha kushangaza teuzi zimekuwa hazina matumaini ta kuipeleka Tanzania kule tunapotarajia.

12: Ukosefu wa uzalendo na ubadhirifu miongoni mwa watumishi wa umma.Siku si nyingi tumeshuhudia kiongozi mkuu wa serikali akiwaasa watumishi wake wale kwa urefu wa kamba zao.Hii inaashiria kwamba hata kiongozi mkuu anashiriki katika ulaji huo. Hali hii ni hatari kwa rasilimali za nchi.

13: Wananchi hususan wa hali ya chini kukosa nafasi katika nchi yao. Siku si nyingi tumeshuhudia wafanyabiashara ndogondogo maarufu kama machinga wakinyanyaswa kwa kuhamishiwa katika maeneo yasiyokuwa tija kwao. Vuta nikuvute hii imepelekea hali ya unyonge na sintofahamu miongoni mwao na kupelekea kuongezeka kwa umasikini miongoni mwa watanzania

14; Mikopo isiyokuwa na tija kwa taifa.Tangu Tanzania ipate uhuru viongozi wake wote walisisitiza kufanya mambo yetu kwa fedha zetu wenyewe bila kutegemea wahisani. Tanzania imebarikiwa rasilimali za kila aina.Mito, Maziwa, Bahari, Madini kama Tanzanite,Mbuga za wanyama, Gesi n.k Inashangaza Sana kuona kiongozi badala ya kusisitiza au kubuni namna ya kuzitumia rasilimali hizi ziweze kuwa na tija kwa watanzania,Badala yake tumekuwa tukijivunia mikopo!

15: Kuongezeka kwa gharama za uunganishaji umeme kutoka 27,000 iliyokuwepo mpaka zaidi ya 300,000 ya hivi sasa.Hali hii imepunguza mno kasi ya usambaaji wa umeme

16: Muingiliano baina ya mihimili kwa kigezo cha uchama.Inasikitisha kuona kiongozi wa mhimili mmoja anakosa uwezo wa kuikosoa na kuurekebisha mhimili mwingine kwa kuhofia kibarua chake.hili tumelishuhudia baada ya kuona spika wa bunge la JMT kujiuzulu baada ya kuhoji kuhusu mikopo na tozo.

17: Safari zisizokuwa na tija wala umuhimu kwa taifa.Tumeshuhudia safari nyingi mno za nje ya nchi,Safari hizi zimekuwa zikiigharimu nchi fedha nyingi.Safari za vikao visivyokuwa na tija kama mkutano wa kujadili athari za gesi ya ukaa sidhani kama ina tija hususan kwa nchi ambazo bado uchumi wake ni mdogo.Ni sawa na mzazi anayemiliki baiskeli kwenda kuhudhuria kikao cha adha wanayopitia wamiliki wa magari kwa tairi zao kukosa ubora.

18: Kukosekana uhuru na ukandamizaji wa demokrasia. Tunaweza kusema kwamba pia hata katika awamu zilizopita hili lilikuwepo, Lakini hili la sasa limekuja kwa namna tofauti.Wakati mwingine baba anaweza kumpa mtoto adhabu ya kulima shamba,Mtoto akalia na kulaumu sana,Lakini shamba hilohilo baadaye likaleta chakula mezani wote wakala na kufurahia. Ila tofauti iliyopo sasa,Hakuna chakula kinachokuja mezani!

19: Kushughulikia zaidi mambo yasiyokuwa na tija kwa wananchi kuliko yale yenye umuhimu na tija kwa watanzania. Imekuwa jambo la kawaida kwa awamu hii kujihusisha zaidi na makongamano,Semina elekezi,Birthday Party pamoja na hafla mbali mbali badala ya kujikita katika kufufua na kubuni miradi ya kimaendeleo itakayosaidia kuwapunguzia wananchi mzigo wa umasikini na kuinua uchumi.Hafla ya machifu na watemi si muhimu kama hafla ya utiaji saini mradi wa uchimbaji na usambazaji wa gesi ya Mtwara!

20: Kukosekana ajira. Ubunifu na uibuaji wa miradi mipya si tu umekuwa na tija kiuchumi Bali umekuwa ukiajiri vijana wengi.Kukosekana kwa ubunifu na sera mbovu za serikali zimesababisha kukoseka kwa ajira miongoni mwa vijana wengi

21: Kuongezeka matukio ya uhalifu.
Mara tu baada ya awamu ya sita kushika hatamu sote tumeshuhudia jinsi wimbi la uhalifu lilivyoongezeka.Sio tu matukio ya wizi na ujambazi bali mpaka uchomaji wa masoko kama Kariakoo, mchikichini n.k wizi mauaji na utekaji nyara vimeongezeka kwa kasi mno. Hii inaonyesha udhaifu katika usimamizi wa majeshi yetu ya ulinzi na usalama

22: Kuongezeka gharama za simu
Kutokana na kodi za miamala Kuongezeka kampuni za simu zimejikuta zikilazimika kupandisha gharama za muda wa maongezi na huduma zinginezo za simu kama vile huduma za vifurushi ili kuweza kubalance gharama za uendeshaji. Hali hii imesababisha mzigo mzito kwa wananchi hasa ukizingatia mawasiliano ni nyenzo muhimu sana katika shughuli zao za kila siku

23: Kutoa vipaumbele kwa mambo ya hovyo na yasiyo na tija kwa taifa hususan kwa wakati huu.Hapakuwa na ulazima kutumia gharama kubwa na uwekezaji katika kutumia kodi za wananchi kiongozi mkuu wa serikali kusafiri na kutumia muda mwingi kutengeneza filamu wakati fedha hiyo haina uhakika wa kurudi.Mfano fedha hiyo ingewekezwa kwenye timu maarufu zinazoshiriki ligi za ulaya ingekuwa na tija na matokeo zaidi na Rais angepata muda kutekeleza majukumu mengine ya kiserikali kuliko kupoteza muda mwingi kusafiri.

Hakika ni mambo mengi ambayo yamekuwa yakifanyika kinyume na matarajio ya watanzania wengi ambao waliwaamini viongozi wao na kuwaweka madarakani huku wakiwa na matumaini makubwa ya kuondokewa na maradhi, ujinga na umasikini ambao ndio maadui wakuu wa taifa kama ilivyobainishwa na Mwl Nyerere badala yake watanzania hao ambao wengi ni masikini na wameteseka kwa umasikini kiasi cha kusahau tarehe zao za kuzaliwa huku wakishuhudia wale waliowachagua wakikata keki ikulu!
Huyu mama yupo Kwa ajili ya matajiri na wazanzibar ila sisi kachoka nani ni mbwa tu kwake ndio maana hausikii akizungumzia matatizo yetu
 
Unatuchosha utatulipa tukimaliza kusoma?

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Nilikuwa naangalia mechi ya Madrild ilikuwa usiku kama saa tano na dakika hivi,jamaa akabadlisha chanel akaweka Itv,Nikamuona mama anatangaza kifo cha JPm,nililia Sana alafu nikajikaza nikachukua Boda mpaka home.
Nikakimbilia kwenye Begi langu kuitafta Rasimu ya katiba inasemaje pale kiongozi/Rais anapfariki kabla ya kumaliza kuhudumu Muda wake,Nikaona wameandika anayechukua nafasi yake ni Makamu wake wa Rais,Machozi yakaanza kunitoka tena,wakati huo sio namlilia JPM nikawa naililia Tanzania,Namuuliza Allah kwanini umemchukua huyu ukamuacha huyu?.
Nilishaona kwamba kwa uongozi wa anayekuja Nchi itapotea,kutaibuka visasi,Uzalimu,Rushwa na mengine ya Hovyo.Na kweli yaani Mama Tangu aingie madarakani mwaka wa pili sasa mvua zimenyesha mara 2tu njaaa imetamalaki kila kitu ni hovyoo.
 
Back
Top Bottom