Miaka ya 90 pale uwanja wa ndege mzee Mwinyi aliwahi kunipa hela, fulana kwa mkono wake mwenyewe kisha akanambia maneno haya...

Wazee wa kuunga story za marehemu huwa wengi misibani hasa msiba wa tajir wanajikutaga wanamjua marehemu ili yapige menyu ya kutosha

Naona mzee wa kuunga na msiba wa tajiri umejiunga sio ...
 
celebrity worship syndrome
 
Basi fanya ukamzike Babu kipenzi cha watanzania.
Alikuachia ushauri wa kuisaka elimu kama dira yako. Je ulifanikiwa kufanyia kazi ushauri wa mzee?
Amekuachia alama kubwa.
Innalillahi waina ilaihi raajiun
 
Nimeskia kuna ile chama cha wafanyakazi walimkacha Mwinyi akiwa rais kwenye maadhimisho ya Mei Mosi wakamualika Nyerere ambae kwa wakati huo alikua mstaafu. Nyerere nae alipofika Mbeya akamkandia sana rais (Mwinyi) lakini mzee wa watu wala hakumind, hakua na kinyongo na mtu na maisha yakaendelea. Nikakumbuka hiki kitendo angefanyiwa JIWE[emoji26] hilo balaa sijui angeamulia nani. R.I.P Alhaj Mzee Mwinyi.
 
Wazee wa kuunga story za marehemu huwa wengi misibani hasa msiba wa tajir wanajikutaga wanamjua marehemu ili yapige menyu ya kutosha

Naona mzee wa kuunga na msiba wa tajiri umejiunga sio ...
Kwa vile comment yako haibadili ukweli wa kile nilichokiandika, basi acha nikupuuze kama ulivyopuuzwa na wengine.
 
Mikoba ya bibi!!

Ili uendeleze ngoma za asili πŸ˜€
Bibi aliacha na kuegemea zaidi kwenye maswala ya dini. Na huo ndio ukawa mwanzo wa kusambaratika kabisa kwa kundi hilo la ngoma zao za kitamaduni.

Ilikuwa wakienda kwenye show wanalipwa na bibi anamgawia kila mmoja sawa na mungine. Alivyojitoa hakupatikana mwenye uwezo wa kuongoza vizuri kama yeye. Wakawa wakienda kupiga sehem wakirudi wanadhulimiana. Hela za kutunzwa bibi alikuwa hata akitunzwa anawapa na wenzake, lkn hawa wengine mtu akitunza anaichimbia kwenye matiti na kuibana na sidiria.

Mwisho kikundi kikaanguka chali πŸ˜€πŸ˜‚
 
Hata mimi nina mambo mengi ambayo nimeshuhudia Mzee huyu akionesha utu na uungwana wake. Uliloandika latosha na nashukuru umefanya kwa niaba yetu sote. Mwenyezi Mungu Amrehemu Mzee Mwinyi! RIP Mzee Ruksa!
 
Hata mimi nina mambo mengi ambayo nimeshuhudia Mzee huyu akionesha utu na uungwana wake. Uliloandika latosha na nashukuru umefanya kwa niaba yetu sote. Mwenyezi Mungu Amrehemu Mzee Mwinyi! RIP Mzee Ruksa!
Nashukuru sana ndugu yangu πŸ™πŸ™πŸ™
Mwenyezi Mungu amuweke miongoni mwa waliokuwa wema na wachamungu hapa duniani.
 
Basi fanya ukamzike Babu kipenzi cha watanzania.
Alikuachia ushauri wa kuisaka elimu kama dira yako. Je ulifanikiwa kufanyia kazi ushauri wa mzee?
Amekuachia alama kubwa.
Innalillahi waina ilaihi raajiun
Bahati mbaya msiba imetokea nikiwa nje ya nchi, lkn nimeanza kumuomba tangu niliposikia taarifa za kuumwa kwake, nikaendelea kumuombea hata baada ya kusikia taarifa za kifo chake.

Ushauri wa elimu niliufanyia kazi, japo sikufika mbali kivile, but i tried to follow his legacy. RIP mzee wetu mwema na mchamungu Ally Hassan Mwinyi.
 
Mwinyi alitengenezewa mazingira ya kuchukiwa, kudhihakiwa na kufedheheshwa na mzee "mchonga" ili kuyafuta mazuri yake yote aliyofanya kwa taifa hili, na kamwe isije kuonekana kuwa amefanya mambo makubwa kwa taifa.

Hao wafanyakazi walimwalika mzee Nyerere na kumkacha Mwinyi huku wakiwa wameshapokea mshahara, wameshiba na kuvaa vizuri. Walisahau kuwa kabla ya Mwinyi kuingia madarakani wengi wao walikuwa wanafanya kazi bila mshahara, wengine wanakwenda shuleni wakiwa wamevaa midabwada baada ya kukosa hela ya kununua nguo lkn pia hata hizo nguo zilikuwa hazipatikani sokoni, wengine walikuwa wanashindia mlo mmoja tena wa mihogo ya kuchemsha nk.

Sema ndo hivyo, wengi walitengenezewa yale mazingira na kujikuta wanasahau kule walipotokea na kukandia neema waliyoipata kwa sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…