Michango ya Harusi Single 100,000 na Dabo 150,000, watu wanaumia kimoyomoyo!

Kwa sasa ni uhuni tu mana hata chakula na vinywaji vya ukumbini haviendani na ukubwa wa michango. Ukitaka kunufaika na mivhango uwe mwanakamati pesa yako itarudi
 
Tatizo watu hawabadiliki wala kujifunza na kwenda na wakati. Mbaya zaidi events hizi ni kutafuta lawama tu Kwa watu; mbaya zaidi utaambiwa 'TAFUTA HELA, ACHA MAKASIRIKO' au 'HUJALAZIMISHWA KUCHANGIA'.
 
Kwa sasa ni uhuni tu mana hata chakula na vinywaji vya ukumbini haviendani na ukubwa wa michango. Ukitaka kunufaika na mivhango uwe mwanakamati pesa yako itarudi
tena chakula kimekuwa kikipelea, mbaya zaidi ni usiku wa manane ukale wapi? Wanadai kuna waalikwa wamekuja na watoto wao ambao hawakuwepo kwenye bajeti ya chakula
 
Kuna waalikwa walilalamika kulishwa chakula kisichoshibisha vema. Walilishwa mikaango ya chipsi, maayonaizi, ndizi na vifinyango vya nyama. Wao walitaka wali/pilau wale mpaka matumbo yakaze wakaambiwa wali/pilau ni mtindo wa chakula ulipitwa na wakati kama ugali na makande harusini. Walilamika michango yao hawakuifaidi vema
 
Wajuba nimepewa kadi nyingi za michango ya harusi na nimeingizwa kamatini bila kuombwa. Nafikiria nitoe kiasi gani nusu, robo au nisitoe kabisa. Nisipotoa nitaeleweka vibaya kuwa sina ushirikiano
 
Ninachojua mchango ni hiari, na mtu huchanga kile anachowiwa. Sichangi kwa kupangiwa kamwe.
 
Tatizo watu hawabadiliki wala kujifunza na kwenda na wakati. Mbaya zaidi events hizi ni kutafuta lawama tu Kwa watu; mbaya zaidi utaambiwa 'TAFUTA HELA, ACHA MAKASIRIKO' au 'HUJALAZIMISHWA KUCHANGIA'.
Ndiyo maana NDOA zinavunjika sana ,watu wanakurupuka.
 
Unalalamikaje wakati kuchanga ni jambo la hiari

Ukisoma comment unapata picha flani huku JF watu wengi ni masikini sana.

150,000/- sio hela ya kulalamika wala kuja kuitolea maelezo mtandaoni

TUtafute hela
Watu wanalalamika kwa usumbufu wenu wa kutuma meseji na kupiga simu kukumbushia michango. Kama unajua ni hiari kwa nini usumbue watu kukumbusha?
Harusi sio dharura jipange kwa kipato chako na sio kusumbua watu.
 

Mimi naona michango ya harusi isiwekewe kiwango maalumu cha kuchangia.kila mtu achange kutokana na uwezo wake, maana siyo kila mchangiaji ana haja ya kuja kula siku ya harusi yako.
Watu wengi wanachanga kwasababu unahitaji support ili kufanikisha jambo lako,wala siyo haja ya kula.
Mtu akitoa mchango wa laki 1.5/2 kwaajili ya kula,halafu aje ale mlo mmoja huwo ni wizi wa 5G.
 
Mimi natoa mchango wa msiba, kuumwa na ada tu

Mchango wa kuchangia watu kwenda kuhalalisha sexual intercourse kwa misingi ya dini za kuletewa sitoi hata mia

Adam na Hawa nani aliwafungisha ndoa?
Good
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…