Miaka Tisa (9) ndani ya JF: Kumbukizi nilivyojiunga na kuishi JF nikiwa kama Mwanafunzi wa Sekondari

Miaka Tisa (9) ndani ya JF: Kumbukizi nilivyojiunga na kuishi JF nikiwa kama Mwanafunzi wa Sekondari

adriz

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2017
Posts
12,207
Reaction score
26,521
Moja kwa Moja.

Mwaka 2015 mitaa Fulani Dar es Salaam muda huo nipo kidato Cha kwanza (Form One) nilikuwa na hamu sana ya kumililiki simu , basi nikatafuta kibubu nikawa naweka pesa za shule kama akiba na kupiga mishe ndogo ndogo kitaa ili kujazia kibubu baada ya miezi kadhaa nikavunja nikachukua kiasi kidogo nikanunua Kiswaswadu kwa mtu.

Japo kulikuwa Kiswaswadu lakini kulikuwa na uwezo na Kasi ya ajabu kwenye masuala ya kimtandao mpaka YouTube ilikuwa Ina support vizuri ,sasa siku moja nilisoma stori kwenye gazeti nikaipenda na nilivyoona itakuwa ngumu kupata gazeti kila siku ikabidi niingie gugo kuisearch ndipo nikaletwa Jf rasmi kwa mara ya kwanza n kuanza kuisoma stori kupitia Jf . Kilichonivutia zaidi upande wa comments watu walikuwa wacheshi sana na jokes za maana zilikuwepo.

Mwaka huo huo ikaja 'Freebasics' kuperuzi kurasa mbalimbali ikiwemo Jf ikawa bure hapo ndio rasmi nikawa nashinda rasmi JF kwa masaa mengi haswa jukwaa la photos, nikawa najaribu kujiunga kama member ikawa inakataa mpaka mwaka 2017 kipindi nipo Kidato Cha Tatu wakati huo nina simu kubwa tayari ndipo siku moja nikadowload app ya Jf kujaribu kujiunga tena ikakubali nikawa Mwanachama wa JF.

Faida
1. JF imenifanya niwe mpenzi sana wa kusoma vitabu ; japo tokea niko shule ya msingi nilikuwa msomaji mzuri wa vitabu na makala mbalimbali za kidini, historia na siasa nilivyojiunga JF nikajiona bado nipo mweupe inabidi niongeze maarifa zaidi ili niweze kujitetea na kuweza kufanya mijadala humu.

2. Imenifanya nijue vitu vingi vipya , kuongeza Maarifa na kupata Marafiki mbalimbali ambao tupo karibu hata nje ya JF.

3. Nk..

Changamoto
JF ilikuwa inakula muda wangu sana mpaka nikawa nahisi najinyima muda wa masomo, baadae nikawa natenga muda Maalumu tu wakuperuzi(Kila siku saa 12 jioni mpaka saa 2 usiku)

Kukutana na mijadala mizito iliyonizidi umri haswa kule Intelligence ambapo nilikuwa napenda sana kutembelea , Kadri nilivyojilazimisha kusoma nikawa naelewa vizuri na kuiona kawaida .

Kasumba ya watu kudharau watoto , kipindi Cha nyuma ilikuwepo sana ilikuwa mtu akiteleza kidogo utasikia "hapa sio fesibuku dogo" au "Kwani shule zimefunguliwa? Hapo nikawa Muoga sana kuchangia na kama nikichangia lazima nijiridhishe kwanza na ikabidi niwe kama mtu mzima mpaka ikafika stage watu wengine kunifuata PM niwashauri kwenye mambo makubwa ambayo hata sijafikia na sina uzoefu nayo.

Mengineyo.
Tokea nijinge sijawahi kupata ban Wala kumiliki ID nyingine zaidi ya hii.

Huwa sipendi watu wanijue kama nipo Jf hata nikiperuzi huwa nahakiikisha hakuna mtu karibu anayekula chabo na Kuna mahali niliwahi kufanya kazi mfanyakazi mwenzangu (JF member) nilikuwa napiga strori nae akawa anasifia JF jinsi ilivyomsaidia kupata baadhi ya Info Mimi nikajifanya siijui kabisa alishangaa sana mtu kama Mimi sipo JF Wala siijui.

IMG_20241022_112814.jpg

#UziUnaendelea
 
Moja kwa Moja.

Mwaka 2015 mitaa Fulani Dar es Salaam muda huo nipo kidato Cha kwanza (Form One) nilikuwa na hamu sana ya kumililiki simu , basi nikatafuta kibubu nikawa naweka pesa za shule kama akiba na kupiga mishe ndogo ndogo kitaa ili kujazia kibubu baada ya miezi kadhaa nikavunja nikachukua kiasi kidogo nikanunua Kiswaswadu kwa mtu.

Japo kulikuwa Kiswaswadu lakini kulikuwa na uwezo na Kasi ya ajabu kwenye masuala ya kimtandao mpaka YouTube ilikuwa Ina support vizuri ,sasa siku moja nilisoma stori kwenye gazeti nikaipenda na nilivyoona itakuwa ngumu kupata gazeti kila siku ikabidi niingie gugo kuisearch ndipo nikaletwa Jf rasmi kwa mara ya kwanza n kuanza kuisoma stori kupitia Jf . Kilichonivutia zaidi upande wa comments watu walikuwa wacheshi sana na jokes za maana zilikuwepo.

Mwaka huo huo ikaja 'Freebasics' kuperuzi kurasa mbalimbali ikiwemo Jf ikawa bure hapo ndio rasmi nikawa nashinda rasmi Jf kwa masaa mengi haswa jukwaa la photos , nikawa najaribu kujiunga kama member ikawa inakataa mpaka mwaka 2017 kipindi nipo Kidato Cha Tatu wakati huo nina simu kubwa tayari ndipo siku moja nikadowload app ya Jf kujaribu kujiunga tena ikakubali nikawa Mwanachama wa Jf.

Faida
1. JF imenifanya niwe mpenzi sana wa kusoma vitabu ; japo tokea niko shule ya msingi nilikuwa msomaji mzuri wa vitabu na makala mbalimbali za kidini , historia na siasa nilivyojiunga Jf nikajiona bado nipo mweupe inabidi niongeze maarifa zaidi ili niweze kujitetea na kuweza kufanya mijadala humu.

2. Imenifanya nijue vitu vingi vipya , kuongeza Maarifa na kupata Marafiki mbalimbali ambao tupo karibu hata nje ya Jf. .

3. Nk..

Changamoto
JF ilikuwa inakula muda wangu sana mpaka nikawa nahisi najinyima muda wa masomo, baadae nikawa natenga muda Maalumu tu wakuperuzi(Kila siku saa 12 jioni mpaka saa 2 usiku)

Kukutana na mijadala mizito iliyonizidi umri haswa kule Intelligence ambapo nilikuwa napenda sana kutembelea , Kadri nilivyojilazimisha kusoma nikawa naelewa vizuri na kuiona kawaida .

Kasumba ya watu kudharau watoto , kipindi Cha nyuma ilikuwepo sana ilikuwa mtu akiteleza kidogo utasikia "hapa sio fesibuku dogo" au "Kwani shule zimefunguliwa ? , hapo nikawa Muoga sana kuchangia na kama nikichangia lazima nijiridhishe kwanza na ikabidi niwe kama mtu mzima mpaka ikafika stage watu wengine kunifuata PM niwashauri kwenye mambo makubwa ambayo hata sijafikia na sina uzoefu nayo.

Mengineyo.
Tokea nijinge sijawahi kupata ban Wala kumiliki ID nyingine zaidi ya hii.

Huwa sipendi watu wanijue kama nipo Jf hata nikiperuzi huwa nahakiikisha hakuna mtu karibu anayekula chabo na Kuna mahali niliwahi kufanya kazi mfanyakazi mwenzangu(Jf member) nilikuwa napiga strori nae akawa anasifia Jf jinsi ilivyomsaidia kupata baadhi ya Info Mimi nikajifanya siijui kabisa alishangaa sana mtu kama Mimi sipo Jf Wala siijui.
View attachment 3132435
#UziUnaendelea

Mimi JF nilijunga baada ya kuwa natumia free basic

Hii free basic ilifungwa na kupotea baada ya march 17 2021 yaani msiba wa magufuli ukivyoisha na free basic ikawa haifanyi Kazi tena

Hongera japo nimeshangaa kuona Kijana wa form two kujiunga katika familia ya great thinkers.
 
Baadhi ya mabadiliko Jf.

Kipindi kile naingia upepo wa Siasa ulikuwa unavuma kwa Kasi sana Jf kiasi ambacho kwenye nyuzi nyingi watu wanaingizia Uccm na Uchadema hata katika majukwaa yasio ya Siasa , baadae upepo ukamia kwenye Simba na Yanga karibia kila nyuzi watu wakawa wanaleta mambo ya utani wa Simba na Yanga.

Sasa JF upepo umehamia kwenye Dini watu wmaekuwa Fanatical na Dini karibia kwenye kila nyuzi kiasi ambacho mijadala imekosa mvuto tena zaidi ya kebehi zisizo na msingi na ushabiki wa kidini hata mahali pasipo taka hivyo , kitu ambacho kilikuwa hamna ilikuwa majadiliano ya hoja na kuelimishana ndio msingi japo Fanaticism na Kebehi zilikuwepo ila sio kama sasa kiasi ambacho Uzi page zote unakuta malumbano , kuchambana na Kebehi zisizo na msingi hayo yapo kwa Waumini wa Dini zote humu.

Jukwaa la Mahusiano
Zamani ilikuwa ukiingia unakuta na nondo za kushiba watu hata wakiomba ushauri wanajibiwa vizuri kipindi Cha karibuni kukageuka kama kama sehemu ya watu kujisifu uzinzi , mambo ya kulana na mengineyo yanayofanana na hayo.
 
JF hii imebaki Historia
Nakiri kusema Jf ilikuwa tamu sana ukiingia unajishauri uanze na jukwaa lipi karibia kila jukwaa kulikuwa na Magwiji haswa ambao wanayatendea haki kiasi ambacho uikikaa siku mbili haujaingia humu unaona kama mwezi , sasa mtu anaweza kukaa hata mwezi na kuona kawaida tu na Magwiji wengi kama wameisusa kabisa Jf sasa tumebaki na kina Mpwayungu Village Maghayo The Mongolian Savage na Scumbag nyingine
IMG_20241022_114644.jpg
 
Mimi JF nilijunga baada ya kuwa natumia free basic

Hii free basic ilifungwa na kupotea baada ya march 17 2021 yaani msiba wa magufuli ukivyoisha na free basic ikawa haifanyi Kazi tena

Hongera japo nimeshangaa kuona Kijana wa form two kujiunga katika familia ya great thinkers.
Kama sio kutu piga ban account zetu humu mwaka huu ningekuwa natimiza miaka 10 sasa ila kwa fitna zao wameamua kukaa nazo mpaka leo...jamii forum sikuiz inaelekea kuwa kama Facebook tu
 
Mm pia mwaka huo nikiwa kidato Cha kwanza hko Kijiji Fulani nilikua hata sijui matumizi ya internet 😆. Vyanzo vyangu vya habari ilikua ni radio tu,hasa radio free Africa. Kipindi hicho mzee pekee kweny familia ndie Alie kua Ana miliki kibatani. Nimejiunga jamii forum mwaka Jana 2023.
 
Back
Top Bottom