Michango ya Harusi Single 100,000 na Dabo 150,000, watu wanaumia kimoyomoyo!

Michango ya Harusi Single 100,000 na Dabo 150,000, watu wanaumia kimoyomoyo!

Wajuba nimepewa kadi nyingi za michango ya harusi na nimeingizwa kamatini bila kuombwa. Nafikiria nitoe kiasi gani nusu, robo au nisitoe kabisa. Nisipotoa nitaeleweka vibaya kuwa sina ushirikiano
Bora usieleweke
 
Nafikiri ni jukumu la mtoaji Kusema dhahiri kuwa sitaweza kutoa, kukubali kujumuishwa au kutoa ahadi ya mchango wa harusi si Jambo la kiume ikiwa ww hupendelei kutoa mchango...Kama unaogopa basi usitoe ahadi yoyote Ile, maana wanasema kuwa sometimes bongo bila unafiki mambo hayaendi
 
Watu wanalalamika kwa usumbufu wenu wa kutuma meseji na kupiga simu kukumbushia michango. Kama unajua ni hiari kwa nini usumbue watu kukumbusha?
Harusi sio dharura jipange kwa kipato chako na sio kusumbua watu.
UShawahi kuona mtu anaomba mchango mtu wa mbali yake

Mtu akimiomba mchango kama siko karibu nae namwambia hapana

Iko simple sana.
 
Vijana wa kisasa, anasoma chuo, akifika mtaani anataka kuoa, hapo hajapata kazi, anaanza kusumbua watu wote wa phone boook yake. Kijana huyo, anataka harusi sawa na mtoto wa GSM, anaishia kupata sress na kugombana na ndugu, swali, je hawa vijana wanastahili kulaimisha kadi za double?

Michango ya harusi imekuwa mada yenye mjadala mkubwa, ambapo viwango vya Tsh. 150,000 kwa mtu mmoja (single) na Tsh. 200,000 kwa wawili (double) vinaonekana vimekaa vizuri kiuchumi. Kiwango hiki kinasaidia sana kufidia gharama halisi za ukumbi, mapambo, na chakula bora kwenye sherehe za kisasa, huku kikiwapunguzia mzigo mkubwa waandaji.

Hata hivyo, ili kuondoa manung'uniko, ni muhimu kadi hizi zitolewe kwa kuzingatia uwezo wa kiuchumi wa waalikwa na ukaribu wao na maharusi, kwani kwa baadhi ya watu kiwango cha single kinaweza kuwa kikubwa kikilinganishwa na kile cha double.

Kuhusu suala la kula mpaka hela iishe na kubeba vyakula, utaratibu huo hauwezekani na unakinzana na maadili pamoja na maana halisi ya mchango wa harusi. Mchango wa harusi si malipo ya kununua chakula kama mgahawani, bali ni sadaka na zawadi ya upendo kwa ajili ya kufanikisha mwanzo mpya wa maisha ya wanandoa. Kwenye sherehe, chakula huandaliwa kwa kiwango maalumu cha kutosha kila mgeni aliyepo, hivyo kitendo cha mtu mmoja kula kupita kiasi au kufungasha vyakula vya kubeba (takeaway) huwanyima wengine haki yao na kuleta usumbufu mkubwa kwa waandaaji.​
Imekuwa too much
 
Ukisikia Tanzania ni nchi ya kijamaa tafsiri yake ndio hii.
Isipokuwa ujamii wa enzi za mwalimu ulikuwa sio wa hiari.
Ujamaa wa kileo ni wa hiari.
Ukisema leo ujiandalie harusi yako kwa fedha zako mwenyewe, pengine kwa nia njema kabisa.....Kamati wewe, kila kitu wewe, kisha ualike watu bure.......hupati watu.......watu hawaji........
Kuna hisia kwamba wanaenda kujidharirisha..............Usipoenda vilioni ni hufungwi........ila utapitishwa kwenye misukosuko mikali.
Kusalimia watu sio lazima.
Ila sasa...
 
Ukihoji utaambiwa huna hela ni kapuku, utaambulia matusi ya rejareja. Huu upuuzi wa michango ya harusi ni fasheni tu, huko nyuma haikuwepo na watu waliooa bila kuchangisha watu. Kwa nini unaoa kwa kutegemea mifuko ya watu? Huu ni usumbufu, kwani bila michango ndoa haifunwi? Fanya harusi kwa bajeji yako
Kwani unalazimishwa kutoa?
 
Mnategemea mke wangu asibond wigi la maana kweli? Nguo kwa Anna collection, make up kwa Glossy parlour, kiatu, kwa Beatrice trend shoez, accessories Pete ofisi zipo makumbusho hapo .....

Hapo ni km milion sita
Yote haya unategemea kutoka kwenye mifuko ya watu? Makubwa , mweee!
 
Imewahi kukutokea au unasema tu?
tatizo unaishi dunia ambayo unataka mambo yawe kama unavyoona wewe

Ina maana umri wangu huu unadhani sijawahi kuchangia harusi au

Sisi tunaotokea kaskazini haya mambo tunayaona kawaida sana

Waswahili wanaona maajabu

Jibu changa au usichangia hakuna anayekushikia panga
 
Hizi harusi za michango waachiwe matajiri wachangiane kufanya sherehe zao za kifahari. Makapuku kuigaiga utamaduni huu ni vituko na vioja. Cha ajabu ndoa zenyewe hazidumu kwa makapuku huku umewakwangua wenzako visenti vyao. Peleka ndoa kwa mchungaji kanisani/kwa sheikh msikitini hakatai kufunga, rudi homu na mkeo bila mwembwe na nderemo kula ugali wako lala, kesho nenda kwenye mishe zako maisha yaendelee
Hii nakubali mkuu👍
 
Back
Top Bottom