Michango ya harusi imekua kero kwangu, mbona mimi sikuchangisha mtu ata senti moja

Kuchanga siyo lazima, ukiona message ya mchango isome lakini usiijibu. Akikutumia kikatuni au meme una reply 'Ha ha haaa'.

Akikuuliza mambo mengine unamjibu vizuri. Akikumbushia mchango unauchuna. Akiku block na wewe unam block halafu unam delete kabisa.

Mtu akitaka kuoa na aoe, akitaka sherehe ni jukumu lake kutafuta pesa na kualika watu wajumuike naye kwenye siku ya furaha yake badala ya kuchangisha watu kwa ajili ya tukio lake, ndiyo maana watu wanagongeana sababu ukichangiwa maana yake unayemuoa ni cha wote usipochanga hautatakiwa kumla.
 
Huu ni upumbavu wa kuiga vitu tusivyoviweza.Nimeongea na mashekh,mapadri na wachungaji.Wanachotaka wao ni ufunge ndoa madhabahuni,wanaruhusu uende na mkeo na wasimamizi wako.Hizo sherehe ni kutafuta sifa za kijinga,haswa kwa wasiojiweza.Mtu anafanya sherehe ya milioni 50 halafu anarudi chumba kimoja cha kupanga.
 
Kama mama yako mzazi bado yupo hai, hio mipango yako, isahau, mama zetu wa kiafrika ndo huwa Wana shughuli, utaona wageni hao siku ya harusi hata huwafahamu wewe kazi yako kupokea zawadi na kuwashika mikono😃😃
 
Umenifundisha umafia hatari mkuu😂😂😂 kwamba una reply hahaaa , akiblock na we block 😂😂😂

💪💪💪
 
Wakihitaj michango wanakuchangamkia weeee unawachangia af harusi ikipita wanaanza kula buyu kama hawakujui.

Swala la harusi kila mtu apambane na hali yake. Haina maana unatumia million 30 kulisha umati alaf ukitoka hapo maisha yanakushinda
 
Nani anekuchangisha humu, nani anakulazimisha ?
 
Kiukweli inakera sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…