Michano/Hiphop/Freestyle

Aliesema bongo bahati mbaya apewe kret la safari maana aliona mbali../
Nchi imepwaya kila sekta, maskini hawana hali wanashindia ugali na kachumbali../
Hakuna michongo wala ajira, vijana wanafilisika kwa kamari/
Rais kapagawa taifa lipo chini ya utawala wa uza madawa../
Tumekubali tuna vuna tulichopanda, ila tayari wingu limetanda 2025 tumejipanga kwa mapigano/
 
Alikuwa ni mtu wa church, hapo ndio nikajua kumpata itakuwa kazi.../

Nilikuwa tayari kwa lolote nimpate, miondoko yake na upole vilinifanya nidate.../

Siku moja alikuwa anakatiza sokoni, nikamfata kumueleza namna alivyonikaa moyoni.../

Akashangaa akauliza kwani kulikoni, unanipenda mimi kwani wengine huwaoni?.../

Nikamwambia mama usiwe na hofu, nakupenda wewe wengine siwaoni nimekuwa mpofu.../

Basi nikamjaza maneno kumpa hope, maana nishachoka daily kutumia soap.../

Akanipa namba tukaaza kuchart, kesho kutwa nikamualika club ku party.../

Akasema hiyo ni dhambi mi nimeokoka, lakini dingi pia ni mkali nikisepa atafoka.../

Nikamuambia we ni nguzo ukiacha nita dondoka, sitaki uwende mbali maisha ya upweke nimechoka.../

Lakini haikusaidia maana aliniaga kuwa anaondoka, anaenda mkoa wa mbali kusoma.../

Akaniahidi kunipa ushirikiano every day, lakini alivyosepa simu zangu akawa hapokei.../

Sometimes akipokea ananikalipia, kuwa nimekuwa kero ameshindwa kunivumilia.../

Nimpe muda nipunguze simu kumpigia, atanitafuta kwa muda wake yeye akisikia.../

Aliambia mengi ya kuudhi, aliniambia nitafute demu mwingine sinabudi.../

Masta nikasema huo ni ushenzi, vipo vya kuhangaikia ila sio mapenzi.../

Nikaacha kutuma meseji, hata nikituma nikawa simuiti baby.../

Kuviziana ndio ikawa mbinu, kila mmoja anamsikilizia mwenzake apige simu.../

Sio siri ilikuwa ni zaidi ya mafarakano, ilipita miezi sita bila mawasiliano.../
 
Hatukutafutana, kila mtu kivyake hakuna kujuana.../

Japo kupitia whatsap niliziona status, mara nyingine anipige vijembe mpaka basi.../

Kuna siku moja alipost nikaona dalili, kuwa tayari kashapata bwana wapili.../

Sikutaka kuumiza kichwa, kwani kila siku alikuwa akipost picha.../

Status ziliwekwa maneno ya nyodo, eti chini ya mnazi kaokota dodo.../

Sikuwa na wivu nilimuacha atambe, alisema ana date na wasomi sio waliokimbia umande.../

Mwanzo alianza kumuita class mate, na kuwa wamefaulu na kupata the same grade.../

Hajui mi kwake nishafunga gate, hata anitambie vipi haniumizi head.../

Akapost eti walokole wakidate, hawapaswi kuitana baby.../

Akamtag na jamaa kimafumbo, akampa sifa za mambo lundo.../

Siku zikapita, upepo ukabadilika.../

Status sa huzuni zikaongezeka, kuonesha kwenye hilo penzi anateseka.../

Zile status za kejeli zilikoma, kuonesha hata yeye namba anaisoma.../
 
Fanya kumpotezea, ukomae na msoto/
Maisha ni safari haziishi changamoto/

Unapovunjwa Moyo unaujenga tena/
Usiweke chuki acha iondoke na iende Vyema/
 
Fanya kumpotezea, ukomae na msoto/
Maisha ni safari haziishi changamoto/

Unapovunjwa Moyo unaujenga tena/
Usiweke chuki acha iondoke na iende Vyema/
Unanipa faraja najiskia furaha mno, navyoona ukitoa ushauri kwa mistari ya uno.../

Kiukweli sina chuki, japo moyoni kaniachia jeraha la mkuki.../

Nasonga mbele ya nyuma sikumbuki, alijidai mlokole kumbe mamluki.../
 
Unanipa faraja najiskia furaha mno, navyoona ukitoa ushauri kwa mistari ya uno.../

Kiukweli sina chuki, japo moyoni kaniachia jeraha la mkuki.../

Nasonga mbele ya nyuma sikumbuki, alijidai mlokole kumbe mamluki.../
Wanasema hakuna mapenzi bila pesa, japo wenye nazo nao wanateswa../
We ni mtu mzima yakupasa kulinda heshima uliyoiweka kabla hujazeeka../
Mapenzi ni hisia anae kuchukia ipo siku atakulialia, ndio maana hata Biblia inatuhasa kuvumilia../
Kuna muda wa kucheka na kulia, ila tambua hakuna jipya chini ya jua na hiyo ndio dunia../
 
Kama mapenzi pesa, basi hiyo ni biashara.../

Kwanini wasiifanye kwa kukopesha, au wanaogopa hasara?.../

Juzi Kwenye TV kuna habari walionesha, mapenzi yalimuua tajiri kwa presha.../

Hata wenye pesa ndoa zao nyingi zina vilaka, nani alitegemea mke wa bilgate kudai talaka?.../
 
Naitwa makovu a.k.a machata, kichwani sina dread afu peace zaid ya marasta.../

Usinipeleke kule hapa ndio napo pataka, pana msosi kibao si unajua leo pasaka.../

Weka amila kiumuke kikando, kwa mkapa tujumuike kumzomea orlando.../

Hii ni mission ya wana appolo, Simba atashinda hata wakinuna utopolo.../
 
Naanza kukuchana kwa kusema "Mazafaka",

Umenikera sana na story za Pasaka,

Wengine tumefunga Swaumu joo amka,

Usidhani kila mtu ni Kafiri ma'fakaa,

Mechi yenyewe shenzi mnaingiza siasa,

Eti Kinana mgemi rasmi, Mazafaka?
 
Sasa muda unaruhusu, Mvumbo nizame Tongwe/
Sio mistari ya Mbususu, bali nionyeshe ukongwe/
Chorus nimuweke Zuchu, nifanye mazingaombwe/
Halafu kichupa na nusu, misuti kama Jongwe/
Midevu kama Zuzu/ nionyeshe nimefuzu/ kwenye hii kitu/
Situmii nguvu/ nang'ata fuvu/ kama Mbwa Mwitu/
Niandike kuhusu Wajuzi, walioshika Power/
Wanaodhani Bongo Movie, itaweka mifuko sawa/
Au niandike kuhusu wapuuzi, wanaojiita chawa/
Wanaoleta makuzi, na wasanii kuwagawa/
Ila bora nifiche kombe, siku hizi game ya kiwaki/
Wanapenda za pombe, sio za kiharakati/
Rabda uwahonge, na utupie swagga kati/
Bila hivyo mwenye Ng'ombe, ndiye atakae ongezewa Samaki/
 
Niko jf kitambo nazidi peruzi mambo, humu kuna watu HUMBLE pia wapo wagumu kama migambo /
Bila kusahau wazee wa majigambo kina billioneo Lugano, wanatupa story za nga'mbo pamoja na mifano /tunaishi kwa umoja na muungano /
Hapa ni jf sio fb wala twitter, tuko huru kutoa taarifa kikubwa ziwe za uhakika/
info zinamwagika na hakuna wakututisha,
 
Heshima kwako yuda,kumbe nawe wayajua./
Nilifikiri na wewe kada,maisha umetusua/
Kitaa kimekaa eda,et vita imetuumbua/
wasema Ukraine shida,bei juu umegundua?/
Mafuta kwa oda,tutaweza sie wakishua?/
Eti tungoje muda,wengine tumedondokea pua/
 
Heshima hamkunipa/ mtalipa/ hata iweje/

Mvumbo Sniper/ napiga za kichwa/ kama Mzee wa Mjegeje/

Moto tippa/ mambo yanajipa/ so pandisha mlege/

Mademu wananipa/ kisha nakipa/ buti la Jeje/

Sijawahi kuwa fala/ sababu ya Mitaa ninayotoka/

Naijua Dala/ na inarudi ikiondoka/

Nipo imara/ kama natumia Ngoka/

Na ukinipiga ngwara/ wewe ndio utadondoka/

Litapigwa kila goti/ uwe Padre au malaya/

Ila haifanyi tusijikoki/ kuzisaka ile mbaya/

Wema haukunipa sapoti/ ndio maana nimeugwaya/

Mimi nahesabu noti/ wewe hesabu mabaya/
 
Wananijua nikishikwa na gadhabu, naweza flow mpaka kizigua au kiarabu/
Mademu wa Dar hawana maajabu, usoni wanajichubua halafu wanavaa ijab/
Hakuna wa kushangaa maana wote tunatambua maisha mahesabu/
 
MARA 1 KWA MWAKA challenge

Kuna vingi navifanya hata bila utata, nikikosa mboga nakula panya hadi siku ya pasaka.../

Huku ukiona tumejazana ujue kinawaka, hakuna mambo ya kusemana-semana/ maana kukutana ni mara moja kwa mwaka/

Kwetu tunapenda umoja marufuku matabaka, jenga hoja acha vioja kama mtu aliedata/

Jf kuna pisikali ila ni ngumu kuzipata, bila shari natongoza mpaka wife wa askari kisha namchakata/

Marapa wengi hawafai couse verse zao zimechacha, hawana mistari thats why wanapga show mara moja kwa mwaka.../
 
Sichagui Mbususu, na wala sina matabaka/

Kama ya mke wa mtu, nachakata mara moja kwa mwaka/

Kwa changudoa sijitusu, maradhi na mashaka/

Na danguro likinihusu, ni mara moja kwa mwaka/

Mc's wanachana nusu nusu, wakigundua nipo hapa/

Kuwakilisha nitawaruhusu, mara moja kwa mwaka/

Nyuki huwezi kum'busu, japo asali unaitaka/

Hivyo Ex kumywea Al kasusu, mara moja kwa mwaka
 
Mara moja kwa mwaka huwa nashinda jamvini na wana-board, tunajadili kuhusu vibaka wa mjini na ongezeko la panya-road.../

Wao wanakaa kando ya feli na matausi kibao, hawaelewi kinachofanyika kule sheli ni matusi kwao.../

Mara moko kwa mwaka huwa nakata tamaa, utelezi ukiwa adimu natumia jamaa.../
 
Leo nawachapa, Ng'ombe nawaswaga kama Mgogo/

Haina kutapa tapa, wala kuleta zogo/

Namuona 2pac anawaka, Mvumbo usiwaachie madogo/

Namjibu tayari nipo hapa, naiwakilisha Hip Hop Logo/

Nawapanga kwa safu, kama natumia Hirizi/

Mistari yangu michafu, kama kwapa la Chizi/

Sitabiriki halafu, naibuka tu kama usingizi/

Na hii ni Chafu tatu, kama Karata za Mwizi/

Cheza uliwe ukashitaki, ukatie tie huruma/

Dunia haina haki, hata sana ukijituma/

Utanikuta nimetamalaki, nakurudisha nyuma/

Na ukijifanya hutaki, natupa jiwe Fatuma/
 
Kama kawa kama dawa, haina kupwaya naweza freestlye hata kwa biti za kwaya/
Maticha wenu wote wanagwaya, wakiniona kitasa maguire/kwenye game niko level za eminem/ sema bongo bahati mbaya/
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…