FaizaFoxy
Platinum Member
- Apr 13, 2011
- 100,246
- 123,145
Huo ni muoni wako, upo huru na fikra zako.Watangulizi wa 001, 003,004, 005 walijaribu kupambana na RUSHWA na MAFISADI.
Awamu hii, ameamua "KUWAPOTEZEA".
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Huo ni muoni wako, upo huru na fikra zako.Watangulizi wa 001, 003,004, 005 walijaribu kupambana na RUSHWA na MAFISADI.
Awamu hii, ameamua "KUWAPOTEZEA".
Wanaopotea kwa sasa na kuuwawa sio bora kama beni saanane sio mbona hao hamlalamiki?World economics shakes up! (very common issue)
Were the causes, but we enjoy in freedom we have, hatuishi kama panya buku!
Awali watu wakuwa wanapotea ovyo kama Ben saanane, iliogofya sana.
unnamzungumzia ben sanane aliepotezwa na Chadema wenyewe 😕World economics shakes up! (very common issue)
Were the causes, but we enjoy in freedom we have, hatuishi kama panya buku!
Awali watu wakuwa wanapotea ovyo kama Ben saanane, iliogofya sana.
halafu wenye vyombo vya dola wakazidiwa akili na CHADEMA ........ama kweli nchi ina watu watepevu sana wa akili, ufahamu na kuona mbele ,unnamzungumzia ben sanane aliepotezwa na Chadema wenyewe 😕
ulitegemea vyombo vya dola inayoongozwa na CCM ihangaike na mambo yanayofanywa na chama cha upinzani ili iweje sasa.halafu wenye vyombo vya dola wakazidiwa akili na CHADEMA ........ama kweli nchi ina watu watepevu sana wa akili, ufahamu na kuona mbele ,
ndio maana majority tunaamini ccm imechoka kabisaa yaani,ulitegemea vyombo vya dola inayoongozwa na CCM ihangaike na mambo yanayofanywa na chama cha upinzani ili iweje sasa.
asante kwa kutambua hilo na ndio ukweli ulivyondio maana majority tunaamini ccm imechoka kabisaa yaani,
ccm inaamini vyama vya upinzani ni uadui , uhasama , uhaini n.k
na ndio maana hata mama Samia akizungumzia kuhusu maridhiano wengi ndani ya ccm wanamuona anapotoka kwasanbabu akili zao zinashabihiana na hayo.
ili tuendelee lazima kuwe na Katiba mpya ambapo kutakua na mpaka kati ya watendaji zao la siasa na watendaji ambao ni zao la mfumo wa Kiserikali.
Mkuu umesahau miamala ya Benki,uko watu hawasemi tunapigwa nje ndani,matozo kibao.Ndani ya miaka hii miwili watanzania wameshuhudia na kupitia katika kipindi kigumu pengine kuwahi kutokea Tanzania. Ni kipindi ambacho huenda kinyozi wa saluni amefunga ofisi yake si chini ya mara 5 kwa wiki, Ni kipindi ambacho tumeshuhudia kuibuka watu wanaoitwa chawa! Ni kipindi ambacho kimeua , kutesa na kudhulumu maelfu ya wananchi hususan wa daraja la chini kiuchumi kwa aidha tozo, miundombinu mibovu (ajali) huduma mbovu na sera mbovu za afya, na usimamizi mbovu wa huduma zitolewazo na serikali.Ni kipindi ambacho tumeshuhudia uzembe na ufisadi kurejea kwa kasi serikalini, Ni kipindi ambacho watanzania wameshuhudia ulambaji wa asali pengine kuliko awamu yoyote ile, Ni kipindi ambacho tumeshuhudia wanafunzi wakikaa chini bila madawati huku viongozi wakila maisha kwa ziara,semina za pongezi na hafla za anasa! N.k
Kwa mambo yanayoendelea hapa nchini kwa sasa, Ni wazi kwamba wananchi hawana tena imani chini ya uongozi wa awamu hii ya sita. Kila unapoenda ni lawama na hali ya kutoridhika na utendaji wa serikali.
1: Uchumi wa Tanzania Umeporomoka. Laiti kama uongozi ungekuwa thabiti hakika uchumi ungekuwa wa kati daraja la juu tofauti na hali ilivyo sasa ambapo Tanzania imeporomoka kutoka nafasi yake ya 8 kati ya nchi 10 zenye uchumi bora Africa mpaka nje ya top 10 na kuzidiwa na vinchi kama Ghana na Angola
2: Laiti kama uongozi ungekuwa imara nidhamu na uwajibikaji kazini ungekuwepo. Leo hii tunashuhudia wananchi wakihoji kuhusu hali ya umeme nchini pasipokuwa na majibu au majibu yenye uwalakini. Lakini pamoja na hayo bado viongozi wamebaki wakiwa maofisini pasipo kuwajibika kwa namna yoyote.
3: Kwa miaka kadhaa Tanzania imekuwa ikiifanya juhudi kubwa kujikwamua kiuchumi kwa kuanzisha miradi mikubwa na ya kimkakati. Licha ya kwamba tangu awamu ya sita iingie madarakani hakuna mradi wowote wa kimkakati ulioanzishwa bali pia hata ile miradi iliyokuwa ikiendelea imekuwa ikisuasua
4: Serikali ingekuwa makini hakika Umeme usingekuwa wa mgao. Tangu Rais Samia aingie madarakani hali ya upatikanaji wa umeme nchini imekuwa mbaya sana. Hali hii imepelekea kurejea kwa mgao wa umeme ambao watanzania wengi walishausahau tangu miaka kadhaa iliyopita.Hali inayopelekea kuwatesa wananchi hususan wale wanaotegemea umeme kujipatia vipato katika shughuli zao za kila siku.
5: Hali ya upatikanaji wa maji imekuwa ya kusuasua.Kwa miezi kadhaa hususan katika jiji la Dar es salaam pamekuwa na mgao wa maji.Hali iliyopelekea kukosekana kwa maji kwa muda mrefu katika maeneo mengi.Hali ambayo hakuwahi kushuhudiwa hapo awali.
6: Tozo zisizokuwa na tija na zilizoua uchumi wa wengi.Serikali ya awamu ya sita imedhulumu na kunyang'anya kwa nguvu fedha za wananchi kwa kigezo cha tozo katika miamala ya simu.Mama mjane anapomtumia mgonjwa wake hospitali kwa ajili ya matibabu anakatwa fedha ambayo kimsingi haikuwa ya biashara. Kwa mujibu wa report kutoka Vodacom hivi karibuni miamala ya simu imepungua kwa asilimia zaidi ya 30!.Hili si jambo la kupuuza hata kidogo kwa uchumi wa nchi.Ni sawa na kutoa fedha mfuko wa kushoto na kuhamishia Kulia.
7: Kupanda kwa bei ya Mbolea.Mara tu baada ya awamu ya sita kuingia madarakani bei ya mbolea ilipanda karibu mara mbili ya bei ya awali.Hii ni imepelekea uchumi wa watanzania wengi ambao ni masikini na wanategemea kilimo kudhoofika.
8: Kupanda kwa bei ya mafuta ya kupikia
9: Kupanda kwa bei ya mafuta ya petrol
10: Kupanda kwa bei ya bidhaa za ujenzi kama cement,Nondo n.k
11: Teuzi za viongozi wasiokuwa na weledi kwa kigezo cha favour/Undugu/Kujuana (Mf. Riziwani Kikwete,Nape Nauye n.k) Tanzania ina vijana wasomi na wenye upeo mpana wa kifikra. Lakini cha kushangaza teuzi zimekuwa hazina matumaini ta kuipeleka Tanzania kule tunapotarajia.
12: Ukosefu wa uzalendo na ubadhirifu miongoni mwa watumishi wa umma.Siku si nyingi tumeshuhudia kiongozi mkuu wa serikali akiwaasa watumishi wake wale kwa urefu wa kamba zao.Hii inaashiria kwamba hata kiongozi mkuu anashiriki katika ulaji huo. Hali hii ni hatari kwa rasilimali za nchi.
13: Wananchi hususan wa hali ya chini kukosa nafasi katika nchi yao. Siku si nyingi tumeshuhudia wafanyabiashara ndogondogo maarufu kama machinga wakinyanyaswa kwa kuhamishiwa katika maeneo yasiyokuwa tija kwao. Vuta nikuvute hii imepelekea hali ya unyonge na sintofahamu miongoni mwao na kupelekea kuongezeka kwa umasikini miongoni mwa watanzania
14; Mikopo isiyokuwa na tija kwa taifa.Tangu Tanzania ipate uhuru viongozi wake wote walisisitiza kufanya mambo yetu kwa fedha zetu wenyewe bila kutegemea wahisani. Tanzania imebarikiwa rasilimali za kila aina.Mito, Maziwa, Bahari, Madini kama Tanzanite,Mbuga za wanyama, Gesi n.k Inashangaza Sana kuona kiongozi badala ya kusisitiza au kubuni namna ya kuzitumia rasilimali hizi ziweze kuwa na tija kwa watanzania,Badala yake tumekuwa tukijivunia mikopo!
15: Kuongezeka kwa gharama za uunganishaji umeme kutoka 27,000 iliyokuwepo mpaka zaidi ya 300,000 ya hivi sasa.Hali hii imepunguza mno kasi ya usambaaji wa umeme
16: Muingiliano baina ya mihimili kwa kigezo cha uchama.Inasikitisha kuona kiongozi wa mhimili mmoja anakosa uwezo wa kuikosoa na kuurekebisha mhimili mwingine kwa kuhofia kibarua chake.hili tumelishuhudia baada ya kuona spika wa bunge la JMT kujiuzulu baada ya kuhoji kuhusu mikopo na tozo.
17: Safari zisizokuwa na tija wala umuhimu kwa taifa.Tumeshuhudia safari nyingi mno za nje ya nchi,Safari hizi zimekuwa zikiigharimu nchi fedha nyingi.Safari za vikao visivyokuwa na tija kama mkutano wa kujadili athari za gesi ya ukaa sidhani kama ina tija hususan kwa nchi ambazo bado uchumi wake ni mdogo.Ni sawa na mzazi anayemiliki baiskeli kwenda kuhudhuria kikao cha adha wanayopitia wamiliki wa magari kwa tairi zao kukosa ubora.
18: Kukosekana uhuru na ukandamizaji wa demokrasia. Tunaweza kusema kwamba pia hata katika awamu zilizopita hili lilikuwepo, Lakini hili la sasa limekuja kwa namna tofauti.Wakati mwingine baba anaweza kumpa mtoto adhabu ya kulima shamba,Mtoto akalia na kulaumu sana,Lakini shamba hilohilo baadaye likaleta chakula mezani wote wakala na kufurahia. Ila tofauti iliyopo sasa,Hakuna chakula kinachokuja mezani!
19: Kushughulikia zaidi mambo yasiyokuwa na tija kwa wananchi kuliko yale yenye umuhimu na tija kwa watanzania. Imekuwa jambo la kawaida kwa awamu hii kujihusisha zaidi na makongamano,Semina elekezi,Birthday Party pamoja na hafla mbali mbali badala ya kujikita katika kufufua na kubuni miradi ya kimaendeleo itakayosaidia kuwapunguzia wananchi mzigo wa umasikini na kuinua uchumi.Hafla ya machifu na watemi si muhimu kama hafla ya utiaji saini mradi wa uchimbaji na usambazaji wa gesi ya Mtwara!
20: Kukosekana ajira. Ubunifu na uibuaji wa miradi mipya si tu umekuwa na tija kiuchumi Bali umekuwa ukiajiri vijana wengi.Kukosekana kwa ubunifu na sera mbovu za serikali zimesababisha kukoseka kwa ajira miongoni mwa vijana wengi
21: Kuongezeka matukio ya uhalifu.
Mara tu baada ya awamu ya sita kushika hatamu sote tumeshuhudia jinsi wimbi la uhalifu lilivyoongezeka.Sio tu matukio ya wizi na ujambazi bali mpaka uchomaji wa masoko kama Kariakoo, mchikichini n.k wizi mauaji na utekaji nyara vimeongezeka kwa kasi mno. Hii inaonyesha udhaifu katika usimamizi wa majeshi yetu ya ulinzi na usalama
22: Kuongezeka gharama za simu
Kutokana na kodi za miamala Kuongezeka kampuni za simu zimejikuta zikilazimika kupandisha gharama za muda wa maongezi na huduma zinginezo za simu kama vile huduma za vifurushi ili kuweza kubalance gharama za uendeshaji. Hali hii imesababisha mzigo mzito kwa wananchi hasa ukizingatia mawasiliano ni nyenzo muhimu sana katika shughuli zao za kila siku
23: Kutoa vipaumbele kwa mambo ya hovyo na yasiyo na tija kwa taifa hususan kwa wakati huu.Hapakuwa na ulazima kutumia gharama kubwa na uwekezaji katika kutumia kodi za wananchi kiongozi mkuu wa serikali kusafiri na kutumia muda mwingi kutengeneza filamu wakati fedha hiyo haina uhakika wa kurudi.Mfano fedha hiyo ingewekezwa kwenye timu maarufu zinazoshiriki ligi za ulaya ingekuwa na tija na matokeo zaidi na Rais angepata muda kutekeleza majukumu mengine ya kiserikali kuliko kupoteza muda mwingi kusafiri.
Hakika ni mambo mengi ambayo yamekuwa yakifanyika kinyume na matarajio ya watanzania wengi ambao waliwaamini viongozi wao na kuwaweka madarakani huku wakiwa na matumaini makubwa ya kuondokewa na maradhi, ujinga na umasikini ambao ndio maadui wakuu wa taifa kama ilivyobainishwa na Mwl Nyerere badala yake watanzania hao ambao wengi ni masikini na wameteseka kwa umasikini kiasi cha kusahau tarehe zao za kuzaliwa huku wakishuhudia wale waliowachagua wakikata keki ikulu!
Wewe ni kibaka?unahofia nini kupotea?wote waliopotea ni wale walikuwa wanajishughulisha na shughuli haramu.Ben Saanane yule alijitakia,unuaji mwingi ulimponza, Magufuli PhD aliipata Chuo Kikuu UDSM kwa kupitishwa na mamlaka za Chuo.Sasa yeye alikuwa anataka nini?World economics shakes up! (very common issue)
Were the causes, but we enjoy in freedom we have, hatuishi kama panya buku!
Awali watu wakuwa wanapotea ovyo kama Ben saanane, iliogofya sana.
Mungu yupi uyo anayetaka Wananchi waishi kwa shida?Mungu wa kweli katupa rasimali zote Madini,mito,Maziwa, Bahari na ardhi safi ya Kilimo lakini kutwa kuombaomba!Sukuma gang na uzushi.
Mmekosa mmekosa tu. Samia ndiye chaguo la Mungu la ukweli, au nalo utabisha?
Ziliminywa habari za kipuuzi!!Kwa miaka 6 habari zilikuwa zinaminywa, umesahau?
Wewe mwehu,Dukani wanaenda Sukuma gang peke yao? timu yenu ya Wahuni ya Msoga gang hawaendi?Wanaoteseka ni sukuma gang pekee, kutoka peponi mchezo? Hivi ndugai yuko wapi siku hizi?
Mungu wapi, Magufuli kauwawa ila siku ikifika mtasema ukweli tu!Shindana na Mungu basi. Sisi hatuwezi.
Yule mwisho 2023 au 2025!Sisi tunamuomba Mwenyezi Mungu ampe afya na utawala mrefu mama Samia.
Sasa Ghana Kuna nini Mjomba,nchi ishafirisika ile sasa hivi,Wana Hali mbaya kiuchumi balaa,fuatilia!Huyo hana akili. He is bitter labda kakatiwa mrija wa asali aliyokuwa ananyonya awamu iliyopita. Halaf hawa Sukuma gang ukiwapinga wanajua matusi tu maana awamu iliyopita walizoea kuua na kuwatesa wapinzani wao na sio kupingana kwa hoja. Kiufupi hawajazoea kupingana kwa nguvu ya hoja wamezoea hoja ya nguvu
Umeme ulikatika wapi,tupe mifano ya maeneo umeme ulikuwa unakatika ovyo awamu ya tan😵nline media kama JF zilikuwa active,tuoneshe ata Uzi wa kuilalamikia kukatika umeme awamu ya tano.Hakika kabisa uhuru wangu ni kitu cha thamani kuliko vyote sasa tupo huru .
Umeme ulikatika sana awamu iliyopita ni vile tu media ziliizimwa uhuru wao.
Ila simshangai sana mtoa mada, awamu iliyopita kuna watu pia waliinjoi, hasa kama una elements ya kanda ya ziwa .
1.Mabomu ya MbagalaBora Mama Samia mara elfu tatu kuliko muuaji
Waislamu ndo watu wenye Huruma
Alilolipanga Allah huwezi kulibadili.Yule mwisho 2023 au 2025!