Michango ya Harusi Single 100,000 na Dabo 150,000, watu wanaumia kimoyomoyo!

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2016
Posts
17,434
Reaction score
27,177
Vijana wa kisasa, anasoma chuo, akifika mtaani anataka kuoa, hapo hajapata kazi, anaanza kusumbua watu wote wa phone boook yake. Kijana huyo, anataka harusi sawa na mtoto wa GSM, anaishia kupata sress na kugombana na ndugu, swali, je hawa vijana wanastahili kulaimisha kadi za double?

Michango ya harusi imekuwa mada yenye mjadala mkubwa, ambapo viwango vya Tsh. 150,000 kwa mtu mmoja (single) na Tsh. 200,000 kwa wawili (double) vinaonekana vimekaa vizuri kiuchumi. Kiwango hiki kinasaidia sana kufidia gharama halisi za ukumbi, mapambo, na chakula bora kwenye sherehe za kisasa, huku kikiwapunguzia mzigo mkubwa waandaji.

Hata hivyo, ili kuondoa manung'uniko, ni muhimu kadi hizi zitolewe kwa kuzingatia uwezo wa kiuchumi wa waalikwa na ukaribu wao na maharusi, kwani kwa baadhi ya watu kiwango cha single kinaweza kuwa kikubwa kikilinganishwa na kile cha double.

Kuhusu suala la kula mpaka hela iishe na kubeba vyakula, utaratibu huo hauwezekani na unakinzana na maadili pamoja na maana halisi ya mchango wa harusi. Mchango wa harusi si malipo ya kununua chakula kama mgahawani, bali ni sadaka na zawadi ya upendo kwa ajili ya kufanikisha mwanzo mpya wa maisha ya wanandoa. Kwenye sherehe, chakula huandaliwa kwa kiwango maalumu cha kutosha kila mgeni aliyepo, hivyo kitendo cha mtu mmoja kula kupita kiasi au kufungasha vyakula vya kubeba (takeaway) huwanyima wengine haki yao na kuleta usumbufu mkubwa kwa waandaaji.​
 
Vijana wa kisasa, anasoma chuo , akifika mtaani anataka kuoa, hapo hajapata kazi, annaza kusumbua watu wote wa phone boook yke. Kijana huyo , anataka harusi sawa na mtoto wa GSM, anaishia kupata sress na kugombana na ndugu, swali, je hawa vijana wanastahili kulaimisha kadi za double?

Michango ya harusi imekuwa mada yenye mjadala mkubwa, ambapo viwango vya Tsh 150,000 kwa mtu mmoja (single) na Tsh 200,000 kwa wawili (double) vinaonekana vimekaa vizuri kiuchumi. Kiwango hiki kinasaidia sana kufidia gharama halisi za ukumbi, mapambo, na chakula bora kwenye sherehe za kisasa, huku kikiwapunguzia mzigo mkubwa waandaji.

Huwa najiuliza mtu anayetaka kuoa halafu hajajipanga anategemea michango ili afanikishe harusi yake ,ni upuuzi.

Ukitaka kuoa atleast uwe na bajeti 90% kutoka kwako ,kama harusi bajeti milioni 10 basi Bwanaharusi uwe na 9m ,hiyo 1m ni kutoka kwa wadau wako wa karibu ,ukishakamilisha 100% unawapa kadi watu ambao unataka wahudhurie regardless hata kama hawajachanga.

Kama unataka kuoa halafu unategemea karibu 99% michango basi hiyo ndoa haitotoboa hata miezi 6 maana ukishamaliza harusi unabaki na madeni ,na hao "HAWA" kuishi na mwanamme suruali ni ngumu.
 
Vijana wa kisasa, anasoma chuo , akifika mtaani anataka kuoa, hapo hajapata kazi, annaza kusumbua watu wote wa phone boook yke. Kijana huyo , anataka harusi sawa na mtoto wa GSM, anaishia kupata sress na kugombana na ndugu, swali, je hawa vijana wanastahili kulaimisha kadi za double?

Michango ya harusi imekuwa mada yenye mjadala mkubwa, ambapo viwango vya Tsh 150,000 kwa mtu mmoja (single) na Tsh 200,000 kwa wawili (double) vinaonekana vimekaa vizuri kiuchumi. Kiwango hiki kinasaidia sana kufidia gharama halisi za ukumbi, mapambo, na chakula bora kwenye sherehe za kisasa, huku kikiwapunguzia mzigo mkubwa waandaji.

Hata hivyo, ili kuondoa manung'uniko, ni muhimu kadi hizi zitolewe kwa kuzingatia uwezo wa kiuchumi wa waalikwa na ukaribu wao na maharusi, kwani kwa baadhi ya watu kiwango cha single kinaweza kuwa kikubwa kikilinganishwa na kile cha double.

Kuhusu suala la kula mpaka hela iishe na kubeba vyakula, utaratibu huo hauwezekani na unakinzana na maadili pamoja na maana halisi ya mchango wa harusi. Mchango wa harusi si malipo ya kununua chakula kama mgahawani, bali ni sadaka na zawadi ya upendo kwa ajili ya kufanikisha mwanzo mpya wa maisha ya wanandoa. Kwenye sherehe, chakula huandaliwa kwa kiwango maalumu cha kutosha kila mgeni aliyepo, hivyo kitendo cha mtu mmoja kula kupita kiasi au kufungasha vyakula vya kubeba (takeaway) huwanyima wengine haki yao na kuleta usumbufu mkubwa kwa waandaaji.​
Nasema hivi, mimi nikiwa na akili timamu SICHANGII NDOA YA MTU,
Tena nipo na staff zangu wanajua kabisa, nachochatoa ni kwa issue ya MARADHI ambayo kimsingi anahitaji surport yetu, takuwa mstari wa mbele kumpigania mpambanaji mwenzangu apone ili aendelee na majukumu maana maisha yanahitaji uimara wa afya, ujinga wote uliobaki SITOI HATA MIA, na kama ikinibidi sana sina namna mchango wangu hauzidi elfu 20,over,
 
Hayo mamichango ya harusi sijui maujinga gani sitoi pesa yangu yaaan !

Msiba, ugonjwa ndo nachangia tu !

Starehe yako uje usumbue watu, mtu eti kisa mmesoma wote, mmepotezana 10+yrs anakuadd kwenye grp anataka mchango..... ujinga huu
 
Wewe mtu anapanga harusi ya milioni 50 na honeymoon Dubai, kisha anategemea marafiki ndio wachange hiyo fedha, daah!
anaanza kuwapostia akila bata na kununua vitu vya gharma huko dubai.
Bila kuacha kuchanga huu ujinga hautakoma.

Ronaldo na Utajiri wake ameamua kufanya sherehe ya watu 8 ,huna pesa Utegemee za nani?
 
Huku kwetu tunaishi kijamaa sana , mchango mkubwa sana ni 30k tena mnakula public sio ndani ya maukumbi kama jela . Wakuja wanaleta hizi tabia za kusumbua watu , inachukiza sana ; watu wanaombaomba michango kuliko hata yatima .
 
Mimi natoa mchango wa msiba, kuumwa na ada tu

Mchango wa kuchangia watu kwenda kuhalalisha sexual intercourse kwa misingi ya dini za kuletewa sitoi hata mia

Adam na Hawa nani aliwafungisha ndoa?
Hii ndio michango tuombwe pamoja na madawati ya Watoto sio ujinga mwingine
 
Mnategemea mke wangu asibond wigi la maana kweli? Nguo kwa Anna collection, make up kwa Glossy parlour, kiatu, kwa Beatrice trend shoez, accessories Pete ofisi zipo makumbusho hapo .....

Hapo ni km milion sita
 
Back
Top Bottom