Michano/Hiphop/Freestyle

Michano/Hiphop/Freestyle

Wapo wapi watoto ndembe ndembe, au wameunga mkono juhudi?/
Wamekubali Mvumbo ni kimbembe, kwenye hii thread vipi watarudi/
Nimeshawapiga za chembe, hawaponi kwa sindano wala udi/
Nimewafukuza kama Membe, wanatoa jicho kama Kabudi/
Hawarudi ka' moshi wa kaya/ wanagwaya/ Mvumbo ni Vimpire/ natawala himaya/ kama Msoga na Jakaya/ waoga wanapwaya/ nawala kiboga ile mbaya/ nikiumiza ndonga WAYA/
Waambie siogopi, hata waje na hirizi/
Kwenye maji ya magoti, eti wanapiga mbizi/

Sent using Jamii Forums mobile app
 
La kuvunda, halina maabara/
maneno wanaunda, ili nisiwe kinara/
hawajui mi ni punda, nimeuficha mnara/
wakizidi nitawala tunda, ile ile kimasihara/
natema hizi tungo, kama Shaaban Robert/
hata waje na UNGO, bado MPUNGA hawapati/
ukimya una FUNZA, ila chunga watakunyonya kindezi/
hadi maktaba INATUNZA, lakini haitoi penzi/

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanasema Mvumbo unajifanya unajua, mbona mziki neema haukupi/
Wenzako wanabana pua, zaidi ya dera kwenye chupi/
Hauwezi kutusua, wenzako wanavaa Gucci/
Kuna kitu haujajua, tafuta dem mpige picha za uchi/
Hapo dunia itakujua, bila Kiki hakukuchi/
Media utasumbua, utawika zaidi ya KUCHI/
Tena imba za kusasambua, ukisifia KUNDUchi/
Nawajibu Hip Hop INANITAMBUA, kabla sijazijua papuchi/

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sisemi nimethibitisha, ila ni habari toka vyanzo huru/
American wamekinukisha, Amani imekuwa lulu/
Bongo Corona imekwisha, kama alivyosema Mkulu/
Upinzani viongozi wanakwisha, kuunga juhudi za Ikulu/
Bongo life bado tafu, na maisha ni mafupi/
Using'atwe na siafu, kwa kushikilia chupi/
 
Siasa ni mchezo halamu chunga usimfunze mwanao, msie ashike sana elimu Maana vyeo na siasa vilimuua farao/

Wako nyuma wanatuweka mstari wa mbele tutumike kama ngao, ili wakubalike wanataka sisi tufe ili dunia nzima ipate mshangao/

Corona si tishio bali tishio ni watu, sambaza taarifa za uongo mtaani kumezagaa wafu/

Utamaduni wa ulaghai sio asili ya mbantu, na hili tumehaswa kitambo tangu enzi za mababu/
 
Flow zao za kitoto acha niwapitishe maji ya magoti/
Maana natema mashairi ya moto kama mdomo una hot pot/
Wanapita bea kama Mpoto wanaiogopa hii post/
Sichekeshi kama Mboto ila hii show mi ndo na host/
Mvumbo nipo mbele hii game naimudu/
Media Mc's wanapiga kelele ka' Vairas Mdudu/
Hadhira inapiga vigelele kwa kulishwa mashudu/
Watangazaji wanataka mchele ndio ngoma waihusudu/
 
Huu uzi ulikuwa wapi mbona sikuuona mapema/
Ngoja mhuni nivute mic maana nina mengi ya kusema/
Niwachane bila huruma mi sio yule said mwema/
Wewe rapa legelege jiandae kulala pema/
Unatamba mainstream sio, mi home jf/
Ila usi'battle na mimi mwana 'coz utabeba F/
Mistari inanyoosha rula mhuni nanyoosha kambi/
'Coz nikiwa high natoa rhymes za kila rangi/
 
Nipo jana na leo kama sanamu posta/
Nikikamata kipaza huwa sifanyi makosa/
Nachana ngumu, niite kitukuu cha ngosha/
The swaga don, kama ni mpunga we dondosha/
We vuta sigara mi navuta mkwanja/
Ila sitokuchangia siku ukianza kubanja/
Eti unaniita hommie, hommie unipe homa!/
Paka majivu usoni kisha kalale kwa sangoma/
 
Amkeni weka shuka pembeni, navyoskika kwa spika namficha mpaka ndugai bungeni.../

Nikichana nawakera kama aliyekosa kazi kwasababu ya foleni, hawanifikii kwa vina wako chini mi niko juu kileleni.../

Rap bila mi ni ka kutegemea kupata uji bila maji, mi na huu mziki tuko benefit ka biashara na mtaji.../

Huko kwenu naskia trappers mnawaita wachanaji, huku tumeshikilia misingi ndo maana huwezi kuwaona wazugaji.../

Msanii wenu anavaa heleni afu pua kaitoboa, insta ana like picha za mashoga na machangudoa.../

Mvheki alivyoshombe kalegeza sauti mpaka inaboa, hali inatisha mtoto wa kiume anaombwa jicho na anatoa.../
 
Ma mcee nawapiga guu la shingo wamedata hawapumui, waliotumwa ku battle wamefyata ka jibwa lililokumbana na chui.../

Wanauliza mbona unasikika japo ngoma zako hawanunui, nabaki kucheka ka mtoto kaoneshwa katuni za futuhi.../

Scars ndo nani huyu rapa mbona hatumjui, mi ni kama kifo ulipo nipo naweza kukubeba hata kama huugui.../

Taifa la rap afu mi ndo raisi, ikulu ni booth katiba yetu ni verse.../

Ndani ya hili taifa ukiimba bongo fleva unasomewa kesi, ni hatari zaidi ka utawala wa magu afu ufumwe na denti.../

Njoo bungeni uone vinasa kila meza, spika ndo deejay kila ngoma ya mbunge anaicheza.../
 
Japo ukoko nimepata kwenye jungu kuu lakini siachi kukokoa, yeah korona imeisha mniga bado navaa barakoa.../

Japo upo kwenye siku zako ila ukinivalia mini naichojoa, kwenye chaka la wahuni bishoo na hiko kipini puani unatuboa.../

Hali tight na ndo maana pesa imekua ngumu kutoa, so sistaduu ukishoboka ntakuchapa sitajali japo nina ndoa.../
 
Vina vyangu viko deep ka packing ya meli, wenye mtumbwi huku hawafiki engine zao zitafeli.../

Nina zutu la kutosha na ndio maana hamnioni sheli, navo flow kibabe unaweza kudhani kafufuka makaveli.../

Niko juu kama tower ya kule babeli, na ndio maana rap yangu iko njema ka imeshushwa na gabriel.../

Kila sekta niko good sijawahi ku-carry, naweza ku flow kiburundi au hadi kingeli.../

Nikishika mic nawalewesha wanasizi kama kuku mwenye kideli, kwa hivi vina acheni niwalainishe zaidi ya ky jelly.../
 
Ma mcee nawapiga guu la shingo wamedata hawapumui, waliotumwa ku battle wamefyata ka jibwa lililokumbana na chui.../

Wanauliza mbona unasikika japo ngoma zako hawanunui, nabaki kucheka ka mtoto kaoneshwa katuni za futuhi.../

Scars ndo nani huyu rapa mbona hatumjui, mi ni kama kifo ulipo nipo naweza kukubeba hata kama huugui.../

Taifa la rap afu mi ndo raisi, ikulu ni booth katiba yetu ni verse.../

Ndani ya hili taifa ukiimba bongo fleva unasomewa kesi, ni hatari zaidi ka utawala wa magu afu ufumwe na denti.../

Njoo bungeni uone vinasa kila meza, spika ndo deejay kila ngoma ya mbunge anaicheza.../
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji119][emoji91][emoji91]
 
Japo ukoko nimepata kwenye jungu kuu lakini siachi kukokoa, yeah korona imeisha mniga bado navaa barakoa.../

Japo upo kwenye siku zako ila ukinivalia mini naichojoa, kwenye chaka la wahuni bishoo na hiko kipini puani unatuboa.../

Hali tight na ndo maana pesa imekua ngumu kutoa, so sistaduu ukishoboka ntakuchapa sitajali japo nina ndoa.../
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Noma kweli [emoji91][emoji91][emoji91]
 
Vina vyangu viko deep ka packing ya meli, wenye mtumbwi huku hawafiki engine zao zitafeli.../

Nina zutu la kutosha na ndio maana hamnioni sheli, navo flow kibabe unaweza kudhani kafufuka makaveli.../

Niko juu kama tower ya kule babeli, na ndio maana rap yangu iko njema ka imeshushwa na gabriel.../

Kila sekta niko good sijawahi ku-carry, naweza ku flow kibudundi au hata ngeli.../

Nikishika mic nawalewesha wanasizi kama kuku mwenye kideli, kwa hivi vina acheni niwalainishe zaidi ya ky jelly.../
Ooooii [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Skiza nikupe adress mahali ninapotokea, mitaa nayokaa wengi tuna exepeience ya kupelekwa segerea.../

Ukiona vijana wanazungumza na hujasikia tusi ujue umepotea, penye wanawake wawili au watatu basi pana msuto au umbea.../

Mabishoo wa huku wengi nguo wanagongea, wakilipuka viwanja hata demu wako akijichengua wanakubebea.../

Giza totoro ka ni bishoo kua makini na chocho, uswazi full vibaka wahuni wanapiga kabali si kitoto/

Wanamafunzo ya karate kungfu hadi taichi, kama ulivaa tai watakukaba nayo hata ukilia hawakuachii.../

jumamosi vigodoro ndo siku mabinti huvaa nusu uchi, wakimwaga radhi we bana zipu kuzuia ashki.../

Mitaa nayotokea sio siri imejaa vurugu, usishangae siku umekuja ukaona doka limejaa mamwela wameshika virungu.../
 
Ooooii [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Yes mkushi niko nyuma ya mic, nasambaza upendo kama mkwepu kwenye batani ya like.../

Niko humu na nyinyi kama chain kwenye bike, kwa hii michano kama kampuni sio metl ni nike.../

Scars anavina vitamu ila ukimuomba hakupi, anavimba sana mwana anabana ka lastic ya chupi.../
 
Punchlines geto la msela

Karibu geto usijisumbue kuvua viatu mlangoni, we timba nalo mpaka ndani kama vile chooni.../

Karibuni masela na wahuni wote SupperVillain hadi Mvumbo, silaha za kijadi nyuma ya mlango nondo shoka na nyundo.../

Geto kuchafu unasikia harufu ya uvundo uvundo, vitu haviko kwenye mpangilio mzuri minguo ipo lundo lundo.../

Unanicheki kwa jicho la kuonesha umekasirika unakuta mi nimesizi, unaomba maji ya kunywa nakupa unakuta yamejaa sisimizi.../

Geto ni full joto hakuna kiyoyozi, wanatimba masela sijawahi leta totozi.../

Nikianza kufagia kama upo ndani utapata kikohozi, geto la kigumu nachukiwa mtaani nafananishwa na walozi.../

Mlangoni hua sina kitasa wala komeo, natumia kimsumari nabado sijawahi kuibiwa mpaka leo.../
 
Skiza nikupe adress mahali ninapotokea, mitaa nayokaa wengi tuna exepeience ya kupelekwa segerea.../

Ukiona vijana wanazungumza na hujasikia tusi ujue umepotea, penye wanawake wawili au watatu basi pana msuto au umbea.../

Mabishoo wa huku wengi nguo wanagongea, wakilipuka viwanja hata demu wako akijichengua wanakubebea.../

Giza totoro ka ni bishoo kua makini na chocho, uswazi full vibaka wahuni wanapiga kabali si kitoto/

Wanamafunzo ya karate kungfu hadi taichi, kama ulivaa tai watakukaba nayo hata ukilia hawakuachii.../

jumamosi vigodoro ndo siku mabinti huvaa nusu uchi, wakimwaga radhi we bana zipu kuzuia ashki.../

Mitaa nayotokea sio siri imejaa vurugu, usishangae siku umekuja ukaona doka limejaa mamwela wameshika virungu.../
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Hii ndio maana hali ya mitaa imetulea [emoji91][emoji91]
 
Back
Top Bottom