Miaka ya 2000's nlifungua Internet Cafe. Ndipo nlipoanzia kupiga bingo na kupasua mioyo

Mkuu hapa nadhani umechanganya madesa, ps1 na ps2 zote zimeanza mwaka 2000, ps ndio ilianza mwaka 94 so utakuwa unazungumzia playstation only ila matoleo ya mbele (ps1 na ps2) yenyewe hayakuwepo miaka ya 90s
 
enzi za

1. Raha dotcom
2. Africa online
3. Cats

na wengineo.
 
Mimi nakumbuka nikikuwa na simu yangu ya tatu ilikuwa siemens c55, ilikuwa na game flani linaitwa prince of persia ilikuwa hatari sana.

Simu yangu ya kwanza ilikuwa philips savy maarufu kidole gumba.
 
Time flies. Mwaka 2004 napata Ngamizi/Computer yangu ya kwanza IBM toka Jozi kwa Madiba,ina Window 98, RAM 512MB, Floppy Disck, CD writer na Mouse yake ya goroli. Hii ni baada ya Mjomba wangu (RIP) kuzamia huko mwaka 98 na kuja bongo 2004 akiniletea Radio ya CD Aiwa na Amplifier aina ya Kenwood na nikaona nifungue studio. Nikafungua Studio yangu mjini kati. Basi unaambiwa kazi yetu ilikuwa kukopi CD albam kali enzi hizo na kuzichoma katika CD za kawaida kila video tukifanya TSH 2000.
Nakumbuka nimewahi mchomea Mhindi albam ya R.Kelly TP2.com na Coast to Coast ya Westlife kwa Tsh 70k ya wakati huo.
Mtoa mada umenikumbusha mbali sana ngoja niishie hapa.

2000's truly gave me some of the best moments of my life.
 
Miaka 90 benzi beach yote,mwenge,tegeta,kimara,tabata,kigamboni,mbagara na airpot ni shamba
Tegeta ni mji mkongwe......naanzza kuuona kuanzia 80' ukiwa umechangamka
 
🤣🤣🤣 Safi sana. Ungeendelea kutiririka usikatishe story .. aiseee kitambo sana. Uncle bado yupo? Huyo mhindi akikuona kwa sasa anacheka sana....
 
Mkuu hapa nadhani umechanganya madesa, ps1 na ps2 zote zimeanza mwaka 2000, ps ndio ilianza mwaka 94 so utakuwa unazungumzia playstation only ila matoleo ya mbele (ps1 na ps2) yenyewe hayakuwepo miaka ya 90s

umazaliwa mwaka gani !.
Ps 1 mwaka 1994 ya kwanza baada ya miezi 5 kutoka inakuja naona kwa jamaa sasa anaishi UK kaletewa. usikalili labda ulikuwa unasubilia vichelewe uje kupokea.
 
Haaa enzi za tagged, myspace, msm messenger, na Yahoo's messenger,

Mileage za watoto kwa sasa zimefunjwa na Badoo!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…