Miaka Tisa (9) ndani ya JF: Kumbukizi nilivyojiunga na kuishi JF nikiwa kama Mwanafunzi wa Sekondari

Miaka Tisa (9) ndani ya JF: Kumbukizi nilivyojiunga na kuishi JF nikiwa kama Mwanafunzi wa Sekondari

Kweli kabisa bila Freebasics sidhani kama ningekuwa Mwana Jf maana nilianza kufuatilia Jf seriously baada ya ujio wa Freebasics mpaka mtaani wenzangu wakawa wananiita 'Mzee wa Freebasics' hatimaye nikazoea na kujiunga rasmi.
2016 Io form two nikiamkaa Kwanza naingia bbc Swahili,jf namalzia na goal.com ndo naenda shule nkirudi naanza kusoma makala za jf sasa kulikua na nondo Sana humu
 
Wengi tulijoin jf kwasababu ya nondo za jamii intelligence, mambo siku yako vululuvululu, uzi sio wa mapenzi kuna kiande anakuaga wa kwanza kuchomekea mizagamuo, uzi sio wa dini kuna viande wanauhusisha na dini na matusi kibao.

Hata wale magreat thinker wa zamani nao wamemezwa na na jf ya kisasa
 
ili mradi umdissapoint
Shukrani kwa kulitambua hilo , sasa watu kama hao hawanisumbui maana nimeshajichagulia kutofocuos na maneno Wala mtu yeyote anayekuja na atakaye kuja kishari ni kuwapuuza tu maana kuhangaika nao ni sawa na kujipa mateso kitu ambacho sina mamlaka nacho na Wala uwezo nao.
 
Moja kwa Moja.

Mwaka 2015 mitaa Fulani Dar es Salaam muda huo nipo kidato Cha kwanza (Form One) nilikuwa na hamu sana ya kumililiki simu , basi nikatafuta kibubu nikawa naweka pesa za shule kama akiba na kupiga mishe ndogo ndogo kitaa ili kujazia kibubu baada ya miezi kadhaa nikavunja nikachukua kiasi kidogo nikanunua Kiswaswadu kwa mtu.

Japo kulikuwa Kiswaswadu lakini kulikuwa na uwezo na Kasi ya ajabu kwenye masuala ya kimtandao mpaka YouTube ilikuwa Ina support vizuri ,sasa siku moja nilisoma stori kwenye gazeti nikaipenda na nilivyoona itakuwa ngumu kupata gazeti kila siku ikabidi niingie gugo kuisearch ndipo nikaletwa Jf rasmi kwa mara ya kwanza n kuanza kuisoma stori kupitia Jf . Kilichonivutia zaidi upande wa comments watu walikuwa wacheshi sana na jokes za maana zilikuwepo.

Mwaka huo huo ikaja 'Freebasics' kuperuzi kurasa mbalimbali ikiwemo Jf ikawa bure hapo ndio rasmi nikawa nashinda rasmi JF kwa masaa mengi haswa jukwaa la photos, nikawa najaribu kujiunga kama member ikawa inakataa mpaka mwaka 2017 kipindi nipo Kidato Cha Tatu wakati huo nina simu kubwa tayari ndipo siku moja nikadowload app ya Jf kujaribu kujiunga tena ikakubali nikawa Mwanachama wa JF.

Faida
1. JF imenifanya niwe mpenzi sana wa kusoma vitabu ; japo tokea niko shule ya msingi nilikuwa msomaji mzuri wa vitabu na makala mbalimbali za kidini, historia na siasa nilivyojiunga JF nikajiona bado nipo mweupe inabidi niongeze maarifa zaidi ili niweze kujitetea na kuweza kufanya mijadala humu.

2. Imenifanya nijue vitu vingi vipya , kuongeza Maarifa na kupata Marafiki mbalimbali ambao tupo karibu hata nje ya JF.

3. Nk..

Changamoto
JF ilikuwa inakula muda wangu sana mpaka nikawa nahisi najinyima muda wa masomo, baadae nikawa natenga muda Maalumu tu wakuperuzi(Kila siku saa 12 jioni mpaka saa 2 usiku)

Kukutana na mijadala mizito iliyonizidi umri haswa kule Intelligence ambapo nilikuwa napenda sana kutembelea , Kadri nilivyojilazimisha kusoma nikawa naelewa vizuri na kuiona kawaida .

Kasumba ya watu kudharau watoto , kipindi Cha nyuma ilikuwepo sana ilikuwa mtu akiteleza kidogo utasikia "hapa sio fesibuku dogo" au "Kwani shule zimefunguliwa? Hapo nikawa Muoga sana kuchangia na kama nikichangia lazima nijiridhishe kwanza na ikabidi niwe kama mtu mzima mpaka ikafika stage watu wengine kunifuata PM niwashauri kwenye mambo makubwa ambayo hata sijafikia na sina uzoefu nayo.

Mengineyo.
Tokea nijinge sijawahi kupata ban Wala kumiliki ID nyingine zaidi ya hii.

Huwa sipendi watu wanijue kama nipo Jf hata nikiperuzi huwa nahakiikisha hakuna mtu karibu anayekula chabo na Kuna mahali niliwahi kufanya kazi mfanyakazi mwenzangu (JF member) nilikuwa napiga strori nae akawa anasifia JF jinsi ilivyomsaidia kupata baadhi ya Info Mimi nikajifanya siijui kabisa alishangaa sana mtu kama Mimi sipo JF Wala siijui.

View attachment 3132435
#UziUnaendelea
Hiyo picha hapo chini unamaanisha nini?
 
Wengi tulijoin jf kwasababu ya nondo za jamii intelligence, mambo siku yako vululuvululu, uzi sio wa mapenzi kuna kiande anakuaga wa kwanza kuchomekea mizagamuo, uzi sio wa dini kuna viande wanauhusisha na dini na matusi kibao.

Hata wale magreat thinker wa zamani nao wamemezwa na na jf ya kisasa
Hili suala la jf kupungua ubora silielewi kabisa.

Kuna thread ya 2018 niliona mtu analalamika jf imeharibika...

Sasa najiuliza imeanza kuharibika lini?

Au watu wanapenda kusema hivyo wakiona flani kaandika kitu kinachowakera?
 
Hiyo picha hapo chini unamaanisha nini?
Begi linamaanisha
1. Masiha ya kiuanafunzi kwani nimetumia mda mrefu kuishi maisha hayo. Miaka 2 awali , 7 primary, 4 secondary , 2 advance na , 3 University. Karibu nusu ya umri nimetumikia kubeba begi kutafuta Elimu.

2. Silaha (Gun) ina Symbolize mapambano , maisha yote ya mwanadamu yanahitaji mapambano katika kufanikisha malengo ,na kuyaendae mambo kwani changamoto ni nyingi mno tukianzia watu kukuatisha ,tamaa ,kukurudisha nyuma ,kufanyia figisu , za kisaikolojia nk sasa inatakiwa kudeal nayo kwa mapambano kielimu , kiakili na mengineyo kama ikihitajia..

Sasa hiyo Gun ina wakilisha mapambano na katika mapambano katika Matumizi ya silaha Vilevile inahitajika umakini kuhakikisha unalenga panapo husika , kwa usahihi ndani ya wakati muafaka

#TheGunMan

Cc : Selikavu
 
Hili suala la jf kupungua ubora silielewi kabisa.

Kuna thread ya 2018 niliona mtu analalamika jf imeharibika...

Sasa najiuliza imeanza kuharibika lini?

Au watu wanapenda kusema hivyo wakiona flani kaandika kitu kinachowakera?
Amna fuatilia tu mijadala ya miaka hiyo na sasa, hata ile tu ya mtu kuomba msaada au maelezo ya jambo fulani.

Comments za mwanzo si ajabu hata zisihusiane na alichoomba zaidi ya kejeli na matusi sometimes, ila nyuma huko watu ni kama walikua wanaoneshana umwamba nani anajua zaidi hivyo utakuta majibu lukuki.

Hata ukisearch kitu google, ukaletewa majibu toka jf, ni majibu ya miaka ya nyuma sio sasa.
 
Kwanini The Mongolian Savage na Maghayo wanakuita nyau??
Na hashtag yao ya nyau de adriz
Sijui kwa nini ila jamaa ana shida kichwani , labda kwa vile nafichua maujinga yake ndio maana ananishambulia hivyo.

Kwa vile nishamjua shida nyaja kichwani zimekatika nimeamua kumpuuza rasmi yaani mtu mzima amefikia stage ya kutishia watu kujamba humu na mpk kurekodi clip akila nyetoh na kurusha Jf live, automatically anakuwa Barbarian wa kupuuzwa tu.
 
Duh, ila hii mitandao inaweza kufanya ukatukanana na mwanao wa kuzaa kabisa.

Unakuta mtu anakutukania mama yako kumbe in reality anamtukana bibi yake tena kwa kutumia pesa za bundle zako mwenyewe.

Anyways hongera kijana kwa kutimiza miaka 10 ya JF.
 
Back
Top Bottom