Mvumbo
JF-Expert Member
- Aug 20, 2015
- 3,489
- 12,137
- Thread starter
-
- #461
Jengo linang'aa kama theluji/
Humo ukikaa jina halichuji/
Hakuna dagaa wala kunywa uji/
Ni chapaa na wanasema hawafuji/
Sio haramu/ japo wengine huingia kwa damu/ fahamu/ ni zamu kwa zamu/
Kalamu/ ya mwenye awamu/ ndio huamua hatamu/ tulie au tutabasamu/
Africa nabaki/ japo ndio kunasifika kukosa haki/
Wengine Ikulu wakifika kutoka hawataki/
Mpaka watakapo aibika, maandamano kutamalaki/
Ama itokee vita, Jeshi waingilie kati/
Chanzo ni ikulu/ thamani zaidi ya lulu/
Vikosi unaviamuru, na bado hulipi ushuru/
Unapangia wengine, bila kujua hali zao/
Wafanye kazi kama mashine, uchukue kilicho chao/
Fungu wamimine, kujua matumizi si kazi yao/
Na wakileta mengine, ni wachochezi hao/
Ila wapo pia, viongozi bora kwenye duru/
Mungu azidi kuwajalia, na husda awanusuru/