Michango ya Harusi Single 100,000 na Dabo 150,000, watu wanaumia kimoyomoyo!

Wajuba nimepewa kadi nyingi za michango ya harusi na nimeingizwa kamatini bila kuombwa. Nafikiria nitoe kiasi gani nusu, robo au nisitoe kabisa. Nisipotoa nitaeleweka vibaya kuwa sina ushirikiano
Bora usieleweke
 
Nafikiri ni jukumu la mtoaji Kusema dhahiri kuwa sitaweza kutoa, kukubali kujumuishwa au kutoa ahadi ya mchango wa harusi si Jambo la kiume ikiwa ww hupendelei kutoa mchango...Kama unaogopa basi usitoe ahadi yoyote Ile, maana wanasema kuwa sometimes bongo bila unafiki mambo hayaendi
 
Watu wanalalamika kwa usumbufu wenu wa kutuma meseji na kupiga simu kukumbushia michango. Kama unajua ni hiari kwa nini usumbue watu kukumbusha?
Harusi sio dharura jipange kwa kipato chako na sio kusumbua watu.
UShawahi kuona mtu anaomba mchango mtu wa mbali yake

Mtu akimiomba mchango kama siko karibu nae namwambia hapana

Iko simple sana.
 
Imekuwa too much
 
Ukisikia Tanzania ni nchi ya kijamaa tafsiri yake ndio hii.
Isipokuwa ujamii wa enzi za mwalimu ulikuwa sio wa hiari.
Ujamaa wa kileo ni wa hiari.
Ukisema leo ujiandalie harusi yako kwa fedha zako mwenyewe, pengine kwa nia njema kabisa.....Kamati wewe, kila kitu wewe, kisha ualike watu bure.......hupati watu.......watu hawaji........
Kuna hisia kwamba wanaenda kujidharirisha..............Usipoenda vilioni ni hufungwi........ila utapitishwa kwenye misukosuko mikali.
Kusalimia watu sio lazima.
Ila sasa...
 
Kwani unalazimishwa kutoa?
 
Bila kuacha kuchanga huu ujinga hautakoma.

Ronaldo na Utajiri wake ameamua kufanya sherehe ya watu 8 ,huna pesa Utegemee za nani?
kwahiyo, anayetaka mambo ya kifahari na michango ajipange mwenyewe?
 
Mnategemea mke wangu asibond wigi la maana kweli? Nguo kwa Anna collection, make up kwa Glossy parlour, kiatu, kwa Beatrice trend shoez, accessories Pete ofisi zipo makumbusho hapo .....

Hapo ni km milion sita
Yote haya unategemea kutoka kwenye mifuko ya watu? Makubwa , mweee!
 
Imewahi kukutokea au unasema tu?
tatizo unaishi dunia ambayo unataka mambo yawe kama unavyoona wewe

Ina maana umri wangu huu unadhani sijawahi kuchangia harusi au

Sisi tunaotokea kaskazini haya mambo tunayaona kawaida sana

Waswahili wanaona maajabu

Jibu changa au usichangia hakuna anayekushikia panga
 
Hii nakubali mkuu👍
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…