Jaji Mfawidhi
JF-Expert Member
- Feb 20, 2016
- 17,434
- 27,177
- Thread starter
- #41
Umeua, gawana furaha na marafiki!
Umeua, gawana furaha na marafiki!
Wazaramo hawachangi zaidi ya buku ten.wanaangaliaga na watu wa kuwashinikiza
point, ngoja wanaume waje .Mtu unaoa, ndio ijulikane kuwa unaenda kuichapa? Hayo ni mambo ya faraghani yaishie huko huko faraghani Mungu ni shahidi kuwa umeoa, usisumbue watu wakuchangie, jibebe mwenyewe ndio inavyotakiwa
Kwa sasa ni uhuni tu mana hata chakula na vinywaji vya ukumbini haviendani na ukubwa wa michango. Ukitaka kunufaika na mivhango uwe mwanakamati pesa yako itarudiKumambuzi, kwenye michango ya harusi kumekuwa na visa, vitimbi na vioja vingi sana *****! Kuna watu wameigeuza ni sehemu ya kupigia kujipatia fedha kufanyia mambo yao mengine. Wanakamati si watu wazuri nao huambulia mgao kama bakshishi yao wakati wanavunja kamati. Kuna dogo alikuwa mtunza fedha huku yeye ndiye muoaji, alipoo michango imenona akaghairi kufunga ndoa kanisani akaenda kufungia bomani kukwepa matumizi makubwa ya fedha. Michango akaigeuza kuwa mtaji wa kuanzisha duka. Kuna bodaboda mmoja yeye kakabidhiwa michango ya harusi yake akaichezea kamari na sasa anapigiwa simu aeleze mpango wa harusi yake hapokei simu. Mwingine aligawa kadi achangiwe na akachangiwa, harusi ilipokaribia akapiga kimya na kudai michango haikufikia lengo kwa bajeti yake, hajarudisha hela za watu, akaanzisha mradi wa kukopesha watu. Anakopesha kwa riba kuanzia buku tano, buku ten, mbau, hamsini, laki na sasa kaanzisha kakikundi chake cha VICOBA
Tatizo watu hawabadiliki wala kujifunza na kwenda na wakati. Mbaya zaidi events hizi ni kutafuta lawama tu Kwa watu; mbaya zaidi utaambiwa 'TAFUTA HELA, ACHA MAKASIRIKO' au 'HUJALAZIMISHWA KUCHANGIA'.Huwa najiuliza mtu anayetaka kuoa halafu hajajipanga anategemea michango ili afanikishe harusi yake ,ni upuuzi.
Ukitaka kuoa atleast uwe na bajeti 90% kutoka kwako ,kama harusi bajeti milioni 10 basi Bwanaharusi uwe na 9m ,hiyo 1m ni kutoka kwa wadau wako wa karibu ,ukishakamilisha 100% unawapa kadi watu ambao unataka wahudhurie regardless hata kama hawajachanga.
Kama unataka kuoa halafu unategemea karibu 99% michango basi hiyo ndoa haitotoboa hata miezi 6 maana ukishamaliza harusi unabaki na madeni ,na hao "HAWA" kuishi na mwanamme suruali ni ngumu.
tena chakula kimekuwa kikipelea, mbaya zaidi ni usiku wa manane ukale wapi? Wanadai kuna waalikwa wamekuja na watoto wao ambao hawakuwepo kwenye bajeti ya chakulaKwa sasa ni uhuni tu mana hata chakula na vinywaji vya ukumbini haviendani na ukubwa wa michango. Ukitaka kunufaika na mivhango uwe mwanakamati pesa yako itarudi
Ndiyo maana NDOA zinavunjika sana ,watu wanakurupuka.Tatizo watu hawabadiliki wala kujifunza na kwenda na wakati. Mbaya zaidi events hizi ni kutafuta lawama tu Kwa watu; mbaya zaidi utaambiwa 'TAFUTA HELA, ACHA MAKASIRIKO' au 'HUJALAZIMISHWA KUCHANGIA'.
Watu wanalalamika kwa usumbufu wenu wa kutuma meseji na kupiga simu kukumbushia michango. Kama unajua ni hiari kwa nini usumbue watu kukumbusha?Unalalamikaje wakati kuchanga ni jambo la hiari
Ukisoma comment unapata picha flani huku JF watu wengi ni masikini sana.
150,000/- sio hela ya kulalamika wala kuja kuitolea maelezo mtandaoni
TUtafute hela
Huwa najiuliza mtu anayetaka kuoa halafu hajajipanga anategemea michango ili afanikishe harusi yake ,ni upuuzi.
Ukitaka kuoa atleast uwe na bajeti 90% kutoka kwako ,kama harusi bajeti milioni 10 basi Bwanaharusi uwe na 9m ,hiyo 1m ni kutoka kwa wadau wako wa karibu ,ukishakamilisha 100% unawapa kadi watu ambao unataka wahudhurie regardless hata kama hawajachanga.
Kama unataka kuoa halafu unategemea karibu 99% michango basi hiyo ndoa haitotoboa hata miezi 6 maana ukishamaliza harusi unabaki na madeni ,na hao "HAWA" kuishi na mwanamme suruali ni
Mimi naona michango ya harusi isiwekewe kiwango maalumu cha kuchangia.kila mtu achange kutokana na uwezo wake, maana siyo kila mchangiaji ana haja ya kuja kula siku ya harusi yako.Vijana wa kisasa, anasoma chuo, akifika mtaani anataka kuoa, hapo hajapata kazi, anaanza kusumbua watu wote wa phone boook yake. Kijana huyo, anataka harusi sawa na mtoto wa GSM, anaishia kupata sress na kugombana na ndugu, swali, je hawa vijana wanastahili kulaimisha kadi za double?
Michango ya harusi imekuwa mada yenye mjadala mkubwa, ambapo viwango vya Tsh. 150,000 kwa mtu mmoja (single) na Tsh. 200,000 kwa wawili (double) vinaonekana vimekaa vizuri kiuchumi. Kiwango hiki kinasaidia sana kufidia gharama halisi za ukumbi, mapambo, na chakula bora kwenye sherehe za kisasa, huku kikiwapunguzia mzigo mkubwa waandaji.
Hata hivyo, ili kuondoa manung'uniko, ni muhimu kadi hizi zitolewe kwa kuzingatia uwezo wa kiuchumi wa waalikwa na ukaribu wao na maharusi, kwani kwa baadhi ya watu kiwango cha single kinaweza kuwa kikubwa kikilinganishwa na kile cha double.
Kuhusu suala la kula mpaka hela iishe na kubeba vyakula, utaratibu huo hauwezekani na unakinzana na maadili pamoja na maana halisi ya mchango wa harusi. Mchango wa harusi si malipo ya kununua chakula kama mgahawani, bali ni sadaka na zawadi ya upendo kwa ajili ya kufanikisha mwanzo mpya wa maisha ya wanandoa. Kwenye sherehe, chakula huandaliwa kwa kiwango maalumu cha kutosha kila mgeni aliyepo, hivyo kitendo cha mtu mmoja kula kupita kiasi au kufungasha vyakula vya kubeba (takeaway) huwanyima wengine haki yao na kuleta usumbufu mkubwa kwa waandaaji.
Ni sisi sisi ila ni kashesheMbona Kila mtu anasema hachangi.. sasa Hawa wanaochanga ni kina nani 🥹🥹🥹
GoodMimi natoa mchango wa msiba, kuumwa na ada tu
Mchango wa kuchangia watu kwenda kuhalalisha sexual intercourse kwa misingi ya dini za kuletewa sitoi hata mia
Adam na Hawa nani aliwafungisha ndoa?