Yahaya haujulikani unapokaa, na unapenda sifa kwa mademu/
Unawadanganya una chapaa, ili wakupe gemu/
Pochi limejaa, kumbe ni ma ATM mpaka ya marehemu/
Umeokota kwenye mitaa, ili mradi upewe ile sehemu/
Mademu shazi, na unakunywa za Kireno/
Hautaki kazi, maana unauza maneno/
Usione paja wazi, unacheza kama Arsenal/
Acha ubazazi, wana watakung'oa meno/
Unaishi kifala, halafu unadanganya ni Jasusi/
Unapanda dala dala, eti unapeleka ma file White House/
Daily upo arosto/ maisha ya ndoto/ sound kwa watoto/ unatoa boko/ unawapelekea moto/ kisha unajisifia tuu/
Unaikimbia mikopo/ unadanganya una mjengo Boko/ kumbe life goto/ acha uchoko/ mafanikio hayapo katikati ya miguu/
Mitaani umekuwa dhalili, ufanyayo haturidhiki/
Ila ndiyo hivyo una akili mbili, kama tyre za Pikipiki/