Punchlines geto la msela
Karibu geto usijisumbue kuvua viatu mlangoni, we timba nalo mpaka ndani kama vile chooni.../
Karibuni masela na wahuni wote
SupperVillain hadi
Mvumbo, silaha za kijadi nyuma ya mlango nondo shoka na nyundo.../
Geto kuchafu unasikia harufu ya uvundo uvundo, vitu haviko kwenye mpangilio mzuri minguo ipo lundo lundo.../
Unanicheki kwa jicho la kuonesha umekasirika unakuta mi nimesizi, unaomba maji ya kunywa nakupa unakuta yamejaa sisimizi.../
Geto ni full joto hakuna kiyoyozi, wanatimba masela sijawahi leta totozi.../
Nikianza kufagia kama upo ndani utapata kikohozi, geto la kigumu nachukiwa mtaani nafananishwa na walozi.../
Mlangoni hua sina kitasa wala komeo, natumia kimsumari nabado sijawahi kuibiwa mpaka leo.../