Miaka ya 90 pale uwanja wa ndege mzee Mwinyi aliwahi kunipa hela, fulana kwa mkono wake mwenyewe kisha akanambia maneno haya...

Daah ker elimu muhimu
Wazazi wa mzee Mwinyi walilenga kumpeleka Zanzibar kujifunza elimu akhera, maana hapa kwao bara elimu hiyo ilikuwa haipewi kipaumbele na serikali ya kikoloni.

Mzee alipofika kule Zanzibar akajiongeza kwa kusoma na elimu dunia, ambayo baadae ilikuja kumletea matokeao makubwa katika maisha yake hadi kupeleka kuwa raisi wa nchi mbili. Huku kwao kwa asili alipozaliwa na kule alipohamia.

So mzee Mwinyi aliuona ubora wa elimu ndio maana alinisisitiza nisimame na elimu iwe jua iwe mvua.
 
Hakika mzee Mwinyi atakumbukwa na wengi kwa sababu ya kuwafanyia watu mema mengi.

Alikuwa tayari kutukanwa, kusimangwa, kuzushiwa ili kuifungua nchi na kuhakikisha kila mtu anapata kile anachotakiwa kupata. Aliruhusu biashara huru, kila mtu alisogezewa huduma alizokosa karibu yake, shule, maduka, hospital, vyakula, barabara na vitu vingine vingi ambavyo havikuwa vinapatikana kirahisi kabla ya uongozi wake.
 
Hakuwa na makuu hata. Siku moja alifika kwenye shule moja akajaribishwa bites kwe darasa akapata, kisha akaenda kujisaidia katika choo cha mkuu wa shule akisindikizwa na askari, alitushika mkono kusalimia. Hakukuwa na mbwembwe hata...
Nakumbuka akiwa raisi, mvua iliwahi kunyesha kubwa ikasabaisha uharibifu mkubwa maeneo mengi ya Dar es salaam. Mzee Mwinyi akiwa raisi alitembelea maeneo hayo tena akiwa mstari wa mbele kuwasaidia watu kutoa takataka mbali mbali katika mitaro iliyoziba.

Mimi nilimuona pale Manzese sokoni akiwa na buti za mvua akiingia matopeni kuwasaidia wafanya biashara kutoka vitu vyao vilivyoharibiwa vibaya na mvua.
 
Leo ndo nimejua kwann wewe ni mtata, mgumu kuelewa kama mawe Yale ya mtoni.

Bibi Yako yaezakuwa amekukabidhi mikoba😀
 
Hakuwa na makuu hata. Siku moja alifika kwenye shule moja akajaribishwa bites kwe darasa akapata, kisha akaenda kujisaidia katika choo cha mkuu wa shule akisindikizwa na askari, alitushika mkono kusalimia. Hakukuwa na mbwembwe hata...
Enzi hizo hapakuwa na hizi Takataka zinazojiita Chawa.

Viongozi walikuwa Real, hawakuwa wakipewa sifa za Uungu na wala kujiona wao ni Wa Pekee kama ilivyo sasa.
 
Sipendi kuzungumzia udini maana hata kipindi cha hayati Magufuli serikali yake ilikuwa na mawaziri watatu tu waislam, huku waliobakia zaidi ya ishirini wakiwa wakristo. Kwako wewe hilo haukuliona maana huenda lilinufaisha upande wako.

Kumbuka raisi Mwinyi ndio raisi wa kwanza kumleta papa John Paul nchini Tanzania. Sasa huo udini wako unaosema hapa sijui ni udini upi?

Ngoja nijikite kwenye point za nje ya udini wako. Unasema Mwinyi alisabisha watumishi waache kazi, huo ulikuwa ni utashi wao. Lakini kwa vile katika taifa huwa kuna watu wengi huwa hawana kazi, basi walioacha kazi nafasi zao zilichukuliwa na watu waliokuwa hawana kazi tatizo liko wapi? Lakini umesahau kuwa wakati Mwinyi anaingia madarakani aliikuta hazina ya taifa ikiwa tupu, haina hela. Serikali nzima ilikuwa imefilisika na watumishi wengi walikuwa wanafanya kazi kizalendo tu bila kupata mshahara wowote. Alipoingia Mwinyi akaifungua nchi, wafanyakazi wakaanza kupokea, na wengine kuamua kuacha kazi ili kutoa fursa kwa wengine alaf wao wakajikita kwenye biashara, sasa kati ya mtu kufanya biashara bila kulipwa na yule anaelipwa na kuamua kujiongeza kufanya biashara ili kukidhi mahitahi ya maisha yake nani aliekosea?

Nyerere kamlaumu Mwinyi kuhusu loliondo, lakini Nyerere huyu huyu wakati wa utawala wake alizuia vyombo vya habari visiandike kuhusu matatizo wanayopitia wananchi kama vile kukosa mahitaji ya msingi madukani, watu wazima kuvaa midabwada na suruali za viraka, kuvaa chachacha, watoto kwenda shule bila viatu, kusababisha watu wenye maono makubwa kama kina Kambona kukimbia nchi nk. Nchi ilikuwa katika hali mbaya hadi kupelekea kuponea kupinduliwa mara mbili na baadhi ya wanajeshi, ambao walichoka na uozo wa serikali yake na kuamua kusimama upande wa wananchi.

Na bado mpaka leo hayati Nyerere tunamsifu kwa mema tu, hatujawahi kumsema kwa baya, ila haujaja kupinga sifa hizo alizopewa baada ya kufa. Wewe ndo mnafiki.
 
Atangazwe mwenye kheri kwenye upande wa Dini/Imani yake Hayati Mzee Mwinyi,,,ana mema mengi mnoo na kwa wengi pia!!###AmpumzikePanapostahili###
Swadakta kabisa, japo sina uhakika kama katika dini yake hilo swala linaruhusiwa.
 
Kibunda kilikuwa cha Sh. Ngapi?

Mimi alinipa bendera ya Tanzania siku aliyokuja Papa John. Tulikuwa miongoni mwa wapokea wageni.

RIP Mzee Mwinyi.
Kilikuwa elf 25, japo mimi niliambulia elf 10 zingine ziliishia kwa wakubwa na wadogo zangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…