Michano/Hiphop/Freestyle

[emoji419]
 
Humu tunadumu wagumu kwenye bato../
Usifuate mkumbo kama mateka wa freemason../
muulize Mvumbo navyo'ogopeka kama nato../

Wajinga wanavimba kwa mistari ya chabo../
Wakiotea wanaringa, utaskia mi ndo rapgod../
 
Haunipi raha, nikitizama zambi zako/
Iweje unaishi dar na hupajui cambiaso/
usihukukumu kama huijui kesho yako/

Natema bars kwakujiamini coz am dangerous/
Huwezi kuwa kama mimi labda uwe mimimars/
Vichwa panzi nawashusha chini kama chupi ya manzi/
na kabla hawajifika chini nawachana bila ganzi/
 
Usilete busara kwenye vita../
Ukitaka utajiri wa kimasihara, jitoe kafara 666../

Kila idara napewa sifa, kama simba wa mbagara anavyoshine insta../
Na bado sitaki ustar, wala machawa kabsa../

Nachohitaji ni kufika far, nakuona hip-pop inapaa kimataifa../

Sina info za michapo kama mange../
Ila nina bonge la nako so wenye punch-laini wajipange../

Namwaga madini, underground muyapande/
 
Unavo chana madogo wanakimbia/

Punch nzito mdundo heavy zaid ya magunia,
ya mpunga, ama pumba natania/

Kwa hizi flow mapunga, waoga wanakimbia/

Hawakai humu kwa hiz ngumu tunazotema/

Huu mdundo wa kigumu bila ndumu hautosema/

Nitawazika wote RIP walale pema/

Kwa hizi flow kali mpaka bubu atasema/
 
Penye amani upendo unatanda..|
Tangu zamani hawagusi hizi anga..|
Veteran kwenye huu mziki usiobamba..|
Underground nae-shine gizani kama shetani au mwanga..|
Nalinda culture utasema bowseman wakanda..|

Masera Vichwa maji na mimi haziivi/
Ni sawa na kum-compare De Opera na prof shivji/
Kunidisi sio rahisi kama kukata div/
We endelea kutema shit utadhani chizi..|
Ila jua huniwezi ata uvae hirizi..|

Huwezi badili mwendo hata uvae buti..|
Unajiona tembo wakati unapigo za pusy pusy..|
Kiufupi na kuona mrembo yaan byuti byuti..| (na)
ukitaka skendo nakugeuza amberuty..|
 
Umeni-poke nikakubali nimejileta,
ku-check tungo yaani zote ni utata,
umeshuka kiustadi na matata,
napiga mbinja kiukweli umenipata.

Wasanii hawana budi kukufata,
maujuzi mistari unavoikata,
nasema waje tu haraka wasije nyata,
wasichelewe iskariot tamkuta.

😀😀😀
 
Anytime niko tayari kutema mistari/
navyowachana utasema mpo hospitali kufanya surgery/
Natem punch-lain ila ni heavy zaidi ya jabari/
Amini Usipoelewa haya madini we ni ndezi kama mjomba nchomar/
 
Anytime niko tayari kutema mistari/
navyowachana utasema mpo hospitali kufanya surgery/
Natem punch-lain ila ni heavy zaidi ya jabari/
Amini Usipoelewa haya madini we ni ndezi kama mjomba nchomar/
😅😅 You killin! 🙌🏾
 
Humu tunadumu wagumu kwenye bato../
Usifuate mkumbo kama mateka wa freemason../
muulize Mvumbo navyo'ogopeka kama nato../

Wajinga wanavimba kwa mistari ya chabo../
Wakiotea wanaringa, utaskia mi ndo rapgod../
Hii nimechelewa kuiona, kama kobe kwenye Mfungo/

Ni kweli mitaa inapona, inaposikia zako tungo/

Ni wengi wamekula kona, maana tunawapiga mtungo/

Hatuchani tunashona, kama wasusi wa ungo/

Hii sio tatu chafu/ hii ni mbombo ngafu/ watapasua mapafu/ ni ngangari zaidi ya Cuf/

Hapa Mvumbo hapa Yuda/ ni vifungo kwa waluga/ tungo kila muda/ pungo kwa wajuba/

Hip Hop iendelee, una Rhymes andika huku/

Ili Vipaji visipotee, kama mkojo wa kuku/
 
Yatapita Remix

Verse

Shida hazikimbiwi, mwenzako pesa ninazisaka/

Kesho yetu haitafsiriwi, kwa hizi nguo za viraka/

Viatu watapaka Kiwi, na kujifanya wanakutaka/

Ila nyuki hakumbatiwi, usijaribu watakung'ata/

Mbele ni ukungu, tulipo pana moto/

Ila na sisi tuna Mungu, na sisi tuna ndoto/

Mateso na kushuka hadhi/ mbeleko sina kazi/

Leso kama una kibanzi/ kesho bado haijafanya kazi/

Tunaisubiri kwa matumaini/ ila hatujui tutapata lini/

Tumebadili mpaka dini/ na bado tupo chini/

Chini ya bajeti ya Mtanza, wenzetu wapo fiti/

Insta ni ya kina Boma Liwanza, Kokobanga Gademiti/

Unasema nasema yatapita, mbona hayapiti/

Bado tunahangaika, na hatuna ridhiki/

Mama maisha ni vita, najua vingi unamiss/

Rabda ni fungu la sita, la saba tutakuwa sisi/

Ipo siku tutafaidi, mpenzi wangu vumilia/

Giza linapozidi, jua asubuhi inakaribia/
 
Natokea mitaa ya maskini..|
kujitegemea sio mpaka ufike miaka ishirini..|.
Ulicho nacho kithamini, kabla ya wanaokitolea macho hawajakufitini..|.

Ukifika kwetu kuwa makini..|.
Mademu wanauza nyeti wakati vyeti wameficha kabatini...|

Kwetu hatuli baga zetu chukuchuku..|
Kwetu usiulize mambo ya ibada wala utukufu..|
Watu wapo busy na udaku wa watu maarufu..|

Mademu wanatembea utupu bila hofu..|
Aliesema hakuna jipya, nadhani alikuwa kipofu..|
 
Kwenye haso sina utani, navuja jasho ili nivute money..|

Sina demu kwani mapenzi kitu gani..|
Mashemu wananitega kishenzi ili niwape korodani/
wanakuta mnyamwezi sina hisia kama natumia mjani..|

Naishi kwenye kizazi cha walafi na majizi..|
Naishi kipweke utadhani mkimbizi, sina mtetezi yoyote kama mwizi..|
Sina chochote kiufupi sijiwezi..|

Nshajaribu kwenda kwa waganga..|
na bado sikuona mwanga zaidi ya visanga..|

Nkaishia kutangatanga kwenye nyumba za kupanga..|
Sina mshauri , Kila nachopanga kinageuka sifuri ni majanga..|
Napiga puri toka skul, maana sina mchumba wala danga..|
 
Niko live! Simba washapigwa kimoko na Holoya/

Makavu live! Inonga anazungushwa tu kama boya/

They won't survive! Chama mpira kizembe anapokonywa/

Lile bichwa la kudaiv! Ndio sababu makolo midomo omeshonwa..

Sent from my M2006C3MG using JamiiForums mobile app
 
Maji ya gundu maji mfu, ni maji ya maiti/

Haufai kurusha turufu, ushazikwa saiti/

Vipi kinyago wa sufu, anitishe Mwenye kiti/

Hata uumbwe maradufu, huuwezi huu mziki/

Una vya kitoto vina, Mvumbo natupa kule/

Niamkie kwa heshima, kama nakupa hela ya shule/
 
Wanajiita Visit vibonde..|
Waana kocha la misifa gadiola kibonge|
Logo inatisha ila mpira wa kinyonge..|
Jana wametandikwa kimoko cha ng'ombe..|
 
salamu sio heshima ata mashoga hufanya/
nimerudi tena kwa vina bwana mdogo kukukanya/
mi ndo title la hii rap huna kipya cha kufanya/
unajitia ununda ila kwa ndani unahanya/

mwenye kiti mwenye siti chukua kiti kalia/
mwenye beat leta kati huyu mtoto atalia/
mwenye kiti mwenye dhiki ukiweza kimbia/
sina kick kwene hiki niko fiti ukiniona potea/
 
Kila story ushoga/ nidhamu ya uoga/ au unatangaza soko/

Tujue unatoga/ mtoto ni mboga/ ile Kiarabu koko/

Acha soga/ umeshaniroga/ nikupige kimoko/

Si utaoga/ na ukishanipa boga/ sitafanya unoko/

Umeweka maji wazi tunanawa bila ganzi mtoto wali nazi nakupanda kama ngazi/

Usitangaze ubazazi naonekana ustadhi utanishusha hadhi wakijua wazi nimekupakua mbaazi/

Imeshakuwa ndefu meku nipe mambo yetu peku kama Mpoto/

Nakudeku unavyo 'repu' mwanakwetu unataka moto/

Game imekupuuza, stanza sio kuvaa wigi/

Ni wazi unajichuuza, kujaribu hii ligi/

Wanasema Mvumbo punguza, konokono hawezi hii speed/

Sasa badala ya kujifunza, unaleta mdomo kama Gigy/
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…