Michango ya harusi imekua kero kwangu, mbona mimi sikuchangisha mtu ata senti moja

Michango ya harusi imekua kero kwangu, mbona mimi sikuchangisha mtu ata senti moja

sahihi.

mdogo wangu alinibana kwenye sherehe yake, ikabidi nitenge saa nzima la kumpatia elimu. alieelewa ama hakuelewa atajua mwenyewe!

kama mtu anataka ufahari wa dunia hii akamsujudie ibilisi, ataupata! kuna haya ma-secret societies mengi ya kisheitwani, ila hatima yake atakuja kujua kuwa hajui.

Mathayo 4 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
⁸ Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mlima mrefu mno, akamwonyesha milki zote za ulimwengu, na fahari yake,
⁹ akamwambia, Haya yote nitakupa, ukianguka kunisujudia.
Baada ya somo na bado hukutoa vile vile mkuu hahaa
 
20241002_181246.jpg
 
Mi hapa Nina kadi 14 na ni kwahii oct mpaka dec, hata sijui nafanyaje..shida ni watu wa karibu mno hata pakuchomokea hupaoni!
Wee ndo tunaelewana sasa ni watu mnaheshimiana huwezi kuwakazia kibandidu

😂😂 sema 14 kazi unayo mkuu
Mnaogopa nini kumuambia mtu hauko vizuri? Ukitoa Tshs. 100k kwa watu 14 ni Tshs. 1.4M ndani ya miezi miwili, hii ni pesa nyingi sana hata kama una mfuko mpana kui-flush toilet just for sake of social conformity. Binafsi huwa sichangii shughuli za sherehe kama harusi.
 
Habari za kuchakarika wakuu,

Aisee hapa navyoandika nimeungwa kwenye magroup matatu ya harusi zinazokuja mwisho wa mwaka huu, 1 ni binti ndugu wa ukoo sio immediate family link kwa mababu huko, mmoja ni jamaa nilitinga nae job kabla sijahamia nilipo, mwingine jamaa tumesoma wote high school.

Me nilioa harusi ya kiislam very simple hawakuzidi watu 200 hv vyakula ilikua chai ya maziwa, tende, sambusa, kabab, cookies, kuku za kukaanga na juice za azam embe vichupa vidogo na maji vichupa vidogo na watu wote walikula na kubeba , eneo nyumba ya ndugu yake wife (hatukutaka ukumbi), kwa kifupi nilitoa 2M tu kufanikisha shughuli + mapambo, usafiri.

Kusema ukweli ukiangalia vzuri sku hz watu wanatumia michango kutafuta mitaji or else mana haiwezekani eti unaweka kiwango cha chini labda 100,000/=

Unakuta mtu hamjaongea kitambo hakuna ukaribu unashangaa simu imeita unapewa taarifa! punde umeungwa kwenye group watu wametiririka ma plege.

Mwezi uliopita kuna jamaa mwngine aliniunga kwenye group pledge kiwango cha chini 200,000 nikamwambia me ntakusupport laki akasema poa ila nilibanwa nikatuma 50k nikamwambia ingne ntamalizia. Asee simu zkawa za usumbufu nikawa simpokelei hadi sku naona status kaoa nikampa hongera akanilia buyu blue tick tu. Nikaja kuonana nae town ananipa attitude nkasema safi ndo imeisha hiyo ila najuta ata kwann nlituma 50 yani unamaind kisa sina? Na muda huo najua kabisa washkaji wetu wengine kweny hiyo circle hawakutoa kabisa.

Wadau mnaonaje hv inakuaje u force michango hivyo kwa jambo linalokuhusu ww na huyo mwenzio kwann utuwajibishe watu kutoa ma ahadi ya kishingo upande imradi tu tusigombane wakati hali yenyewe mambo kizungumkuti songombingo mafrekeche ya kutosha.

Kama hujajipanga kuoa si kausha kwanza, watu tuna support ila imekua too much imekua ni shuruti sasa dah, usipotoa unaonekana mbinafsi na haufungamani na jamii.

Sijioni nikiendelea kua mtoa michango sijioni kabisa kwanza in real sense nakuchangia kwenda kukojozana kwenye hotel honeymoon uko... Shabaash,!!
Piga chini. Nmeenda kikao cha harusi familia imepnaga budget milion 25 halafu eti wao wanatoa milion 2 kama familia.
Vijana wanaenda teketeza hyo pesa wakati anayeoa anapanga chumba kimoja
 
Mimi binafsi kwa vila najiwezi angalau natoa kwa sababu hata kama sipendi , kuna ile leo na kesho ...Kama unach obasi toa maana bado tunawasiliana na marafiki zetu ambao tulikuwa na nyakati nzuri huko nyuma .

Utafutaji wa maisha unakutana na watu wengi sana , kuanzia shule ya msingi mpaka chuo ..
 
Plan yangu ya kuoa nimepanga watakao hudhuria harusi yangu ni wazazi wangu na ndugu watatu, wazazi wa mwanamke na ndugu zake 10 hakuna kuomba michango, wala hakuna habari za mziki na kukodisha kumbi za sherehe ndoa inafungwa Asubuhi hadi saa 12 kila mtu anarudi kwake.
Unakua muweka hazina, muhasibu, MC mdogo wako basi.
 
Back
Top Bottom