Michango ya harusi imekua kero kwangu, mbona mimi sikuchangisha mtu ata senti moja

Na siku hizi kuna wapuuzi wanaomba hadi michango ya graduation, vipaimara sijui na Birthday. Shenzi kabisa sijui sherehe zao huwa ni dharula au wanahisi ni kitu flani cha lazima mtu kutoa.

Mwingine hujawasiliana naye zaidi ya miaka 3 ukiona simu inaita unawaza hapa kama sio mchango sijuiunakuta kweli anaomba mchango anaoa. Wadau wanazingua sanaa.
 
Imagine mchango wa kipaimara, upuuzi tu bora tuonekane mabandidu
 
Juzi tu hapa kuna jirani kafanya shughuli ya kufungua saluni yake, kachangisha watu na walienda na wakamzawadia!

Siku hizi michango kama hii ni biashara tu. Kuna hadi vikundi vya kuchangishana na kupeana zawadi.

Tuigeni kwa wenzetu waliopiga hatua kimaendeleo. Ukiwa na shughuli yako alika watu kadhaa hakuna michango wala nini
 
Ya kwangu nilifanya hivi mpaka leo amani ndugu wanabaki wakishangaa tu hawazubutu kunisumbua kuchanga
 
Wenzetu walishatoka huko ,nasi tutafika tu kwenye ndoa za mikataba na harusi pasipo michango.

Kiukweli kama unataka kuoa ni vyema wewe muoaji na muolewaji kujipanga ,unaandaa watu wa kuwaalika majirani,ndugu ,jamaa na marafiki tu ambao ukipiga list yote hawazidi hata 200.

Sasa bajeti ya kulisha watu 200 mpaka utembeze bakuli? Kujipanga kwa 6m mwaka mzima hutashindwa? Kama sherehe tu unachangisha watu vipi kurun familia ,ujenzi ,ada za watoto nazo utachangisha maana hizo ndiyo kubwa kuliko hata gharama za harusi.

Tuondoe mentality ya kwamba lazima harusi uchangiwe....Nakubaliana na Mwana FA alivyosema kwamba yeye achangii harusi ya mtu yeyote.
 
Yote hii ni kutaka kuiga kunya kwa tembo kupasuka msamba.
Fanyeni mambo kwa uwezo wenu. Hata chupa ya soda tu kwa waalikwa wa karibu inatosha na utaanza maisha bila stress
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…