Miaka Tisa (9) ndani ya JF: Kumbukizi nilivyojiunga na kuishi JF nikiwa kama Mwanafunzi wa Sekondari

Kwanini The Mongolian Savage na Maghayo wanakuita nyau??
Na hashtag yao ya nyau de adriz
Jitu zima likifikia stage hii ni wakuonewa huruma tu , huyo jamaa akiwa na Maghayo na The Mongolian Savage wanaunda kikosi hatari Cha Kihuni humu " The Ghayos Gang " kwa vile Mimi ninazo siri zao na nimepanga kuwalipua kwa ushahidi nahisi ndio maana jamaa amekuwa akiniaAttack frequently.

Sasa nimempuuza kitambo simjibu , kumtag Wala kumQoute nasubiri achoke maana atafanya maujinga yake kisha atachoka na kutulia hapo ndipo ataona ' My vicious move ' sasa anasomewa ramani tu.
IMG_20241022_151358.jpg
 
JF ni ya watu wenye akili sio kila mtu anaweza kujiunga JF, wapo watu wengi niliwapa abc lakini hawajashawishika kujoin, wanaona lakini hawaelewi!

mimi nilijaribu kujiunga mwaka 2012 bila mafanikio, nikaendelea kuitumia kama guest, nilichojivunia ni kwamba kila nilichokitafuta ama kukiwaza, tayari kilikuwa kimejadiliwa humu!
JF bado haijapoteza thamani kwakuwa hata hizo nondo mnazozisema bado zipo humu na ninaamini hujazimaliza zote, zimehifadhiwa kwa manufaa ya badae
 
Jitu zima likifikia stage hii ni wakuonewa huruma tu , huyo jamaa akiwa na Maghayo na The Mongolian Savage wanaunda kikosi hatari Cha Kihuni humu " The Ghayos Gang " kwa vile Mimi ninazo siri zao na nimepanga kuwalipua kwa ushahidi nahisi ndio maana jamaa amekuwa akiniaAttack frequently.

Sasa nimempuuza kitambo simjibu , kumtag Wala kumQoute nasubiri achoke maana atafanya maujinga yake kisha atachoka na kutulia hapo ndipo ataona ' My vicious move ' sasa anasomewa ramani tu.View attachment 3132658
😂😂 Kwa kuanika rika yako si ajabu atakua kaona aibu, bila shaka ni mtu mzima kabisa, atakua na majuto kuandika upuuzi mbele ya wanae.
 
Ahse kwanz picha linaanza kipind hicho nipo Chuo nimewah vzr kipind cha Asubuh maan yule Lecture alikuwa mtabe balaa.
vile sijakaa sawa nakuta Ka display pale Front images ya PC yake kwa projector. kuangalia vzr nakuta ana App ya JamiiForum.

ahse nikawaza hap usikute hata huyu mzee tukiwa kweny Mada zetu pendwa za vijan nae yumo na tunajibizana nae😁😁
 
Moja kwa Moja.

Mwaka 2015 mitaa Fulani Dar es Salaam muda huo nipo kidato Cha kwanza (Form One) nilikuwa na hamu sana ya kumililiki simu , basi nikatafuta kibubu nikawa naweka pesa za shule kama akiba na kupiga mishe ndogo ndogo kitaa ili kujazia kibubu baada ya miezi kadhaa nikavunja nikachukua kiasi kidogo nikanunua Kiswaswadu kwa mtu.

Japo kulikuwa Kiswaswadu lakini kulikuwa na uwezo na Kasi ya ajabu kwenye masuala ya kimtandao mpaka YouTube ilikuwa Ina support vizuri ,sasa siku moja nilisoma stori kwenye gazeti nikaipenda na nilivyoona itakuwa ngumu kupata gazeti kila siku ikabidi niingie gugo kuisearch ndipo nikaletwa Jf rasmi kwa mara ya kwanza n kuanza kuisoma stori kupitia Jf . Kilichonivutia zaidi upande wa comments watu walikuwa wacheshi sana na jokes za maana zilikuwepo.

Mwaka huo huo ikaja 'Freebasics' kuperuzi kurasa mbalimbali ikiwemo Jf ikawa bure hapo ndio rasmi nikawa nashinda rasmi JF kwa masaa mengi haswa jukwaa la photos, nikawa najaribu kujiunga kama member ikawa inakataa mpaka mwaka 2017 kipindi nipo Kidato Cha Tatu wakati huo nina simu kubwa tayari ndipo siku moja nikadowload app ya Jf kujaribu kujiunga tena ikakubali nikawa Mwanachama wa JF.

Faida
1. JF imenifanya niwe mpenzi sana wa kusoma vitabu ; japo tokea niko shule ya msingi nilikuwa msomaji mzuri wa vitabu na makala mbalimbali za kidini, historia na siasa nilivyojiunga JF nikajiona bado nipo mweupe inabidi niongeze maarifa zaidi ili niweze kujitetea na kuweza kufanya mijadala humu.

2. Imenifanya nijue vitu vingi vipya , kuongeza Maarifa na kupata Marafiki mbalimbali ambao tupo karibu hata nje ya JF.

3. Nk..

Changamoto
JF ilikuwa inakula muda wangu sana mpaka nikawa nahisi najinyima muda wa masomo, baadae nikawa natenga muda Maalumu tu wakuperuzi(Kila siku saa 12 jioni mpaka saa 2 usiku)

Kukutana na mijadala mizito iliyonizidi umri haswa kule Intelligence ambapo nilikuwa napenda sana kutembelea , Kadri nilivyojilazimisha kusoma nikawa naelewa vizuri na kuiona kawaida .

Kasumba ya watu kudharau watoto , kipindi Cha nyuma ilikuwepo sana ilikuwa mtu akiteleza kidogo utasikia "hapa sio fesibuku dogo" au "Kwani shule zimefunguliwa? Hapo nikawa Muoga sana kuchangia na kama nikichangia lazima nijiridhishe kwanza na ikabidi niwe kama mtu mzima mpaka ikafika stage watu wengine kunifuata PM niwashauri kwenye mambo makubwa ambayo hata sijafikia na sina uzoefu nayo.

Mengineyo.
Tokea nijinge sijawahi kupata ban Wala kumiliki ID nyingine zaidi ya hii.

Huwa sipendi watu wanijue kama nipo Jf hata nikiperuzi huwa nahakiikisha hakuna mtu karibu anayekula chabo na Kuna mahali niliwahi kufanya kazi mfanyakazi mwenzangu (JF member) nilikuwa napiga strori nae akawa anasifia JF jinsi ilivyomsaidia kupata baadhi ya Info Mimi nikajifanya siijui kabisa alishangaa sana mtu kama Mimi sipo JF Wala siijui.

View attachment 3132435
#UziUnaendelea
Hongera kijana upande wangu id yangu ya kwanza ni mwaka 2008 nikiwa form 6..
Then ikapotea nikarudi ten rasmi 2011
 
Kabla kuniomba code ya DLS uwe unanisalimia hahahahhahahaha
 
Dogo' .....umepata bahati kujua mitandao yenye 'ustaarabu' na maarifa mapema. Ama sivyo na wewe ungekuwa unatega camera ya simu unabinua makalio kama wenzako wa miaka 2000.
Kweli kabisa , kipindi nipo O _level nilianya research fupi darasani kati ya wote ambao tulikuwa tunamiliki simu hakuna anayeijua Jf nikaConlude Mimi tu mwana Jf karibia shule nzima tena hapo ni Dar ila Facebook, IG karibia wote walikuwa nazo.

Advance nikajaribu tena darasani kwangu kuuliza nikijifanya siijui wakatokea wengi kidogo kuonyesha wanaifahamu ila walikuwa Wana mitizamo hasi kuhusu Jf na wakasema kuwa ni mtandao wa wazee nisijaribu kujiunga.

Ila sasa nikawa napendwa na Wanafunzi wenzangu ikawa mambo mengi naulizwa Mimi nielezee au nifanye uchambuzi kwa kuniona najua mengi na Niko very deep hata katika masomo ya darasani hadi wakawa wanashangaa nasoma vitabu vipi ambayo wao hawasomi na source za information zangu ni zipo ?
 
Mwaka 2015 upo kidato cha Kwanza, ina maana kama utakuwa ulisoma Masomo ya Sayansi na ukaenda Chuo Kikuu kusoma Engineering, utakuwa unaingia Mwaka wa nne kukamilisha miaka minne ya Engineering 🙌👏👏👏

Kweli miaka inakimbia, hongera sana
 
Back
Top Bottom