Miaka yangu 6 Jf

Miaka yangu 6 Jf

Nilikuwa kwenye magroup fulani ya kisiasa Facebook watu wakawa wanaiongelea saa nyingine wanaleta link, nikalike page yao baadae na mimi nikajoin, halafu mwanzo nilijua ni forum ya kisiasa tu.
Zamani za kale ilikuwa imejikita huko zaidi...

Haya majukwaa mengine ni watoto na wajukuu wa jukwaa la siasa...
 
Habari zenu wakuu,
Leo nimetimiza miaka sita tangu nimejiunga na huu mtandao wetu pendwa (yaani nilijiunga nikiwa kijana mpaka nimekuwa mzee hahaa). Nampongeza sana mwanzilishi wa JamiiForums kwa kuanzisha hii platform maana ni ya kipekee na ina ladha ya peke yake.
Kusema kweli nimejifunza mengi sana kupitia mada za hapa na zimenisaidia sana katika kubadili mtazamo kuhusu maisha achilia burudani zisizokwisha aisee kweli hii ni stress free zone.
Hum ndani kuna kila kitu, kuna wakati utafurahi, utajifunza,utapenda, utapendwa, utahuzunika, utaumia, yote tumeumbiwa wanadamu cha muhimu ni kusonga mbele huku ukimtegemea Mungu na kuzichukua changamoto kama sehemu ya maisha.
Cha mwisho ninashukuru miaka yangu yote hii sijawahi kula ban [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]. Hili nalo la kujivunia eti, si kwamba mimi ni mwema sana kuzidi akina fulani wanaokula ban kila baada ya siku mbili ( siwataji [emoji87]), ni neema tu.
Nawapenda nyoote hata msionipenda naomba niwatakie heri ya Christmas na mwaka mpya.

NB
Kwa mtu yeyote niliyewahi kumkwaza katika kipindi nilichokuwepo Jf naomba anisamehe hata akinifungukia hapa sehemu niliyomkwaza au ambayo huwa namkera. Mimi wengi nimewasamehe bado wachache tu [emoji87][emoji87][emoji87]
Huwa unanikera ...

Maandishi yako madogo

Hafu unaongea kwa sauti ndogo sana we msichana
 
Hahaa mimi 2014 ndio nimeacha, nawakumbuka baadhi ya memba akina Kimeta wa Mpui, Bruno Kims, mheshimiwa Bananga, akina Ben daah magroup yalikuwa hot yale
Hahahaha

Hivi bado yapo haya magroup? Sijaingia FB toka 2015
 
Back
Top Bottom