Michano/Hiphop/Freestyle

Sina title mi natamba kibishi bila promo, kama denti hana vitini afu ana pass kila somo..../

Mistari ina upako na power ya kukukosha, sioni sababu ya kuiacha na kumfata mwamposa.../
 
Bhagooshaa, nang'aka kistaa kama chibudenga/ nimejaa kila kona, sifa kwangu kwao skendo

Mitaani wamekaa, kapteini nawachabanga/ Kila mechi wakisogea nawaachia vumbi adoado

Sisikii la muadhini wala la mnadi swala/
Dhamira yangu ni kung'aa Dar mpaka Kemondo

Mistari naidondosha ving'asti wanagaragara/ vumbi limewatapakaa si usoni tu mpaka kwa mgongo

Wanachekesha na kuhuzunisha, wanaweza'kuliza/ na mkaksi ndio naanza nawachoma sindano za mkongo

Hala
 
Bado Hip Hop naibeba, kama Ngamia mwenye nundu/

Watoto wanakwenda Leba, wanaponisikia wanapata uchungu/

Life bado ni shega, wananiwangia namwomba Mungu/

Kwenye Love sijalega, nakamatia mtoto KHUMBU/
 
Acha rhymes niendelee, maana mimi ndiye Kuchi/

Wanashangaa kama balehe, aliyeona nyuchi/

Wanapenda starehe, mandinga na pamba za Gucci/

Na mfukoni wako tee, vipi watapinga kuwekwa uchi/
 
Song; HIYO NI CHAI

Chorus;
Jf umekuwa uwanja wa kujidai
Nina majumba na mandinga
Jua hiyo ni chai
Wote matajiri hakuna Mmachinga
Jua hiyo ni chai
Toyota ni chinja chinja nina Benz
Wanajimwambafai
Ukimkuta anaishi kindezi
Hajanywa hata chai

Verse 1

Wengine wanapenda bisha bisha kienyeji/
Hawana fact wala point na wapo Age/
Wengine eti na Passo wana aleji/
Kumbe wanaandika wakiwa kwa shemeji/
Juu ya sofa/ akisubiri dada apewe ofa/
Ili na yeye aondokane na ulofa/
Avae moka/ wengine wanapenda matusi/
Wengine ni Mamajusi/ mademu wengine nuksi/ wameweka Dp za Warusi/
Ukadhani hugusi/ kumbe ni akina Tausi/
Ila poa si wanakwepa majasusi/
Ila mbaya ni kuigiza/ humu unaabudu Jesus/ mtaani unaabudu yai viza/
Upo ubishi wa Siasa na kabumbu/
Zipo anasa za akina KHUMBU/
Warembo wa kisasa wenye nundu/
Wote eti wamepata life la kizungu/
Tamaa usijekata kisa huna fungu/
Hiyo ni chai matata tena ni Mbupu/
 
Huku hakuna maskini kila mtu katusua, we kama wauswazi wenzako wakishua.../

Milo yao ni kwa hotel za kifahari kama hujajua, ukiwa huku ni mwiko kutaja ashua.../

Mademu vimbaumbau huku wamekosa soko, hupewi namba kama humiliki mkoko../

wengi wanaigiza kuficha misoto, hali yetu ya kimaisha imefanya matatizo tuyape kisogo.../

ukiwa real utakosa ushawishi, hutafuatiliwa michango yako hata kama ina teach.../

Njoo uone jf yenye wanachama wenye utashi, kipimo chao cha elimu ni kujua english.../
 
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16] Hiyo ni chaiii. Aminiaa kabisaa [emoji2935]
 
[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28] hatari sana hii chai.
 
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]
 
Mvumbo nilipotea kwa muda, kabla ya msiba wa Mkulu/
Nikabaki kwenye ushuhuda, mpaka Mama anaingia Ikulu/

Makundi yakachuja, nini asali wakasifu sukari guru/
Jina wakalifuja, ili Bimkubwa awanusuru/

Siasa ni ukuda, watakutukana waliokuona lulu/
Namuombea Bimkubwa, makundi yasije mdhuru/

Kwenye game nimeona wakuja, mara Paula mara mikono mvululu/
Nikasema huu ndio muda, wa game kuinusuru/

Hawana adabu mara kuku na vifaranga/
Mara makushabu mara tembo kwenye banda/
Picha za ajabu na mambo ya kwenye kitanda/
Majibizano ya Taarabu wote hawataki kusanda/

Pumbavu nawaonya, nahubiri kama Pastor/
Heshima nitawapokonya, zaidi ya yule RC mtata/
Rudini kunyonya, kabla sijawapiga mbata/
Wengine mziki unatuponya, hivyo acheni kudata/
 
Najaribu..

Mi sio mc japo nawasha ka pilipili
Na tuzo ya fasihi toka kidato cha pili
Nawahukumu wasonitii niite pilato wa pili
Laiti ngezaliwa chato sahii ngekuwa waziri

Ningekuwa na gari sita ferrari na Benz
Hata DJ sinyorita angeshanipa penzi
Madem wenye saasita kutoka bara na zenji
Ngewavuta kama shisha yaan full ushenzi

Ngoja nisiiandike sana maana bado najaribu
Ngechana kingereza sema kwa wengine tabu
Na nikichana kifaransa watahisi n kiarabu
Basi naishia hapa maana sifanyi taarabu
 
Walidhani nimekata ringi, kisa jukwaani sisomeki.../

Kumbe mchizi nilikua mtaani nazidaka shilingi, shazipata sasa unaye nidai njoo unicheki.../

Mko wapi warembo wakali, leo nina kisu njoo mnichune.../

Mnifanyie masaji, na hicho kitambi mkikune.../

Nina mipango kabambe ya kufungua miradi, Nimkalishe baharesa mpaka haters wanune.../
 
Najivunia kuwa mtanzania, amani na upendo ndo nguzo kubwa tunajivunia.../

Wako wapi wakoloni na pupa walizokujia?, Umewatupa wako mbali wamekukimbia.../

Rest in peace john, nina mengi ya kusema kama nakudiss sorry.../

Naskia ume fight, umekuza uchumi hadi sasa tupo wakati.../

Elimu bure na shule hazina madawati, mtaani pesa hakuna ulikaza nati.../

Waajiriwa uliwawekea ugumu kwenye posho, mtwara nao wanalia eti uliwadhulumu korosho.../

Ulipendwa sana ukapewa kura za kishindo, ukapewa promo utawale milele mpaka pale maisha yako yakifika ukingo.../

Ulipenda sifa kila msanii alikutungia nyimbo, ukaweka mtego waliokupinga walinasa kwenye huo ulimbo.../

Ulipo wadaka ulihakikisha jamii haijui walipo, japo wapo waliookotwa kwenye mifuko kando ya mito.../

Bado hakuna aliyethubutu kufungua mdomo, Wengi walihofia maisha yao yangefikia ukomo..../

Ulitudanganya Ndege zinaingiza kipato, tukaamini ukaendelea kajenga kiwanja kingine chato.../

Siasa za haki na uhuru uliziweka kando, wasiolipa ushuru ulio wabambikiza waliwekwa lupango.../

Napenda amani ndo mana natangaza upendo, ukipenda haki utakumbukwa ukiumaliza mwendo.../
 
Neema...

Neema ukija ghetto usije kama Vanessa
Alienipa mchecheto na kuacha nimedisa
Nkaishia kupiga nyeto huku nakodolea picha
Alinikera kama meko yule jiwe mpenda sifa

Tena Neema ukinipa usinipe ka resituta
Kiuno kata katika na usichoke kuzungusha
Usiige ya ughaibuni kikubwa punguza pupa
Sitaki kwa mparange siwazagi kuruka ukuta

Tafadhali tena neema usije fanya ya rejina
Alipenda kugawa jicho wakapasua retina
Jikubali umbo lako usitamani ya mchina
Tusije kua na mgogoro ka zena na betina.!
 
Chelu natema vina vya moto, cheche zake ni disaster/
Nabeba maono tuliza mshono ewe bastard/
Nakupa neno la haki usikaze fuvu Damn I’m a pastor/
Japo nina sura laini but I’m a motherfuckin’ gangster/

Subira inavuta heri, mimi navuta ganja/
Na-meditate ile time wewe unaruka kwanja/
Sitafuti papuchi, natafuta mkwanja/
So, hata nikimgonga Uwoya sitojiona Dogo Janja/
 
Neema,

Nilikupenda ulikua mwema, uzuri wako ulikua gumzo kila mtu alisema.../

Nikakuweka moyoni ukawa chanda chema, ukaahidi kua nami na kuwaacha manyangema.../

Tumetoka mbali halafu mwisho umenitema, Ziko wapi ahadi zako kama sio sinema?../

Naskia umepata kibopa tabata, ana mpunga kila utakacho muomba unapata.../

Kitandani ulikua mvivu sikukuponda nkakuacha, naskia huko unakatika nyonga matata.../

Umekua mtundu hadi bomba unalamba, umemkosha ngosha asione noma mkwanja kukata.../

Wakati pesa imeondoka utakurejea utashi, utagundua ulinusa moshi ukidhani marashi.../

Utavuna maradhi, haijalishi unauzuri gani ila utashuka hadhi.../

Pesa ya kodi ikikata utakosa hifadhi, najua utapagawa ila usije kuniomba radhi.../

Neema
 

Neema

Nilikupenda, nikakulinda, nikakutunza nikakujali/
Nikaamini wewe ni mwenzangu wa safari/
Nikajipa hamasa ya kuzichanga dorali/
Kumbe mwenzangu hukunipenda, na umenitupa kikatili/

Sasa hivi nakuona unazurura tu kwa mtaa/
Sometimes unashinda na kulala baa/
Na wahuni wamegongesha besela/
Na sasa umegeuka kuwa demu wa masela/

Neema yaani unatoa papuchi ka’ sadaka/
Chini ya miti, hadi kwenye vichaka/
Wanaopanda dau hadi nyuma unawapa/
Neema unafukuliwa mtaro, damn, what the fvck/
 
Mpaka napanga hivi vina, nasikia umechina, unatanga tanga/

Maisha sio pina, yamekuzidi kina, unakesha kwa waganga/

Yuko wapi mtu wako wa China, si ulijiona winner, ukanipanga/

Kidume nipo sharo tina tina, cha kukusaidia sina, rabda ungo uende kuwanga/

Neema ulikuwa na neema gani?, mbona kwangu sikuiona/

Una cheat unasema samahani, na kesho unagawa huku naona/

Nashukuru sijashika gun, nimeruhusu wabaya wangu kupona/

Sikutaka niondoke uraiani, japo moyoni ilinichoma/

Ulikuwa na Waarabu, ulikuwa na wahindi/

Ulikuwa na vibabu, ulikuwa na wenye vigimbi/

Hadi wavuta makushabu, nao walipiga pindi/

Nimekuacha kistaarabu, na leo mimi ndiye mshindi/
 
Sitapasahau mbalizi...

Kule songwe viwandani palinipa pesa kede
Mademu walijigonga ka shilole kwa uchebe
Wengine walinizonga eti niwavishe pete
Niliishia kuwagonga halafu wakala mateke

Mi ni wakala wa kete na ganja za arachuga
Waulize wapiga debe wa ubungo na buzuruga
Mitonyo mikwanja tele mingi si ya kuzuga
Ndo ilinipa kiburi hadi mbalizi nkavuruga

Nilipata demu soja ngoja niwape stori
Ni kama aliniroga nkasahau kwenda pori
Mtoto anakata nyoga bila uoga wala ngori
Kwa mizuka ye haifai ni ka Masai mwenye mori

Nilidata na ye akanasa akanihonga ATM
Na anavonya donga ka fisadi wa CCM
Wazungu wakanitoka kwa mlipuko kama bom
Kitanda kikawa vita zaidi ya boko haram

Aisee to cut a story now we have two kids
Na hii n true story wazee na wala sio fix
Yaan nimeoa mjeda mbalizi bila blade price!
Hakika sitapasahau hata nihamie Paris![/b]
 
Oyoooooooh
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…