Mfano, Wanafunzi shuleni hapo wanatakiwa kulipa Tsh. 15,000/-, Debe mbili za mahindi na lita moja ya mafuta kwa kila Mwanafunzi mmoja.
Shule hiyo ya Serikali yenye Wanafunzi 400 (darasa la kwanza hadi la sita) ina Walimu sita wa kuajiriwa na Walimu wa tatu wa kujitolea ambapo wazazi ndiyo wanawalipa posho wale wa kujitolea Tsh. 100,000- kwa mwezi.
Mchanganuo wa michango hiyo ipo kama ifuatavyo: -
a) 5,000/- ya kukobolea Mahindi
b) 10,000/- inatumika kwenye matumizi mengine ikiwemo kulipia Walimu hao wanaojitolea.
Ikitokea Mzazi au Mlezi hajatoa mchango anamakatwa na Mgambo na kutupeleka kwa Ofisi ya Mtendaji, tunajiuliza mbona wanatukamata bila hata kutupa barua ya wito.
Suala la michango ni hiyari lakini imekuwa kama Sheria na kama ni kuisaidia Serikali tumeshaisaidia sana, nadhani umefika muda na sisi tusaidiwe.
Tunapokamatwa tunalazimika kwenda kukopa kwa riba kubw aili Watoto wetu waweze kusoma.
Wazazi wanahoji matumizi ya fedha hizo ambazo wanasema hawajawahi kusomewa matumizi yake.
Michango hiyo huitishwa na Walimu wenyewe, tunachohoji ni kuwa kwa nini Maafisa Elimu au Mkurugenzi wasiende shuleni hapo na kutangaza rasmi kuhusu michango hiyo na uhaba wa Walimu na kwamba wazazi wabebe jukumu la kujitolea kwa kutoa michango hiyo.
Aidha, walilalamika kuwa nguvu hutumika kwa Wazazi wanaochelewa kulipa kwa kukamatwa na migambo ya kijiji na kupelekwa kwa Mtendaji kujibu mashtaka.
Vilevile Wazazi wa kila kitongoji wana zamu ya kwenda kuwapikia Watoto wao shuleni kwa kujitolea.
Ukiacha kuwa wanatakiwa kulipa hiyo michango bado wanatakiwa kwenda zamu ya kuwapikia watoto na pia Wanafunzi ndiyo wenye jukumu la kukata kuni za shughuli hiyo.