Michano/Hiphop/Freestyle

Michano/Hiphop/Freestyle

Nina mistari isiyokwisha, mi mgodi wa madini/

Wanasema natisha, kama sikukuu ya Halloween/

Nawavuta kama Shisha, mi ndio Master wa hii dizain/

So hawawezi nitisha, hata wakiwa kombaini/

Nipo juu kama Sky, hii ni kabla ya Dai, na watoto wanaoji mwambafai/

Wanao Try waambie Mvumbo hafai, atarusha mawe juu ya mayai/

Nimewazidi mzani, yaani vina mpaka dhambi/

Mvumbo ni mwembe wa uwani, nyani hatambi/
 
Mashairi yangu ni vinu vya Tehran, nikitema ni maafa/

Ninapotimba haina samahani, mbishi kama Kayafa/

Mkongwe ka' Marijani, ndio maana watoto wanasafa/

Mvumbo namba one, mnae mtegemea kafa/

Bado nipo shega, nawawangia wanga/

Wananisaka kama masega, ila nimejipanga/

Wenye uchungu wende Leba, kidume nishatia nanga/

HIP HOP naibeba, zaidi kapu la muuza karanga/
 
Niite mwamba natamba/
Kwa hii michano, Kibindoni nina gamba/
Akili kubwa kifua mbele najigamba/
Mungu fundi bhana kanipa mistari leo natamba/
Mc's fake Jf washashtuka nmewabamba../
Natamani niseme kila kitu,
Ila koo langu ni kama lina kutu/
Cha mapinduzi mmewakaba pinzani hivi hamna Utu??/
Mjini siku hizi hamna kitu, si bora ndiende shamba nkafuge kuku!
 
Yahaya haujulikani unapokaa, na unapenda sifa kwa mademu/

Unawadanganya una chapaa, ili wakupe gemu/

Pochi limejaa, kumbe ni ma ATM mpaka ya marehemu/

Umeokota kwenye mitaa, ili mradi upewe ile sehemu/

Mademu shazi, na unakunywa za Kireno/

Hautaki kazi, maana unauza maneno/

Usione paja wazi, unacheza kama Arsenal/

Acha ubazazi, wana watakung'oa meno/

Unaishi kifala, halafu unadanganya ni Jasusi/

Unapanda dala dala, eti unapeleka ma file White House/

Daily upo arosto/ maisha ya ndoto/ sound kwa watoto/ unatoa boko/ unawapelekea moto/ kisha unajisifia tuu/

Unaikimbia mikopo/ unadanganya una mjengo Boko/ kumbe life goto/ acha uchoko/ mafanikio hayapo katikati ya miguu/

Mitaani umekuwa dhalili, ufanyayo haturidhiki/

Ila ndiyo hivyo una akili mbili, kama tyre za Pikipiki/

IMG_20210427_000003_136.jpg
 
Dawasco wanakata maji, mi nakata ngebe/

Wachawi wanaupiga mtaji, mi napiga za Uchebe/

Wako wapi wajuaji, wamesepa wanacheza rede/

Nishapiga tisa 'Manyota inchaji', na bado nipo dede

Haina shanapa, maujuzi toka kitambo/

Mc's nawachapa, zaidi ya Commando ya Rambo/

Haina tambo haina majigambo, ila ukweli ndio ninaosema/

Wanaandika vijambo, nafanya mambo 16 Bars kila nnapohema/

Mitaa imenipa heshima, sipagawi na chuki za kiwaki/

Nacheka madogo wanapopima, hawana meno wanataka mswaki/

Nawaandikia Rappers kisha wanakwenda mjini/

Baadae wanajiona bora eti kuliko mimi/

Benson Moto hauzimi, nakata vilimi/

Niamini siku hizi hawapimi/

Nishatengwa na warembo, kama BUTI lakuchumpa/

Siku nachinja tu tembo, sio bata life ni supa/
 
Haipoi hii speed, nimewazidi wanagwaya/

Mkaidi hafaidi, mpaka siku ya Eid SABAYA/

Harakati kama Mugabe, wanapaswa kuniita Baba/

Sio mpaka vibao niwazabe, ndio m Like bara saba/

Maujuzi yanajieleza, wapuuzi hawataweza/

Makuzi na kujikweza, Mwamuzi kishanipendekeza/

Wananisoma kimoyo moyo, kama jarida la ngono kwa mzazi/

Madogo ni vibogoyo, mswaki wa Rhymes kwao hauna kazi/
 
Mvumbo kwenye Mdundo ni fumbo kwa mafala/

Hizi tungo ni kumbo zipo rundo maabara/

Naandika zaidi ya mwalimu wa Hisabati/

Natandika hata ungekuwa Goriati/

Nawika hata bila kutumia Mkuyati/

Nasifika bila dundo kwenye chati/

Wanga wameufyata, ka' wamevaa barakoa/

Ona wanashuka fasta, ka' chupi ya changudoa/
 
Mvumbo kwenye Mdundo ni fumbo kwa mafala/

Hizi tungo ni kumbo zipo rundo maabara/

Naandika zaidi ya mwalimu wa Hisabati/

Natandika hata ungekuwa Goriati/

Nawika hata bila kutumia Mkuyati/

Nasifika bila dundo kwenye chati/

Wanga wameufyata, ka' wamevaa barakoa/

Ona wanashuka fasta, ka' chupi ya changudoa/
Changudoa, nipe penzi staki ndoa.../
Nguo chojoa, Njoo unichune kisu nishaki noa../

Maisha hayana mbinu ni sanda kalawe, nani alijua niki ataiongoza kisalawe.../
Mliokosa uteuzi acheni mpagawe, Kama hamjaona msosi siku nyingine msinawe../
 
Chelu sina time na marapa wateketeke,
Nawabinya kama funza kisha nasukuma kete,
Nishashika rungu niite komredi kipepe,
So chagua moja, nikugonge ama nikuchomeke,
 
Leo nishawasha mambo, dah! akili haipo sawa/

Kichwa kipo kama pambo, maana nime smoke dawa/

Nawaza Simba ingefanya jambo, kumsajili Mpili mzee wa Power/

Au Mwijaku wa majigambo, angekuwa msemaji wa Yanga aache uchawa/

Mmakonde mjeshi Rambo, kule Tax na yeye si angeleta ngarawa/

Au tu wanamtoa chambo, Simba aweze kumnawa/

Agh! Naona mengi mambo, ambayo kama hayapo sawa/

Yule Jesus wa VIJAMBO, hivi hana kipawa?/

Mbona anaendekeza michambo, wakati Corona inauwa wazawa/

Mvumbo nipo moto kitambo/ zaidi ya birika la kahawa/

Naishia hapa japo nipo mtambo, ila vina vichafu kama chawa/

20210616_204032.jpg
 
Mvumbo kwenye Mdundo ni fumbo kwa mafala/

Hizi tungo ni kumbo zipo rundo maabara/

Naandika zaidi ya mwalimu wa Hisabati/

Natandika hata ungekuwa Goriati/

Nawika hata bila kutumia Mkuyati/

Nasifika bila dundo kwenye chati/

Wanga wameufyata, ka' wamevaa barakoa/

Ona wanashuka fasta, ka' chupi ya changudoa/
Hiyo bar ya mwisho balaaa sana
 
Bado napambana, niwe maridadi wa makazi usafiri na nguo/

Mvumbo siku hizi nachana, kama nimemeza shanuo/

Masnitch nawashukuru sana, kwa maarifa zaidi ya elimu ya chuo/

Siku hizi hawawezi nibana, hawajiamini ka' wamevaa mpasuo/

Kitambo nipo town, kama Carina tako la Nyani/

Pisi nishawavua sana gauni, ila siku hizi ya kazi gani/

Nikitema rhymes mpo down, Mvumbo ni namba wani/

Na msiponivisha Crown, nitavishwa hata na wasio na imani/

Nyendo zangu unaefuatia, eti kisa napendwa na akina Khumbu/

Jua mengi nilivumilia, zaidi ya mfuko wa p*mbu/
 
Kila Verse ni majanga, kama risasi za Korosso/

Haina kujipanga, hii sio Charanga za Mbosso/

Kama huwezi hizi mbanga, ya nini kuwanga bora uvae Soso/

Mvumbo ni kisanga, kitambo natamba kama viatu vya Losso/

Nakata ngebe, walevi wanakata supu/

Sipigi tena za Uchebe, napiga za Mbupu/
JamiiForums1120482783.jpg
 
Niite Mzee Mpili, maana Jamii Forums nina watu/

Ukinikosa jukwaa hili, nipo uzi wa warembo wanaoshika safu/

Chit chat kwangu sio dili, maana wana mambo machafu/

Habari mchanganyiko siwezi subiri, japo kila muda habari za wafu/

Mauaji yamekithiri, mara moto mara risasi za mapafu/

Kule MAHUSIANO sio shwari, kutwa kuwaponda madem halafu/

Ndio hao hao wanaanzisha habari, Pm kwa watoto wa watu/

Kule SIASA ni mabishano makali, usiwaamini hata washike Msahafu/

Na nimeshaizoea hii hali, JF kila mtu ana Sarafu/
 
Bado nipo yechu siachi gape, mpaka nitakapo ritaya/

Tatizo taarifa zetu mnaziuliza kwa adui zetu, ndio maana mnatuona wabaya/

Ndio maana ukinitazama, uso wa mbuzi uso wa dagaa/

Na siogopi lawama, kama tinga tinga la Manispaa/

Haina kujuana, kama nimeingia Barreta Bar/

Kufahamiana sana, ndio mwanzo wa dharau kwenye mitaa/

Bora nipambane isini cost, nikaishi kindezi/

Mmachame choma noti, usimchome mpenzi/
 
Back
Top Bottom