Michango ya ujenzi wa shule sio lazima, wilaya ya Hai Kingereka mnatia aibu

Michango ya ujenzi wa shule sio lazima, wilaya ya Hai Kingereka mnatia aibu

Mung Chris

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2017
Posts
3,474
Reaction score
4,007
Kuna watu wanapita kuchangisha fedha sh.5,200 kwa ajili ya ujenzi wa shule ya kingereka ndani ya wilaya ya Hai sehemu inaitwa kingereka jirani na mlima Kingereka walipopita ni nyumba zilizopo jirani na kanisa la wasabato. Hivi kama sijakosea Waziri wa Elimu si alisema watajenga madarasa?

Hawa watu wanasema ni lazima kutoa na ni amri sio ombi kama umetoa onyesha risiti, tunataka kujua tuna serikali ya mtaa ya kimabavu au niya ki-amri au ni amri kutoka serikali kuu. muda huu wamepita wamekuwa wakali sana.

Niseme hivi CCM mjitathmini huu uongozi sio uongozi wanao utaka wananchi nafahamu viongozi waliopo huko wanakodai fedha hizo sio wa vyama pinzani hata Halmashauri tafadhalini tuacheni wananchi tupumue sh 5,200 sio hela ndogo na hamuwezi kuomba kwa lazima na iwe amri maana maisha ya juzi sio ya leo.

Kama kuna viongozi ambao hawaja watuma hawa kuchangisha kwa lazima tafadhali shughulikieni swala hili haraka imekuwa kero wanazungukia kila nyumba na kila mpangaji.
 
Back
Top Bottom