Habari zenu wakuu,
Leo nimetimiza miaka sita tangu nimejiunga na huu mtandao wetu pendwa (yaani nilijiunga nikiwa kijana mpaka nimekuwa mzee hahaa). Nampongeza sana mwanzilishi wa JamiiForums kwa kuanzisha hii platform maana ni ya kipekee na ina ladha ya peke yake.
Kusema kweli nimejifunza mengi sana kupitia mada za hapa na zimenisaidia sana katika kubadili mtazamo kuhusu maisha achilia burudani zisizokwisha aisee kweli hii ni stress free zone.
Hum ndani kuna kila kitu, kuna wakati utafurahi, utajifunza,utapenda, utapendwa, utahuzunika, utaumia, yote tumeumbiwa wanadamu cha muhimu ni kusonga mbele huku ukimtegemea Mungu na kuzichukua changamoto kama sehemu ya maisha.
Cha mwisho ninashukuru miaka yangu yote hii sijawahi kula ban [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]. Hili nalo la kujivunia eti, si kwamba mimi ni mwema sana kuzidi akina fulani wanaokula ban kila baada ya siku mbili ( siwataji [emoji87]), ni neema tu.
Nawapenda nyoote hata msionipenda naomba niwatakie heri ya Christmas na mwaka mpya.
NB
Kwa mtu yeyote niliyewahi kumkwaza katika kipindi nilichokuwepo Jf naomba anisamehe hata akinifungukia hapa sehemu niliyomkwaza au ambayo huwa namkera. Mimi wengi nimewasamehe bado wachache tu [emoji87][emoji87][emoji87]