Michango ya harusi imekua kero kwangu, mbona mimi sikuchangisha mtu ata senti moja

Siku nyingine usijichoshe kuanzisha uzi. Unatulia na kuendelea na harakati zingine tu.
 
Kama mama yako mzazi bado yupo hai, hio mipango yako, isahau, mama zetu wa kiafrika ndo huwa Wana shughuli, utaona wageni hao siku ya harusi hata huwafahamu wewe kazi yako kupokea zawadi na kuwashika mikonoπŸ˜ƒπŸ˜ƒ

Haya ni maneno ya wengi wanaopenda sherehe kusingizia mama zao.

Majizo mama yake yupo hai. Na lulu mama yake yupo hai. Ila hawajafanya sherehe kubwa ya kuitaji michango.

Millard ayo mama yake yupo hai ila hajafanya sherehe kubwa ya kuitaji michango.
 
Moja ya kanuni zangu za kuishi kwa furaha ni kwamba huwa sichangii harusi, send off, au birthday. Na ukileta kadi nakuambia hapo hapo kuwa "MIMI HUWA SICHANGII SHEREHE ZA HARUSI, SEND OFF NA BIRTHDAY". Hili limenisaidia kuishi kwa amani na imesaidia kuwa na marafiki wachache.
 
Kwanza kumpigia mtu kudai mchango siwezi, hizo harusi ni kutafuta uhasama tu usio na misingi yoyote.
 
Na wanapoachana hawatuchangishi kwenda kushangilia kuachana kwao....
 
Mimi huwa nina Msimamo! Kama sina huwa naeleza ukweli tu na wananielewa! Kama ninazo sawa!
Just imagine unapokea kadi ya Harusi kila mwezi au unapokea kadi sita baada ya miezi kadhaa kwa pamoja! Unafanyaje?
Usipoangalia Kadi za Harusi ni PEPO LA UMASIKINI!
 
MICHango ya harusi ni uchawi na roho mbaya tu ya kimaskini...kwa nini tusichangishane kufanya harambee za kupeleka mwanafunzi ulaya kuusoma,,,kwa nini tusichangishane mtoto wa flani kamaliza degree tumchangie mtaji afungue biashara yake.... tumchangie ajenge kiwanda chake...tuchange tuje tulewe kwa kujumuika na kuonyeshana umevaaje...
 
Michango imekuwa shida sana kuna mwana grupo la kazini alikuwa anataka kuoa basi ile michango watu wamesha pledge kila kitu ila kila muda anarudia mkeka. Basi bwana si nikamchana kuwa atulie tushaona mkeka tutachanga. Kumbe raia wengine walikuwa wanakereka sana lakin hawasemi ila baada ya kuanzisha hivyo ndio wakajitokeza.

Ila michango imekuwa mingi sana ila ni kutokana na tecnlojia ya whatspp na Instagram hii

Mwanzoni zilikuwa hazipo hizo ilikuwa ngumu kutafutana na kupeana info.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…