Miaka ya 2000's nlifungua Internet Cafe. Ndipo nlipoanzia kupiga bingo na kupasua mioyo

HTC alikuwa smart sana ila kilicho mponza ni jeuri ya bado kuwaza hakuna mpinzani kama BB na Nokia
Saana. Nakumbuka BBM nilikuwaga na mtoto mkali kipindi hiko ndio iko hot. Ilikuwa ni hakuna kulala! πŸ˜€
 
Miaka 90 -2000 wenye pikipiki walikuwa wachache na hata muhimbili ikutarajia kuwa na kitengo kwa jina bodaboda wodi yao.

Toyota Baloon,escudo,Mark 2,Pegoti na n.k wajanja wa mjini.

Kubeba sanduku la mkononi unaonekana ndio mjanja.

Posta ndio sehemu kila kitu tanzania unapata mpaka sahii ya raisi.

Ukiishi kino,kijitonyama,masaki,mikocheni,makumbusho na sinza basi unaogopwa na maeneo mengine
 
Miaka 90-2000
Demu anayesoma jangwani anaonekana kichwa sana alafu kicheche
 
Miaka 90-2000
kuna watoto waleo sijui kama wanafahamu jiwe la fatuma.
sijui kama wanafahamu antena ya makopo ya castle na mifupa ya samaki.

Gari ya saibaba na ile iliyokuwa chinja chinja.

Miaka hiyo sabasaba ilikuwa sabasaba kweli na nanenane kweli.

Panasonic,JVC,Nation na hitach uwezi kukosa nyumba ya mtu.

Makongo kipindi cha kina marehemu ngwear na afande miraji.

wemesepetu na kajala mpaka leo walitakiwa waitwe bibi.

Chesko mzee wa matunda alitamba sana clouds fm bado hipo posta karibu na IFM.

Dar ya zamani ilikuwa nzuri sana
 
Kabisa.... Upo sawa.
 
Chesco mzee wa matunda yupo wapi? Zamani sana. Akina bokoman mwanamkongo man, tewa s tewa, father nagumo fanani comoro?
 
Hawa ndo walikuwa wateja sana.... Akiinuka unamwona anashindwa hata kutembea....jicho jekundu.... Unacheka tu.. anakuja mwingine na makaratasi kibao kama ana issue ya msingi vile. Anakwambia nina issue nyeti nataka computer ya sehemu tulivu. Kumbe anataka akacheck porno.
 
Umenikumbusha myaka hiyo nilimiliki desktop pekee kitaani.
Basi masela walikuwa hawakauki magetoni kipindi hicho nina ots turntable ma dj wa uswazi hawakauki achana na wale wanakuja kucheza need for speed.
Kulikuwa na need for speed underground na mortal combat...baadaye ikaja GTA
 
Wengi hawajawahi hata kulisikia jiwe la fatuma. Ukisikia Kiih.... Tayari jamaa wamo ndani.
 
Yaani Kwa hicho kichwa nilijua lazima unavuts bangi
 
umeacha bangi wee mzee? πŸ˜€ au bado unashtua mara moja moja πŸ˜€
Sasa unaachaje Bhangi ndugu yangu? Yaani niache bhangi nivute hewa tu? We mwenyewe mbali na kunywa maji kuna vitu vingine unakunywa....uongo?
 
Wazee wa Java tulikuwa tukijifungia ndani kusaka magemu kwenye Waptrick. πŸ˜†

Nashangaa watoto wa Android na IOS wanavimba!
Achana games za waptrick na java, watu tumeanza kuperuzi kwa Siemens zile zinatoa mwanga wa orange
 
Wewe ni mwanamke? Utakuwa wa kwanza mimi kumsikia amecheza GTA.
yap ni mwanamke, hio need for sped nilikia siiwezi naona imekaa kiume ume sana lakini GTA na ile sjui ni bar sjui ni club inaitwa MALIBU nimecheza mnoo mpaka bas
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…